Naomba kufahamishwa kiwango cha elimu ya Rais Samia Suluhu Hassan

Inaonesha unayo CV yake tunaomba tuletee hapa kwa ufasaha ili tunufaike.
mimi inachonichosha elimu ni kitu kimoja tu, yeye asiye na elimu kama wewe ni raisi wa nchi sasa na taifa lote linamsikiliza yeye, mkiwemo na nyie, wakati huo huo nyie mko humu saa hizi hoooi bin taaaban mkihangaika huku ye akiwa hajui tu na wala hahitaji kujua (sababu hamna impact yoyote) kama kuna mtu au watu wanaongea......
 
Kuwa Rais wa Tanzania siyo lazima uwe na Degree.

Degree ni upumbavu mwingine usio na maana yoyote.

Note: Sijasema anayo au hana: Ila degree karne hii ya 21 siyo issue. Dunia iko kwenye SKILLS na PERFORMANCE.
Karume snr degree alikua hana na alikua rais
Sembuse ssh
 
Mtu mwenye degree akiongea huonekana tu... Elimu hua haijifichi.
 
Ana advance diploma ya public adminstration ya mzumbe wakati huo ilikuwa ni chuo sio chuo kikuu
 
Nyerere hakuwai kuwa na degree, soma historia yake. Pia katiba ya Sasa sidhani Kama imetamka elimu ya rais. Katiba pendekezwa ndio Ina hicho kigezo
 
Wewe unademka😅😅
 
Alisoma mzumbe advanced Diploma. Alisoma Masters kwa equivalent qualification.
 
Na mwenye elimu ndogo zaidi?

Nenda kwenye mitandao kama Google kasome historia ya kila mmoja utaona pale, usilete pumba hapa! Hadi unauliza pumba hizi wewe elimu yako ni darasa la ngapi hadi unashindwa ku-google!
 
Yule jamaa sijui alipataje PhD? Kwangu mimi bila kujali kiwango cha elimu, marais vichwa walikuwa ni Julius, Benjamin na Jakaya!
Julis & Benja hapo kwa mkwere piga chini mmmmmbruuuuuu hamna kitu
 
Nimeanza kupata mashaka na elimu yake mkuu sababu Kuna dalili mbaya nyingi kuwa huenda kiwango chake hakiridhishi
Yaani serikali ishindwe kuona hizo dalili uje kuona wewe?

Kitendo cha wewe kushindwa kujua elimu ya kiongozi mkubwa tayari uwezo wako wa kufikiri na elimu yako vinatia shaka.

Hizi dalili ilibidi uzinotice kwako mwenyewe kabla ya kwenda kwa kiongozi na mtu mkubwa africa.
 
Inabidi akomae kweli. Tanzania ya wasomi na wajuaji kibao. Mambo ya vidole juu siyo sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…