Madam B, kuna meeengi yanayosemwa haswa ulaya kuhusu hiyo picha ya Mona Lisa
"(My lady Lisa in Italian)" yenye miaka 500 hivi sasa.
Watafiti wa Uingereza mpaka mwaka 2011 walikuwa wanatafuta ukweli kuhusiana na siri za picha hiyo na hata wamarekani.....google utaelewa!!!
¤ Miongoni mwa fictions /facts zake ni kuwa:-
- Kwanza rangi nyeusi ya nywele za bibie huyo ina maana yake kuwa nyeusi na iliindicate aina ya cheo
-Pia Rangi ya kitambaa cha nguo aliyoivaa na style aliyokaa ilimaanisha utawala wa kifalme (ndio maana anahusishwa na Yesu aliyetoka kwenye ufalme wa Daudi) hivyo kuwafanya wengi kuamini alikuwa na uhusiano na Kristo Yesu.
-Nyingine ni namna picha hiyo ilivyo yaani tabasamu la Mona Lisa kuna jina lilitungiwa kabisa wakimaanisha inaashiria furaha na huzuni kwa wakati mmoja
-Pia jicho la kushoto katika picha hiyo na mdomo inafanya picha hiyo kuwa ya Mwanaume pia si ya mwanamke tu.
-Mwisho na ambayo ni siri kubwa zaidi iliyowachanganya watu ni kuwa picha ya kwanza kabisa ya da Vinci ilikuwa na Codes ndogo sanaa na ilipochinguzwa kwa makini sana na kiteknolojia ikagundulika kuna maandishi ambayo:
Katika jicho la kulia pameandikwa LV ikimaanisha jina "Leonardo da Vinci"
Katika jicho la kushoto pia kuna mchoro wa ramani ya siri (haijaelezewa)
Na katika uso mzima pia kuna codes zingine ambazo hazijatafsiriwa vizuri mpaka leo ukiacha kwny kitabu cha Da Vinc Code. By Dan Brown
Hii picha ipo Ufaransa na zimeshachorwa picha kama hizo zaidi ya 300 na kuwekwa kwenye makumbusho ya mataifa mbalimbali.
Mwaka 1963 ilipelekwa kwa Meli mpaka Marekani na Rais J.F Kennedy pamoja na raia 1.7 million walipiga nayo picha.
Ni picha iliyochorwa kwa miaka almost 12 bila kukamilika, 1505 - 1517, na da Vinci alipoenda france aliibeba hiyo tu kati ya picha zake zote alizochora.
Mbali na hiyo, picha nyingine maarufu na nzuri sana ya da Vinci ni ile ya Karamu ya mwisho ya Yesu Kristu, japo nayo ilitungiwa uzushi kuwa maria magdalena akijuwa miongoni mwa wanafunzi wa Yesu.
Hayo ndio yanayosemwasemwa.
Naa
View attachment 426871View attachment 426872mini umeelewa kwa sehemu kubwa.