Naomba kufahamu changamoto katika usafirishaji kwa wafanyabiashara

Naomba kufahamu changamoto katika usafirishaji kwa wafanyabiashara

Joined
Mar 8, 2021
Posts
6
Reaction score
12
Habari wana JamiiForums,

Mimi ni mtaalam wa kuunda software za simu na kompyuta. Natamani kutengeneza mfumo wa logisitics/delivery ambayo itagusa kila mfanyabiashara ambaye biashara yake inafanya delivery ndani na nje ya mkoa husika. Sijaona mifumo inayogusa maeneo hayo moja kwa moja.

Sanasana tunaishia kuwatuma boda na kukodi kirikuu iliopo karibu. Natamani nitengeneze mfumo ambao utarahisha eneo la logistics kwa kila mfanyabiashara.

Natanguliza shukrani na kuahidi kufanyia kazi mawazo yenu.
 
Wazo zuri, endelea kutia nia… bali nyie watu wa IT mnaboanga kwa kweli!

Kuna mwaka nlikuwa kwenye group la IT huko fb nlikiwa na wazo la kuundiwa app ya board game (drafti) kwa ajili ya wacheza bao woote nchini na hyo nliwaza kama angepatikana muundaji tungeunda app tofauti na zilizopo online na offline ila nlichokutana nacho ni ubabaishaji wa BEI tu.


Hilo group la IT huko fb saiv limejaa wakodishaji muvi (wamiliki library)
na wahariri picha.
 
Wazo zuri, endelea kutia nia… bali nyie watu wa IT mnaboanga kwa kweli!

Kuna mwaka nlikuwa kwenye group la IT huko fb nlikiwa na wazo la kuundiwa app ya board game (drafi) kwa ajili ya wacheza bao woote nchini na hyo nliwaza kama angepatikana muundaji tungeunda app tofauti na zilizopo online na offline ila nlichokutana nacho ni ubabaishaji wa BEI tu.


Hilo group la IT huko fb saiv limejaa wakodishaji muvi (wamiliki library)
na wahariri picha.
Kutengeneza app ni kazi ngumu sana, utaenjoy mwanzoni unapoanza carrier lakini kadri siku zinavyozidi kwenda na kutengeneza project kubwa akili inachoka sana kwasababu kazi ya kutengeneza software ni kazi usiofanya kwa uzeofu kwasababu kila project ina namna yake ya kuitengeneza na pia inabidi ulewe biashara husika ya mteja wako.

Factor nilizoainisha hapo juu ndo inafanya bei kuwa juu, na pia clients huwa wanaleta shida sana kwenye malipo baada ya kumaliza kazi. Mara nyingi wateja wetu huwa wanataka kuongeza vitu vingi ambavyo havikuwepo kwenye makubaliano tokea mwanzo ndipo mvutano unapoanzia.
 
Back
Top Bottom