Mkuu, siku ukija kugundua Sub-Conscious Mind na power yake utagundua kiini cha imani zote, matendo yote, na matokeo yote ya kazi za mwanadamu.
Mind ya mwanadamu imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni CONSCIOUS MIND na SUBCONSCIOUS MIND.
Conscious mind kazi yake ni kutumia milango ya fahamu kutafuta maelezo na pia kazi yake ni kujaribu kukusaidia uweze kupata maana ya vitu. Ni sehemu ya Mind inayojua wakati/time. Ni sehemu ambayo taarifa zako tangu ulipozaliwa na tangu ulipoanza kujifunza hii dunia ilivyo taarifa zake zinawekwa kwenye sehemu hii.
Subconscious Mind, ni sehemu isiyo na mipaka. Ina asilimia kuwa ya akili yako lakini unaitawala kwa kiasi kidogo sana. Tafiti zinasema wapiga vifaa vya mziki, walimu wa imani, enlightened Beings, na watu waliofunguka ufahamu wanaweza kuiongoza kwa kiasi zaidi. Ni sehemu isiyojua wakati, haijui ubaya wa vitu na haiwezi kuhukumu unachokiamini. Ni sehemu ambayo kazi yake ni kuongoza matendo ambayo wewe huyajui kama vile mapigo ya moyo, kiasi cha sukari n.k. Ni sehemu ambayo ipo kukusaidia. Mfano unaweza ukajisemea nataka niamke saa 11 asubuhi. Huku ukisema hivyo unaamini kuwa lazima uamke kwa sababu unasafiri. Utaona asubuhi lazima uamke (ilishawahi kunitokea) hata kama ukiwa hauna saa unaweza ukaamka mapema tu na usingizi huwa unaisha. Subconsious mind inakusaidia pia ukiwa katika hatari kwa kukupa akili ya ziada. Ni sehemu ambayo wazo likipita kwenye conscious mind na ukalikubali na kuamini linaamia kwenye upande wa subconscious na linaanza kufanyiwa kazi.
Tukirudi katika mada ya uchawi. Mwanadamu anaweza kuumba au kufanya jambo lisilo na mpaka hata wa kisayansi. Mchawi anapofanya matambiko, kafara, chants, kuimba au na madoido mengi kazi yake ni kujitengenezea imani na kuanza kuamini jambo (hapo linaamia kwenye subconscious na linafanyiwa kazi). Pia ni sawa na wanaosali, wanaorudia rudia sala, kutumia rosari, meditation, yoga na vitendo vingi vya kiimani vinamjenga mtu subconsciously bila yeye kujua kuwa anajengewa imani.
Asante.