Naomba kufahamu Madhara ya kupeana talaka baada ya ndoa Kuvunjika

Kama unaitaji kutua mzigo ulobeba moyoni mwako pasipo kujali madhara yake,Basi mwambie tu ili upate amani.
 

Mazara ni makubwa sana kwa viumbe visivyo makosa
 

Kuishi nao kwa akili ni pamoja na kutomwambia hicho kitu
 
Sijui ni dini gani ila kwa Mungu kuna amani. Najua unaitaka amani ila amani ya kweli ipo kwa Mungu pekee. Rudi kwake muombe muobgozo. Hapo kuna maisha ya viumbe wawili. Pia kuna maisha yako hasa nafsi itakavyojutia ikiwa utaachana na mkeo. Mimi nina changu japo sio cha ndoa. Nilienda kwa Mungu nikamuomba nikimaanisha sitarudia tena. Huwa Mungu anahuruma mno. Alinisamehe na kuonesha anakupa amani kuu. Shetani atajaribu kuichukua ila ukisimama na Mungu hawezi. Ndio umekosa ila kuivunja ndoa ni kosa kubwa mno. Maadam hujaua kiri kwa Mungu, utafute uso wake atakupa majibu yake.
 
Siku zote Na Mara nyingi wanawake ndio huanza kuomba talaka. Kama humtaki, tengeneza mazingira aiombe.
Majukumu yako yatakuwa pale pale mf. Kuhudumia watoto Na hata yeye pia kama ambavyo Mahakama itaamua.
Pia jaribu sana kuwa amicable - yaani anza kujitoa pole pole, ukojotoa haraka Na yeye hataki au hayuko tayari- mtiti wake si wa mchezo...
Watoto ndio huathirika zaidi. Na wewe pia itakuathiri Mara tu akiangukua Kwa mkunyenge mwingine halafu unapangiwa masharti ya kuwaona watoto wako...lazima utagundua tu...
 
Iseme hiyo siri, kuna wenye busara zao humu kina Mshana Jr ERoni Watu8 Glenn Heaven Sent watakupa ushauri mzuri wa a way foward.

Niliposoma uzi mwanzo kwa namna alivyoandika kwa vificho nilidhani labda jamaa kaamua kuwa choko...

Kumbe mwamba kaongeza familia na anakuwa muoga muoga...

Kitu pekee naweza muhakikishia ni kwamba ajiandae kumpoteza huyo mke wake wa miaka 8 ya ndoa...
 
mkewangu ni mtumishi wa serikali hapa canada kwenye mambo ya women and Girls empowerment
Je mkeo ni MTanzania au MCanada wa kizungu, na wewe umeshachukua uraia wa huko Canada ? ili upewe ushauri vizuri na wadau.
 
Kumbe ni jizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…