Naomba kufahamu wizi wa magari unafanyikaje

Mimi niliibiwa gari mwezi 12 mwaka 2020,
Ndani ya geti walivunja kioo cha gari na kutoa lock.naamka asubuh nakuta vipande vya kioo tuu chuma haipo na ilikua bado mpwa
 
Mimi niliibiwa gari mwezi 12 mwaka 2020,
Ndani ya geti walivunja kioo cha gari na kutoa lock.naamka asubuh nakuta vipande vya kioo tuu chuma haipo na ilikua bado mpwa
Wezi wanaakil nying sana,yaan wamevunja gari na wakavunja na geti afu hakuna aliesikia,tuwe tunafuga mbwa kumbe znaweza saidia japo kdogo
 
Mbwa anaweza akasaidia kidogo sana kwa mwizi ambae hakujiandaa kukutana n mbwa, mbwa anamalizwa kimya kimya bila kelele mwizi hapo hana kipingamizi, fungeni PIR motion sensor makwenu, zungusheni nyumba nzima movement au motion yeyote inawasha alarm yenye sauti kali hata huyo mwizi nae atashtuka maana sensor waweza zificha zisionekane, teknolijia ndio mbadala wa hao mbwa
Wezi wanaakil nying sana,yaan wamevunja gari na wakavunja na geti afu hakuna aliesikia,tuwe tunafuga mbwa kumbe znaweza saidia japo kdogo
 
Sio hadi kuchonga tu finguo kama ya gari yako! Wana finguo kibao
 
Umakini kaka
 
Sasa hivi kuna wizi mpya wana chukua spare parts za maana na ktk gari ya maana, Wana ingia ndani ya uzio wa nyumba yako uliko paki gari. Wana fungua kila kitu na kuacha skeleton car alafu wana sepa. Nitakuja tena kuwajuza jinsi wanavyo fungua mlango na bila alarm kulia.
 
Halafu anaitumia wapi hiyo gari?
Wanaweza wasiitumie, bali wakaibucha (wakaitawanya) then mlango unauzwa Tegeta, Engine shaurimoyo kwenye used spares, Rimu Temeke kwa waziba pancha, vikorokoro vingine vitatawanywa kwa mujibu wa vinauzika maeneo gani
 
sa ivi wanang'oa spare parts tu, wanakuachia chesisi
 
Ili uepuke wizi was gari Fanya haya
1.gari yako usiwe unampa mtu unaweza mpa akachonga funguo na anakujua inakuwa rahisi kuibiwa
2.kama hakuna ulazima was kuosha gari nunua sabuni OSHA ww mwenyewe kama imeshindikana basi peleka uoshe lakini uwepo
 
Sio hadi kuchonga tu finguo kama ya gari yako! Wana finguo kibao
Mafundi umeme wa magari wanaweza washa gari bila funguo wezi wakifanikiwa kufungua mlango wa gari hasa wa dereva.

Kwa alam za magari wanatumia kitambaa kushika bonet kufungua na kuchomoa betri alarm apo haiwezi fanya kazi tena.

Cha msing kama mdau alivosema kufunga motion sensor ambazo pia n bei rahisi sna ukienda africable wanauza 30,000+ kingora nlinunua kariko 40,000 na taa moja 17,000 umemaliza kazi ukiongeza na car track kidogo ulizi utakuwepo
 
Mimi nmekua mhanga wa ukibiwa gari so nmefanya research za kutosha ili nisije rudia kosaa na wizi mwing unafanyika usiku kuanzi saa 8 so mda huo wez wanajua watu wamechokaa kuhusu funguo mi naona kwa sasa technology imebadilika sana.
Nimeandika haya ili yasije watokea na wenzangu inauma sana kuibiwa!!! Japo nlikata bima comprehensive na nmelipwa
 
Cha msing kama mdau alivosema kufunga motion sensor ambazo pia n bei rahisi sna ukienda africable wanauza 30,000+ kingora nlinunua kariko 40,000 na taa moja 17,000 umemaliza kazi ukiongeza na car track kidogo ulizi utakuwepo
Mkuu hii si unafunga kwenye gari ama kwenye nyumbani ndani ya geti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…