Naomba kufundishwa mbinu za kuepuka watu wa Jumuiya na Parokia

Mkuu kwa pole sana masikitiko mengi sana.

Kwanza ujue sala sio kwa ajili ya padri, katekista au wanajumuiya Yako ni kwa ajili Yako mwenyewe.

Ukiongoka ni wewe Wala sio mkeo na watoto wako Bali ni nafsi Yako.

Kama hutaki kwenda kanisani au jumuiya kwa maana huamini kwenye ukristo usione aibu. Kawaeleze paroko wako ila nawe usitegemee huduma ya kiroho kutoka kwao endapo utabidili msimamo. Maana lazima ukakiri Imani upya kabla ya kupewa huduma.

Huhitaji kuomba eti kukwepa jumuiya na paroko. Kuna mawili TU shiriki ama jitoe. " Aidha baridi au Moto hakuna vuguvugu"

Huyu hata hahitajiki kwenda SDA, Wala KKKT au pentekost maana kasema haamini kwenye ukristo au Uislamu lakini anasema anataka kukwepa jumuiya na mapadri.

Tangaza Rasmi kwa familia Yako na viongozi wako wa kiroho wewe sio mkristo Tena. Hapo unaona aibu.

Ukisikia aibu na ukaona huwezi kufanya basi jua Bado ukristu upo ndani Yako. Fanya jitihada kuokoa nafsi yako
 
Ndiyo naondoka hainiingii kichwani mifumo ya bahasha na michango yenu ambayo haina tija kama huyo Mungu yupo ROMAN CATHOLIC basi ataniua maana nimeijua kweli kuwa Dini ni wizi ambao umejikita mizizi yake kwenye vichwa vya waoga na wenye roho nyepesi
 
Ungekuwa kitandani unapambania uhai, usingeandika huu upumbavu!!
 
Wahindi wanachomwa moto unataka kuniambia kuwa adhabu ya moto itawahusu tena
Tatizo lipo kenye utamaduni; ndio maana tunavaa suruale miguuni na si kichwani, ila ukivaa kichwani utaonekana chizi ingawa kila mmoja ana uhuru wa kuvaa mavazi.
Kwa hiyo kuanzisha utamaduni mwingine kama pendekezo lako lilivyo, inaweza kuchukua miaka mingi mpaka jamii kuukubali.​
 
Jumuiya ni sehemu ya ziada kupata mapato niliachaga mara moja baada ya siku kulazimishwa kuchangia kias ambacho walitaka wao siku nilikaa chini nkapiga hesabu kias cha pesa nachopeleka kanisani pekee ndio nilipoona hapa sitaendelea, kiongozi wa jumuiya alipoleta bahasha siku chache baada ya kurudisha ya kwanz nikamtimua mbio mbaya zaidi tulikuwa tunachangia ujenzi wa kanisa ulitakiwa kukamilika miaka miwili ilopita ila viongozi wakapiga hizo pesa. Mimi nani nipate dhambi nikigoma kuwafaidisha watu kwa kigezo cha dini sadaka yangu nishasema nitatoa physically kwa wale walemavu ninaokutana nao njian hawanipangii kima na wananishukuru sanaaa na pia natoa nikiwa roho imedhamilia na ninafurahia kabisa.
 
Biblia historia ya wayahudi,coran historia ya waarabu nyingi watu weusi historia yenu iko wapi
 
Ndiyo naondoka hainiingii kichwani mifumo ya bahasha na michango yenu ambayo haina tija kama huyo Mungu yupo ROMAN CATHOLIC basi ataniua maana nimeijua kweli kuwa Dini ni wizi ambao umejikita mizizi yake kwenye vichwa vya waoga na wenye roho nyepesi
Martin Luther aliondoka na kanisa limeendelea itakuwa wewe nenda mwanakwenda
 
Martin Luther aliondoka na kanisa limeendelea itakuwa wewe nenda mwanakwenda
Na wewe baki na ukondoo wako ukistuka kuwa unaliwa utanifuata kwa ushauri.
Kuna siku niliitwa kwenye Harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Sundey school ya parokia nikaropoka bundle mbili za bati na kweli walinikomalia nikazipeleka tena walikuwa na kigezo kuwa wanataka kampuni ya ALAF na inatakiwa tupeleke hela nikapeleka milion moja ikaja siku nikasema ngoja niwatest nikachelelewesha ada coz mtoto wangu yupo pale anasoma shule ile ile si wakanipigia simu na wakamrudisha aisee NILIGUNDUA KUWA WANATUONA SISI NI NG'OMBE ZA KANISA WHY MIMI NA HISA YA KUCHANGIA UJENZI WA SHULE ALAFU KUCHELEWA KIDOGO TU KULIPA ADA DOGO AKARUDISHWA
 
Ungekuwa kitandani unapambania uhai, usingeandika huu upumbavu!!
Alipambania uhai papa Paulo wa pili akafa sembuse mimi.
Nani kakuambia kutia huruma mbele za bwana ndo kinga ya mabalaa ya maisha yako.
Haijalishi una wema gani ikifika muda wa kupatwa na balaa unapatwa tu hata unajiona una Mungu sana.
TB Joshua yupo wapi na kujifanya alikuwa anaokoa uhai wa watu ina maana MUNGU alimkaushia au?
 
Ndio maana hujui nini maana ya kanisa, sasa wewe unataka Utoe pesa upate Vitu kwa kanisa . Kanisa haliendi hivyo, kanisa kwa maana hasa ya Imani linakusaidia kwenye mambo ya kiroho yanakuwezesha kupata Baraka zinazokuwezesha kupata Mali na vitu vitakavyokuwezesha kuendesha maisha. Vitu au Mali haviwezi kumtosheleza mtu ila mtu anatosheka kwa Mungu tu. Kanisa linaendeshwa na waumini kwa Michango Yetu.
 
Njia rahisi ni kuwakwepa kwepa kijanja hivyo hivyo. Ikitokea event yoyote unatengeneza excuse usijumuike nao ingawa usiache kwenda katika ibada. Mwishoe watachoka na kukupotezea. Kwetu sisi introverts ni kazi rahisi mno hiyo.
Hizo ibada ndio kasema hataki kujumuika pamoja
 
Hakika umenena vyema Mkuu Ndio maana YESU alisema hivi πŸ‘‡


Yohana

4.20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia.


4.21 Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.


saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.πŸ‘‰ Kumuabudu MUNGU Sio swala la mahali fulani hapa ndivyo YESU alivyomaanisha, kwamba sehemu fulani ndipo mahali pa Kumuabudu MUNGU Baba yetu Wakati unakuja haitakua hivyo


Kiukweli kuna tofauti kubwa kati ya dini na ufalme wa MUNGU na dini zimetukalilisha Kwamba kumuabudu MUNGU ni kanisani au SEHEMU fulani something wrong kiukweli MUNGU anaiabudu NDANI ya MTU na kila second inayopita ni ibada katika ulimwengu wa Roho inategemea na Nini unawaza au kufanya ndicho kinacho determine ni Aina Gani ya ibada unafanya Kama ni ibada mbele za MUNGU wa Kweli au ni ibada ya sanamu


Yohana

4.23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu.


4.24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli

(MUNGU ni Roho) Roho mtakatifu ni MUNGU katika Roho na mtume Paulo alisema haya


1 wakolintho

6.19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;


6.20 maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.


mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu πŸ‘‰ Hekalu ni nyumba ya Bwana


Kwahiyo tunajifunza hapa kwamba MUNGU anaabudiwa NDANI ya MTU na ni swala la kila wakati , kila muda na kila Siku kwa Mawazo na Matendo ya MTU 😊


Ndio maana mtume Paulo akasema πŸ‘‰Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu.


Zao la ibada yoyote ni utukufu kwa lugha NYEPESI hapa tunaweza kusema basi muabuduni MUNGU katika (NDANI ya) miili YENU


Wakolosai

3.5 Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu;


hapa Paulo alitaja Mfano wa Matendo na mawazo ambayo tunayatenda na kuyawaza NDANI yetu ambayo si ibada mbele za MUNGU wa Kweli bali ni ibada ya sanamu na kama ni ibada ya sanamu basi utukufu ni kwa ibilisi


wanao tenda na kuwaza Hayo yote Hapo juu kumbe wanafanya ibada NDANI ya miili Yao lakini Sio ibada ya Roho na ya kweli mbele za MUNGU Baba na YESU KRISTO Bwana wetu 😊



Ndio maana YESU akasema πŸ‘‡



"Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli" πŸ‘‰ na Sio mahali Fulani au SEHEMU fulani


Miili YETU ni hekalu (nyumba) ya MUNGU Kama ni nyumba ya MUNGU huko NDANI ndipo ibada inapo fanyika kila wakati na kila Siku kwa Mawazo na Matendo YETU na Sio mahali au SEHEMU fulani


Lakini tumepotoshwa Kwamba kumuabudu MUNGU ni mahali au SEHEMU fulani kumbe ibada ni kila Wakati, kila Siku na Ndio maana watu kama hawa wanakuja na kuanza kumdhihaki MUNGU B'se badala ya dini kuwawafahamisha Kweli ya MUNGU dini zinawalazimisha kutoa Pesa masikini πŸ™†πŸ»β€β™‚οΈ


Inaumiza Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…