Siku hayo magari yakiondoka na pesa nayo ikaondoka utawatafuta watumishi wa Mungu kwa bidii. Pia ukizeeka ndio utaanza kumtafuta Mungu. Na ukifa ndio utaanza kwenda kanisani na kwenye jumuiya ili uzikwe na Kanisa.
Mungu yupo, tofautisha ubabaishaji wa wanadamu na uaminifu wa Mungu. Sapoti Kanisa lako kuna faida za kuwa mwanachama huko ila angalia pia usibaki kwenye mambo ya kidini tu, faidi nguvu za Yesu na mambo yake mazuri kama ulinzi na mengi mengine. Jifunze zaidi MAARIFA YA KIROHO, usibaki kwenye mazoea ya dini pekee, yanaua!