Naomba kujibiwa haya maswali kuhusu Maiti

Naomba kujibiwa haya maswali kuhusu Maiti

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Hope mmeamka salama. Naomba anayejua anisaidie na mimi kujua÷

1. Kwanini mtu akifa anaoshwa?
Anazikwa ardhini na kufukiwa sasa huo usafi anaofanyiwa unamsaidia nini as long as atachanganyikana na mavumbi soon?

2. Mtu akishazikwa baada ya miezi au miaka kadhaa ndugu huanza kwenda kufagia kaburi lake tena wanapiga deki kabisa. Hii inamsaidia nini mtu aliyeoza kaburini?

3. Kuna nadharia kwamba tutafute pesa ili tukifa tukumbukwe, Maiti huko iliko inapata faida gani ikikumbukwa na walio hai kwa mema iliyotenda? Mfano Mengi anapata faida gani kukumbukwa na walemavu ambayo Maiti ya kimasikini haipati?

Mshana Jr na wengine njooni mnisaidie kuelewa haya mambo.
 
Hope mmeamka salama.Naomba anayejua anisaidie na mimi kujua÷

1.Kwanini mtu akifa anaoshwa?
Anazikwa ardhini na kufukiwa sasa huo usafi anaofanyiwa unamsaidia nini as long as atachanganyikana na mavumbi soon?

2.Mtu akishazikwa baada ya miezi au miaka kadhaa ndugu huanza kwenda kufagia kaburi lake tena wanapiga deki kabisa.Hii inamsaidia nini mtu aliyeoza kaburini?

3.Kuna nadharia kwamba tutafute pesa ili tukifa tukumbukwe,Maiti huko iliko inapata faida gani ikikubwa na walio hai kwa mema iliyotenda?Mfano Mengi anapata faida gani kukumbukwa na walemavu ambayo Maiti ya kimasikini haipati?

Mshana Jr na wengine njooni mnisaidie kuelewa haya mambo.
Sikukuu za mwanadamu ziko tatu KAGAMEE
Ya kwanza ni kuzaliwa
Ya pili harusi
Ya tatu kifo
Tukio la sikukuu linajumuisha kula, kunywa, kuvaa vizuri nk.. Na ndio maana kuna nguo zinaitwa za sikukuu

Makaburini sio sehemu baki la hasha pale ni makazi ya wafu, hivyo panastahili kuhudumiwa kama makazi mengine japo si kila siku..

Kukumbukwa ni legacy, je maisha yako hapa duniani uliyaishije? Umeacha nini? Huu husaidia wengine kwenye mapambano ya maisha nknk
 
Asante kaka.Kumbe legacy kuwafaidisha wanaobaki.
 
Ukweli yote tunayofanya kwa maiti ni kwajili yetu sisi wafanyaji na sio hiyo maiti. Maiti haitajua imeoshwa, au imepaliliwa kaburi. Kifo ndio mwisho.

Lakini Sisi bado tunauona ule mwili wa marehemu kama sehemu ya marehemu, na kwa vile wote tunaogopa kifo tumejitungia story za kujifariji...Srory za ukifa unaenda mbinguni, au roho yako inakua haijafa na bla bla zngne.

Lakn hizo story zipo kutufariji sisi wafiwa na kupeana moyo kuwa kifo sio mwisho....ila hayo yote hayamsaidii kitu marehemu
 
Mambo mengi anayofanya mwanadamu ni kwa ajili ya nafsi yake. Ukijua hilo basi migogoro mingi na maswali mengi hupungua akilini.
 
Ukweli yote tunayofanya kwa maiti ni kwajili yetu sisi wafanyaji na sio hiyo maiti.
Maiti haitajua imeoshwa, au imepaliliwa kaburi.
Kifo ndio mwisho.
Lakini Sisi bado tunauona ule mwili wa marehemu kama sehemu ya marehemu, na kwa vile wote tunaogopa kifo tumejitungia story za kujifariji...Srory za ukifa unaenda mbinguni, au roho yako inakua haijafa na bla bla zngne.
Lakn hizo story zipo kutufariji sisi wafiwa na kupeana moyo kuwa kifo sio mwisho....ila hayo yote hayamsaidii kitu marehem
Umejibu vyema mkuu,Asante sana
 
Hope mmeamka salama. Naomba anayejua anisaidie na mimi kujua÷

1. Kwanini mtu akifa anaoshwa?
Anazikwa ardhini na kufukiwa sasa huo usafi anaofanyiwa unamsaidia nini as long as atachanganyikana na mavumbi soon?

2. Mtu akishazikwa baada ya miezi au miaka kadhaa ndugu huanza kwenda kufagia kaburi lake tena wanapiga deki kabisa. Hii inamsaidia nini mtu aliyeoza kaburini?

3. Kuna nadharia kwamba tutafute pesa ili tukifa tukumbukwe, Maiti huko iliko inapata faida gani ikikumbukwa na walio hai kwa mema iliyotenda? Mfano Mengi anapata faida gani kukumbukwa na walemavu ambayo Maiti ya kimasikini haipati?

Mshana Jr na wengine njooni mnisaidie kuelewa haya mambo.
Halafu mtu akifa anageuka kuwa mzimu, kesho mnaenda kumuomba alete mvua, huu upuuzi tumeupata wapi? Mfu anapata wapi Nguvu za kuleta mvua?
 
Kwanini mtu akifa anaoshwa?
Anazikwa ardhini na kufukiwa sasa huo usafi anaofanyiwa unamsaidia nini as long as atachanganyikana na mavumbi
Kwamba hauoni umuhimu wa kuusafisha mwili?. We inaonekana huogagi
Mtu akishazikwa baada ya miezi au miaka kadhaa ndugu huanza kwenda kufagia kaburi lake tena wanapiga deki kabisa. Hii inamsaidia nini mtu aliyeoza kaburini?
Binadamu kaumbiwa akili, kujali na huruma......sio kama wanyama akishafukia tu ndo imetoka
Kuna nadharia kwamba tutafute pesa ili tukifa tukumbukwe, Maiti huko iliko inapata faida gani ikikumbukwa na walio hai kwa mema iliyotenda? Mfano Mengi anapata faida gani kukumbukwa na walemavu ambayo Maiti ya kimasikini haipati?
Aisee🤔

Pia unaweza kusoma....

Kwamba hauoni umuhimu wa kuusafisha mwili?. We inaonekana huogagi

Binadamu kaumbiwa akili, kujali na huruma......sio kama wanyama akishafukia tu ndo imetoka

Aisee🤔

Pia unaweza kusoma....

umuhimu wa kusafisha mwili ili ukafukiwe kwenye udongo?
 
Namba tatu ndo inashngaza naona Bora hata kama hauna pesa uwe na roho ya kusaidia watu utagain heshima kubwa na mioyo ya watu na kuacha alama.
 
1. kwanini tunasafisha maiti?

Jibu; Kuna sababu za kidi na sababu za kiutu/ kibinadamu. kidini ndugu waislam na wakristo watakuja kuelezea kwanini tunasafisha maiti, sababu za kiutu/kibinadamu tunasafisha maiti kwa kuuheshimu ule mwili wa mpendwa wetu hatuendi kumfukia kama mzoga wa punda, ile ni maiti lakini ni maiti ya binadamu lazima tuheshimu kumsafisha as na sisi ni binadamu pia.

2. Inamsaidia nini maiti kusafisha kaburi lake au kwanini tunasafisha kaburi?

Jibu;sababu kuu ni kumbukumbu, kaburi linasafishwa ili kuonesha bado tunamkumbuka mpendwa wetu na tunasafisha ili kaburi lisisahaulike kizazi na kizazi watu waendelee kujua pale kuna ndugu yetu amehifadhiwa.

3. Kuna nadharia kwamba tutafute pesa ili tukifa tukumbukwe, Maiti huko iliko inapata faida gani ikikumbukwa na walio hai kwa mema iliyotenda?

Jibu; Maiti haipati faida yoyote ikikumbukwa na walio hai. kwaiyo nadhali ya kutafuta pesa ili ukumbukwe ukifa hii itabaki kuwa nadhali tu, Haina ualisia.
walio hai ndiyo wanajukumu la kumkumbuka alie kufa maiti haina mda wa kumkumbuka alie hai, uwe masikini ama tajiri ukifa utakumbukwa tu.
 
Back
Top Bottom