Naomba kujua faida wanayopata NBC

Naomba kujua faida wanayopata NBC

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Mimi ni mshabiki wa mpira ila mpka sasa sijui huyu mdhamini mkuu anapataje faida kwa kudhamini ligi kuu.Ukiniambia anajitangaza na anapata wateja sijui kama ni kweli maana mimi tangu aidhamini sijawahi kuvutiwa kwenye kufungua acc kwao.
Kwa Azam najua anapata faida kwa sababu anatangaza vitu ambavyo ni consumable na watu wote.Hata GSM sijui anapataje faida kwa kuwa mdhamini mwenza maana sijui kitu kingne anachouza zaidi ya Magodoro (Sijui nitanunua godoro lini).

Au kuna watu mlikuwa hamna acc NBC na sasa mmefungua baada ya NBC kuidhamini league?Kuna watu mlikuwa mnanunua magorodo kwingne na baada ya udhamini sasa mnanunua ya GSM?

Kwa Mo najua pale anapiga pesa ndefu maana watu kibao ndani ya Nchi hii wanambea,wanaingia ofsini,wanapiga vibarua,wanavuja jasho kuchimba mitaro huku WAMEBEBA SABUNI MGONGONI.

Narudia tena,Sina mpango wa kununua godoro hivi karibuni labda baada ya miaka 5 ijayo na sina mpango wa kuhamisha maburungutu yangu kupelekea NBC kisa mpira.
 
Kama pangekuwepo na faida ya maana sidhani kama Vodacom wangejitoa.
Haimaanishi kama voda hapati faida basi na nbc hapati, kumbuka voda kampuni ya simu za mikononi inayoongoza tz kwanini huzani ligi ndio imewafanya waongoze? Vilevile nbc tulishawasahau lakini baada ya kudhamini ligi kuu saivi wanatajwa midomoni, binafsi ninampango wa kuwatembelea nijue product zao
 
Kingine Kuna ushirikiano kati ya NBC na kampuni ya kutengeneza mabasi ya Youtong ,vilabu vitakopeshwa vikidhaminiwa na tff hapo watapiga pesa na vilabu vitafungua acc NBC ili wawekewe pesa ya udhamini.
Sijaona mkataba ila nahisi moja ya kipengele vilabu, tff na bodi ya ligi vitatakiwa kuwa na akaunti nbc. Pesa za azam za udhamini na wadhamini wenza zitapitia pale.
 
NBC ilikuwa imepoteana Ila kwa sasa hata wewe unaitaja lazima Kuna kitu kitaongezeka kwa sana
Mimi ni mshabiki wa mpira ila mpka sasa sijui huyu mdhamini mkuu anapataje faida kwa kudhamini ligi kuu.Ukiniambia anajitangaza na anapata wateja sijui kama ni kweli maana mimi tangu aidhamini sijawahi kuvutiwa kwenye kufungua acc kwao.
Kwa Azam najua anapata faida kwa sababu anatangaza vitu ambavyo ni consumable na watu wote.Hata GSM sijui anapataje faida kwa kuwa mdhamini mwenza maana sijui kitu kingne anachouza zaidi ya Magodoro (Sijui nitanunua godoro lini).

Au kuna watu mlikuwa hamna acc NBC na sasa mmefungua baada ya NBC kuidhamini league?Kuna watu mlikuwa mnanunua magorodo kwingne na baada ya udhamini sasa mnanunua ya GSM?

Kwa Mo najua pale anapiga pesa ndefu maana watu kibao ndani ya Nchi hii wanambea,wanaingia ofsini,wanapiga vibarua,wanavuja jasho kuchimba mitaro huku WAMEBEBA SABUNI MGONGONI.

Narudia tena,Sina mpango wa kununua godoro hivi karibuni labda baada ya miaka 5 ijayo na sina mpango wa kuhamisha maburungutu yangu kupelekea NBC kisa mpira.
 
🤣🤣🤣🤣🤣yaan mi nitaje jina lako upate faida?
Ndiyo mkuu.

Kwa mfano mimi mwaka 2012 nikiwa kwenye basi nilisikia mtu anaongelea habari ya Dkt Slaa ambayo aliisoma JamiiForums.

Kwa wakati huo sikuwa naifahamu JF.

Lakini baada ya kusikia nikaamua kuitafuta.Mpaka leo JF imekuwa chanzo changu kikuu cha habari....

Lakini kama yule asingeitaja ningechelewa mno kuijua JF au nisingekuwa na mzuka nayo kama ilivyo sasa!
 
Haimaanishi kama voda hapati faida basi na nbc hapati, kumbuka voda kampuni ya simu za mikononi inayoongoza tz kwanini huzani ligi ndio imewafanya waongoze? Vilevile nbc tulishawasahau lakini baada ya kudhamini ligi kuu saivi wanatajwa midomoni, binafsi ninampango wa kuwatembelea nijue product zao
Nenda tu utakuwa very disappointing maana AD kwao ni kichaka cha kupiga pesa tu ila uhalisia wote wana poor customer care na sio NBC tu ni wote tu.
 
Ndiyo mkuu.

Kwa mfano mimi mwaka 2012 nikiwa kwenye basi nilisikia mtu anaongelea habari ya Dkt Slaa ambayo aliisoma JamiiForums.

Kwa wakati huo sikuwa naifahamu JF.

Lakini baada ya kusikia nikaamua kuitafuta.Mpaka leo JF imekuwa chanzo changu kikuu cha habari....

Lakini kama yule asingeitaja ningechelewa mno kuijua JF au nisingekuwa na mzuka nayo kama ilivyo sasa!
Ooh nmekupata but ongeza nyama kdogo.
 
Back
Top Bottom