Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 31,559
- 42,179
Faida ya kwanza ni huu uzi wako, sio lazima ufungue account wao kupata faida kukuza tu brand name na muda wote kutajwa tajwa kwenye midomo ya watu kunaongeza nguvu ya brand.Mimi ni mshabiki wa mpira ila mpka sasa sijui huyu mdhamini mkuu anapataje faida kwa kudhamini ligi kuu.Ukiniambia anajitangaza na anapata wateja sijui kama ni kweli maana mimi tangu aidhamini sijawahi kuvutiwa kwenye kufungua acc kwao.
Kwa Azam najua anapata faida kwa sababu anatangaza vitu ambavyo ni consumable na watu wote.Hata GSM sijui anapataje faida kwa kuwa mdhamini mwenza maana sijui kitu kingne anachouza zaidi ya Magodoro (Sijui nitanunua godoro lini).
Au kuna watu mlikuwa hamna acc NBC na sasa mmefungua baada ya NBC kuidhamini league?Kuna watu mlikuwa mnanunua magorodo kwingne na baada ya udhamini sasa mnanunua ya GSM?
Kwa Mo najua pale anapiga pesa ndefu maana watu kibao ndani ya Nchi hii wanambea,wanaingia ofsini,wanapiga vibarua,wanavuja jasho kuchimba mitaro huku WAMEBEBA SABUNI MGONGONI.
Narudia tena,Sina mpango wa kununua godoro hivi karibuni labda baada ya miaka 5 ijayo na sina mpango wa kuhamisha maburungutu yangu kupelekea NBC kisa mpira.
Kesho NBC wakizindua bidhaa mpya kila mtu ataijua sababu ya brand ina nguvu, ila anzisha chako hata kama quality inaweza kuwa kubwa zaidi hakuna atakayejali.