Naomba kujua historia ya Urusi

Siku ambayo huyu rais wa urusi wa sasa Vladimir Vladimorovich Putin akifa wamarekani na washirika wao watafanya sphere he. Ni umiza kichwa kwao sana, namkubali sana huyu jamaa
Hahahahaaa ndo maana umeweka avart yake Mkuu. Jamaa anatumia akili nyingi sana
 
Ndio maana wapinzani wa chama cha vladimiry Putin hawatakaa wapate madaraka kwa kua mmarekani anawaunga mkono lakini asilimia kubwa ya warusi wanamkubali putini
Ndio maana sikushangaa aliacha urais akawa waziri mkuu na baadae akarejea tena kwenye kinyanganyiro cha urais
Hii ilimpa nafasi ya kuona nchi za mangaribi zinaiwazia nini urusi
Ndio maana amerudi na akili nyingi sana mmarekani anajuta tu pamoja na vikwazo vyote naona vimegonga mwamba
Kuna jarida moja lilitoa neno kwamba Putin anaushawishi mkubwa sana duniani katika nyanja ya siasa
 
Daaaah Mkuu hii season nimeipenda sana hasa kwenye ukweri kwa nin wajeruman waliwaua kwa kuwachoma moto wayahudi. Maauaji ya holikost. Umenena vyema na umenifungua macho, nimpenzi sana wa DW lakin wakifikaga hapa huwa wanamung'unya maneno. Thanks
 
Mkuu haya maswali yako yote ni rahisi sana kwa @The Emperor.
We subiri kidogo tu,atakuja
 
Pro-Americans wanasema Russia kuna rushwa,hakuna democracy, kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kwa upande wa kiuchumi Russia imeadhiriwa na vikwazo vya U.S.A na EU hadi imepelekea Inflation kubwa , kushuka dhamani ya sarafu yao (Rubles), kushuka kwa bei ya mafuta (OPEC members & nonmembers kama Russia), Kuzuia mali za vigogo na warusi wenye ushawishi mkubwa na Ufaransa kubatilisha makubaliano ya kuiuzia Russia Meli za kivita.

Hili unalizungumziaje Mkuu, au ni Western propaganda???
 

Mkuu kwanza inabidi uelewe kuwa warusi ni multi-ethnic society lakini jamii(race) ya slavic ndio inayotawala na kushika nafasi muhimu zote katika uongozi wa nchi. Hii inatokana na jiografia ya nchi yenyewe upande moja upo ulaya na mwingine upo asia. Hii ni historia ndefu ambayo ipo hata kabla ya soviet union. Sasa wahasimu wao wakiongozwa na wamerekani walipofanikiwa kuisambaratisha hiyo soviet union, walibariki pia ubadhirifu, unyonyaji, ukiukwaji wa haki za kibinadamu na uporaji wa mali za uma na kikundi cha watu wachache ili kuidhoofisha kabisa nchi ya urusi(ambayo ilibaki baada ya kusambaratika huko) na ndio mwanzo ama era ya oligarchs wakiwemo Roman Abromivich, Mikhail Khordokovsky na wengine ambao waliweza kuyanunua makampuni makubwa ya serikali kwa njia za bei za kutupwa na kujilimbikizia assets ambao kibongo tungeuita unalala maskini unaamka tajiri. Pia hichi kikundi kiliweza kuwa na ushawishi mkubwa sana kwa serikali na viongozi wengine. Kumbuka pia kipindi hiki nchi ilikuwa chini ya raisi Boris Yeltsin, lakini mnamo mwaka 1999 kuingia 2000 alistaafu ghafla kutokana na sababu za kiafya na kuachia ngazi kwa Vladimir Putin ambaye alikuwa waziri mkuu kipindi hicho. SASA NIRUDI KWENYE MASWALI YAKO

Russia ni nchi yenye historia ndefu na interesting na ni watu wazalendo na wanaopenda tamaduni zao. Hawa oligarchs ndio waliweza kuuleta huo mchezo wa rushwa na kutumia kila njia kupata kila wakitakacho. Huo utamaduni ulishika kasi sana kipindi cha raisi Yeltsin hadi alipoingia Putin ndio mambo yakanza kubadilika. Yeye aliweka mkazo kwenye uchumi na maendeleo ya nchi kiujumla na sio maslahi ya kile kikundi cha matajiri. Hapo ndio mchezo ukadilika na Putin kuonekana mbaya kwa hao jamaa na serikali za magharibi. Kumbuka hawa jamaa walimilki vyombo vingi vya habari na pia walikuwa na ushawishi mkubwa hata na viongozi wakubwa duniani so kuwaharibia hao ni kama unawaharibia wakubwa wengine huko duniani mana walikuwa wanakula wote katika hiyo michezo yao. Kinachoendelea mpaka leo sio kwamba rushwa imeisha urusi lakini imepungua kwa asilimia kubwa mno ukilinganisha na hapo awali kabla ya Putin. Kuhusu democracy na ukiukwaji wa haki kila nchi ina haki ya kujitawala vile inavyotaka kutokana na historia na jamii yake. Hakuna nchi ambayo inalea wahaini au wakwepa kodi au wahujumu uchumi au wapinzani wasiofuata taratibu zilipozo za nchi husika. Na hapa ndio Putin anapowaweza nchi za magharibi mana wanatamani sana atolewe madarakani hata kinguvu lakini mara zote hajawafikiwa.

Kuhusu vikwazo vya kiuchumi ni ukweli usiopingika kama kweli viathiri maendeleo ya nchi husika. Labda tuanzie sababu za wao kuwekewa hivyo vikwazo, ambayo ni mgogoro wa ukraine. Huu mgogoro ni mada nyingine kabisa lakini kiufupi ilichochewa na nchi za magharibi kumshinikiza raisi wa kipindi hicho Viktor Yanukovich kukubali msaada wa kiuchumi ambao iluratibiwa na EU. Bwana Yanukovich pia mezani alikuwa na package nyingine kutoka urusi ambao ilikuwa na masharti nafuu zaidi . Sasa hawa viongozi wa magharibi kutumia wapinzani wa kiongozi huyu na taasisi(NGOs) zake nchi humo waliweza kumuondoa raisi huyo madarakani kwa maandamano makubwa mno(maiden protests) ambayo yalipekea machafuko nchi humo. hayo machafuko ndio sababu kubwa ya urusi kubeba hizo lawama na kuwekewa hivyo vikwazo.

Sasa hivyo vikwazo vimemfanya urusi kuufikiria upya uchumi wake na kujipanga upya. Kumbuka kipato kikubwa alikitegema kutokana na. Mauzo ya oil na gas ambayo bei yake imeshuka kwenye soko la dunia, na wateja wake wakubwa ilikuwa ni EU. Amefanikiwa kupata soko Asia kama nchi ya china na india. Pia imemfanya kukuza uchumi wa ndani zaidi na kuacha kutegemea vitu kutoka nje ambayo pia itawaadhiri sana EU hata kama hivyo vikwazo watavitoa mana itakuwa ngumu kurudi kwenye masoko hayo nchi humo. Pia sio nchi zote EU zinasupport hivyo vikwazo ikiwemo Italy na hasa duniani kwingine kwa sababu kisheria ni lazima viidhinishwe na UN na sio kila nchi zinapokosana basi ruksa kuwekeana hivyo vikwazo. Na pia waatharika wakubwa ni wananchi wa kawaida ambao wanaona wanachofanyiwa n hizo nchi za magharibi na kuongeza chuki kwa hizo nchi na serikali zao.

Kuhusu mgogoro wa meli za kivita ilikuwa ni mkataba ambao waliingia kabla ya huo mzozo wa ukraine. Sasa mfaransa baada ya kukaliwa kooni na mmarekani amekubali kuvunja mkataba huo ambao mrusi alikuwa tayari ameugharamia kwa kiasi kikubwa na hivyo kudai fidia. Swali ni je mfaransa anajenga taswira gani kama business partner kwa mataifa mengine?

Lakini hayo yote ukumbuke tu urusi ni nchi kubwa mno yenye rasilimali nyingi mno na inasemekana ndio nchi pekee duniani inayoweza kujitegemea katika kila kitu. Pia kijeshi binafsi naamini iko juu vizuri hasa upande wa defensive hata zaidi ya marekani na ndio mana hawajawahi kuwaletea chokochoko zaidi ya propaganda.
 
Swali

Mnadhani umoja wa nchi za kisoshalisti unaweza kupanuka tena?

China kwa nini haina uchumi wa kisoshalisti kama urusi japo ni nchi ya kisosholiati?
 
Niliwahi kusoma historia ya Urusi kwa sehemu.
Leo nimejifunza kitu kipya hapa.

I believe kama Tanzania tuna sehemu ya kuiga hapo

Kweli kabisa kuna mambo mengi sana ya kujifunza kama:-
1. kuwa na uzalendo kwa nchi yetu.
2.Kuwekeza kwenye elimu na sayansi.
3. Tujenge uchumi wetu bila kuwa wategemezi wa kila kitu kutoka mataifa makubwa. Hii inasaidia kukwepa makali ya vikwazo vya kiuchumi.
4. Kuwa na morale na spirit ya kufanya kazi kujenga taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…