Wadau Naombeni mnijuze mambo yafuatayo kuhusu USSR na Urusi ya sasa
1. Je ni kwanini USSR ilijiingiza katika mgogoro wa Afghanstan (Soviet Involvement in Afghan War 1989-1991)?
2. Je USSR walizidiwa nguvu na mbinu dhidi ya mahasimu wao hususani nchi za magharibi zikiongozwa na U.S.A ndo maana wakashindwa vibaya vita hiyo?
3. Je ni kwa kiasi gani kushindwa katika vita hiyo ilichangia kusambaratika kwa USSR miaka ya 1990s?
4. Je kwanini China ilikuwa inapambana upande wa wapinzani ama ilikuwa inasaidia wapinzani wa ujamaa wa ujamaa, ikiwa ni mshirika mkubwa wa USSR?
5. Je kushindwa kwa USSR ilikuwa ni mchango mkubwa wa Osama Bin Laden aliyekuwa anatumiwa na U.S.A? Ingawa baada ya vita hiyo akawa mpinzani wa U.S.A, Kumbuka U.S.A huwa wanasema hawana rafiki wa kudumu.
6. Je ni kweli kuwa Baada ya kusambaratika kwa USSR, Urusi ndiyo jamhuri pekee iliyoridhi madeni, mali,teknolojia, uanachama wa kudumu wa baraza la ulinzi la umoja wa mataifa na mambo yote ya iliyokuwa USSR?
7. Mwisho, Je Urusi baada ya kusambaratika kwa USSR ilikuwa na hofu dhidi ya U.S.A na NATO yake pamoja na washirika wake.Hivyo kuifanya Urusi kuwa na hofu kujiingiza katika migogoro mikubwa ya kijeshi. Je kuingia kijeshi Syria mnamo septermber 30,2015 kunaashiria kuanza kwa mvutano mkuwa baina yake na U.S.A kama ule uliyokuwepo kipindi cha vita baridi? Je huu upinzani wa Urusi unaweza kuondoa Dollar economy ya Mmarekani? Je inaweza leta vita ya tatu (WW3 or WWIII) ama Nuclear War baina ya hawa wababe?
************** Nawasilisha