30 mln minimumHabari nyingi wakuu.
Tumeanza mwaka na mipango mipya.
Sina maneno mengi sana ila naomba msaada wa kujua gharama za hii nyumba tu maana ndio nataka nianze baada ya kumaliza tarehe 17 Inshaallah.
Vyumba vitatu vya kulala (1 bedroom)
Jiko
Dining
Kitchen
Store
Sitin room
Public toilet
Chumba kimoja cha kuongea na wageni au kwajili ya mambo ya ofisi.
Nawasiliza.
Shukrani mkuu kwa ushauri wako.Gharama za ujenzi wa nyumba ya aina hiyo haziwezi kufanana au kuwa Constant kutokana na sababu mbalimbali miongoni mwao ni hizi:-
1. Ramani. Kuna ramani "simple" na "complicated". Moja itakuwa na gharama kubwa japo zote zina vyumba vitatu vya kulala sitting room nk. Hapa kwenye ramani pia kuna ukubwa wa nyumba. Je, hiyo nyumba unayotaka kujenga ina ukubwa kiasi gani- Sqm
2. Unatumia malighafi aina gani katika ujenzi.
- Mfano matofali, je ni ya saruji au udongo (kuchoma)
- Bati za kuezekea utatumia zenye kiwango gani? je, bati ni za kawaida, za rangi, mgongo mdogo au mpana au vigae? Je, ni za Kichina au za ALAF?
- milango na madirisha. Utatumia ya mbao au aluminium; nk.nk
3. Je, unajenga eneo/ sehemu gani? Kijijni, mji mdogo, mji wa kawaida, manispaa au jiji? Nayo inaweza kusaidia kukadiria gharama za ujenzi?
4. Ufundi. Je, unatumia fundi wa aina gani? Mafundi wanatofautiana viwango vya gharama.
NB: kama unajenga jijini Bongo Daresalama kwa nyumba ya viwango vya kawaida jiandae kuanzia milioni 40.
Mimi ngoja niishie hapa, na wengine watakuja kuongezea kulingana na uzoefu wao.
Acha kumdanganya. 30m ni nyingi ila kwa alivyoeleza hatopungua 40m. Writing from my experience in building.30 mln minimum
Aiseeeehhh mbona kama pesa ndogo sana,kwani hii ina ukubwa gani?Eneo lipo slope au flat ardhi ni mchanga au udongo mfinyanz unajengea wap mkoan au mjini
mkoani ukiwa na 15ml mfano morogor wanatumia tofar za kuchom na kokoto bei poa mafuni wa mkoan hawana gharama kama mjini ni wastan wa 23/ 25 ukiwa na uelewa wa ujenz na usimamiz wako wa hali ya juu kama unataka kila jambo afanye mtu basi ni 30+ ml nakupa mfano haisi hii nyumba adi napiga bati imesimamia 11.8ml finishing kila kitu hapo ni imesimamia 20ml hapo umeweka gril, rangi ndan nje tiles mfumo wa maji milango gypsum nk View attachment 2070433View attachment 2070432
Sent from my SM-G965U using JamiiForums mobile app