Azizi Ki amepewa na Yanga $500,000 sawa na Tsh. 1.2B pamoja na mshahara wa Tsh. 48M kwa mwezi. Lakini pia alikuwa na fursa ya kupewa mshahara wa Tsh. 91M na CR Belouizdad, amezichomoa. Sharti alilotoa kwa Yanga ni kwamba kabla hajasaini, kati ya hizo 1.2B, nusu yake yaani 600M ziwe zinasomeka kwenye akaunti kabisa, maana alishashuhudia kwa wenzie wanaoenda kushtaki FIFA. Yanga imekubali yote