Pombe ni kilevi cha zamani sana ukisoma kwenye historia na kwenye Quran pombe imekatazwa mara tatu kwasababu maswahaba walikuwa wamedumbukia kwenye ulevi uliopitiliza ikaja katazo la kwanza likisema
"Msikaribie swala ikiwa mmelewa' (an nissa:43)
Ila haikusaidia maana walikuwa wakitoka kwenye ibada break ya kwanza kwenye pombe likaja katazo jingine likisema
'Enyi ambao mmeamini hakika ya ulevi na na masanamu na ramli na mishale ya kutizamia ramli ni uchafu na ni miongoni mwa matendo ya shetani jiepusheni nayo huenda mkawa wachamungu wa kweli,
Uharamisho wa ulevi katika uislam,
Kwa hakika shetani anataka kukuleteeni uadui na bughudha baina yenu kwa ajili ya ulevi na kamari na anataka kukuzuilieni dhikiri za Allah na kuswali basi je mtaacha hayo (al maida:93)
Pombe ilikatazwa kwasababu watu walikuwa wanaenda kwenye ibada lakini hawana yakini na ufahamu wa kitu wanachokifanya wote tunajua pombe ilivyo na mtu akilewa kwa hyo lengo lilikuwa mtu akienda kwenye ibada ajue anachokifanya na mtume alipata sana tabu kukataza jambo hilo.
Sent from my SM-N950F using
JamiiForums mobile app