Naomba kujua sababu ya gari kuchemsha (overheat)

Jarib kutumia pure water hayo ya uhai ukiangalia pale kwenye PH utagundua kuwa sio pure water coz mengi yanazid 7.1 au below 6.9......
Pure water ni kama yale maji ya AC zile za maofisini au majumbani au unaweza kutumia maji ya kilimanjaro kwasababu yenyewe ni pure water
 
Nashukuru kwa elimu,licha ya kuganya service ya mara kwa mara,ya kumwaga oili,sevisi ya injini hutakiwa kufanyika kila baaada ya mda gani? Huu ni mwaka wa pili tangu niinunue show room,
 
Engine kuchemsha inainyesha kuwa cooling system imekufa.

(1) Ama injini inavuja maji.
(2) Water pump inayosukuma maji imekufa
(3) Ama radiator imeziba kwa kuzuia maji ya kupooza injini yasizunguke.
(3).................. nitanedelea; mgoja sasa nikakojoe halafu nikalale!
 
Nashukuru kwa elimu,licha ya kuganya service ya mara kwa mara,ya kumwaga oili,sevisi ya injini hutakiwa kufanyika kila baaada ya mda gani? Huu ni mwaka wa pili tangu niinunue show room,
Muda wa kufanya service inategemea na matumiz yako.

Kwa mfano service ya daladala ni tofauti na service ya coster inayoshinda bila kufanya kazi

Ukiangalia vizuri kwenye manual ya chombo chako kuna masaa ambayo wamekuwekea ya kufanya hiyo service
 
Mkuu umeongea vyema ila kuna coolant temperature sensor ni muhim sana kwny coolin system ya gar ipo karibia na thermalstart inafanya kaz ya kupima joto la maji pind joto likiwa juu sana inaamuru fen kuzunguka na maji lupoozwa lkn pia nanuwezo wa rejetor kutunza maji kama imetoboka au mfuniko mbovu inaweza changia
 
Majibu yote hapo juu ni sahihi ila nitaongezea moja, ambalo ni kuwa na 'warped cylinder head'.

Hapo chini nimeambatanisha mchoro wa 'engine' iliyoharibika (warped cylinder head) kutokana na kuchemka (overheating).



Hili hutokea pale ambapo gari imekuwa ikichemka kwa muda mrefu sana (kutokana na sababu zilizotajwa na wenzanu hapo awali) na kusababisha 'cylinder head' kupinda. Matokeo yake maji (coolant) kuingia kwenye chemba na kuunguzwa na kusababisha mvuke mweupe.

kama kila ukiongeza maji kwenye 'cooling system' (radiator or expansion tank) na maji kupotea 'kimazingara' bila ya kujua yanapokwenda basi cylinder head imepinda. Na kadri 'engine' inapozunguka ndipo maji yanapojipenyeza kwenye chema na kuunguzwa. Hii hufanya engine kuzidi kuchemka, kwa kukosa maji ya kuipoza.

Tatizo hili unabidi ulitatue haraka (by removing and resurfacing heads) kwasababu siku moja gari itashindwa kuwaka kabisa kutokana na kupoteza 'compression'.

Hii chini ni 'cylinder head' niliyoitoa kwenye gari iliyokuwa ikichemka, nikiipina kwa kutumia rula (straight edge) kuangalia jinsi ilivyopinda . Utaona kichuma (feeler gauge) kikipenya chini ya rula kuonesha kuwa hii 'cylinder head' imepinda sana.



.
Huu ni mchoro wa 'Engine' ambayo haina matatizo ya kuchemsha.



Na hii ndiyo 'cylinder head' nzuri utaona kachuma (feeler gauge) hakawezi penya katikati ya 'cylinder head' na rula (straight edge).

 
Mkuu mimi gari yangu inatabia ya kujizima kwenye foleni,au ikiwa silencer,nimejaribu kupandisha silnce lkn bado tatizo lipo?service naw kila kitu kipo vizuri,tatizo nini?
 
Topic nzuri sana hii kwa sababu inasaidia wengi wetu kuwa na uelewa wa magari, hasa kwa wale wenye nayo au wenye ndoto ya kumiiki gari. Wataalamu shusheni nondo za uhakika tufaidike na elimu yenu murua.
 
Ok Poa Mkuu ngoja nimcheki
 
Ok
 
Imejitoshereza kabisa
 
Hata pure water si sahihi kutumia kama coolarnt kwa sababu maji hata kama ni pure ni lazima yatasababisa kutu kwenye radiator na more kule yanakopita. Coolant ilivyotengenezwa haiwezi kusababisha kutu.
 
Hata pure water si sahihi kutumia kama coolarnt kwa sababu maji hata kama ni pure ni lazima yatasababisa kutu kwenye radiator na more kule yanakopita. Coolant ilivyotengenezwa haiwezi kusababisha kutu.
Ninaongea by experience mimi ni marine engineer katika cooling tunatumia sea water na fresh water

Iv unaijua sea water katika corrosio?

Watu wa magar wanatakiwa wabadilike kunakitu kinaitwa cathodic protection hutumika kwaajili ya kuzuia kutu hata kama chuma kimezamishwa kwenye acid hakiwezi kupata kutu

Kwa ufupi pitia electrochemical serie ndo utajua namna ambavyo maji yanaweza kutumika as coolant bila matatizo
 
Kwa swali lake hilo hapaswi hata kuwa na gari! Au awe anaendeshwa!
 
Hata pure water si sahihi kutumia kama coolarnt kwa sababu maji hata kama ni pure ni lazima yatasababisa kutu kwenye radiator na more kule yanakopita. Coolant ilivyotengenezwa haiwezi kusababisha kutu.
.
Pia coolant inafanya kazi kama 'solvent' kumeza 'deposits' kwenye 'cooling system'. Systems nyingi za kisasa zina 'temperature sensors' kwenye radiator ku - monitor temperature ya coolant. Kama kuna deposits kwenye sensors basi readings zinazo kwenda kwenye computer zinaweza zisiwe sahihi na kufanya feni za kupozea zisiwake kwa muda muafaka na kusababisha overheating (hasa unapokuwa kwenye foleni).

Vile vile kutokana na coolant kuwa na higher boiling point than water, inasaidia kuendela kupoza engine (heat transfer) bila tatizo hata kama joto la engine litafika 100°C. Maji yakifikia kwenye anga za 100°C yanaanza kutengeneza bubbles (za hapa na pale, unless ni pressurized system) na hii inazuia uwezo wake wa kupoza vizuri na kusababisha overheating.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…