Naomba kujua sababu ya gari kuchemsha (overheat)

Mkuu kuhusu hedi mpk kutoa moshi ndio exactly nilioexpirians hadi leo najaza maji tu na kuchapa mwendo naomba unielewshe solution ipoje na garama kwa makisio bcs sina uelewa kuhusu magari . Nitashkuru sm ukinijibu.
Inabidi utafute fundi aifumue injini aangalie kama hedi ipo/zipo flat kulingana na vipimo vilivyowekwa na waundaji (manufacturer).

La sivyo itabidi utumie gharama zaidi kuirudisha hedi kwenye ubora wake wa mwanzo. Gharama yake kwakweli sifahamu kwa kuwa nipo nje ya nchi.
 
Mkuu hebu rudia kusoma reference zako, kazi ya cooling ni ya maji au coolant. Jaribu kukagua engine uone pipes za maji kutoka kwenye rejeta zinaingia wapi. Check water pump thermostat nk. Kwa kifupi kwenye engine kuna njia za maji kama wengine walivyoeleza. Cylinder head gasket ina njia za maji na oil na ndiyo maana gasket ikiungua maji na oil vinachanganyika. Pia tatizo la gasket husababisha compression inayopotea kutokea njia za maji hivyo inapush maji nje yanakuwa hayakai mwenye rejeta
 
Sababu kubwa ni kutu kutokana na kutumia maji ya bomba. Baada ya hapo inakuwa ni ama water pump au thermostat failure ambazo pia husababishwa na hiyo kutu. Zaidi ya hapo labda itakuwa ni serpentine belt kuchakaa kiasi kuwa haizungushi pump sawasawa.
 
Hapa pana darasa zuri sana asante ma engineer we2.
 
Mi gar yangu naona kama Coolant inaisha haraka kuliko kawaida. Shida inaweza kuwa ni nini??
Gari ni Carina Ti.
 
Kuna hatari gani ukiendesha gari huku alert ya ABS ikiwaka kwenye dashboard?
 
Mimi Gari yangu ni Vitz 2001.Ilikuwa inachemsha nikabadili radiator nikaweka used radiator, ikawa inachemsha Kwa umbali mfupi zaidi.Ikasafishwa ikafungwa Tena.Kwasasa Nina uwezo wa kwenda kutoka airport paka Magomeni Na kurudi hila Maji yanapungua.Natumia maji ya kawaida Na Thermostat ilitolewa.
Nini shida?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kuondoa Thermostat kwenye gari mfano Vitz vvti engine.haiwezi kuwa shida ya kufanya Maji kupotea Na hatimae Engine kuchemsha?
Gari aina gani? Angalia mfuniko wa redetor unaweza kua unavuja afu kuna kitu inaitwa themostart kama aifungui gari inachemsha sehemu zenye joto uwa zinatolewabkabisa ili maji yazunguke free

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nashauriwa nibadili cylinder head gasket lakini Kwa utaalamu wako kuwa kama ikiungua Maji Na oil ujichanganya nafikiri haijaungua.Maana Maji yapo meupe kabisa.Labda nianze kutumia coolant Na pia nirudishe Thermostat.Maana Nina uwezo wa kutola airport paka kinondoni bila gari kuchemsha hila maji yanapungua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu samahani kdg..
Rod nock unaiskiaje kama oil ni kidogo.. yaani mlio gani unasikia?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda mwingine ni water pump kama imeanza kufa huwa engene inachemsha.
Mfuniko upo sawa, feni inazunguka kama kawaida. Engine imefanyiwa overhaul na situumii coolant. Je tunawezaje kuondoa kutu ndani ya radiator? Na kuhusu timing belt naomba ufafanuzi zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Asante sana


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bado upo nje ya nchi?
 
Sababu kubwa ni kutu kutokana na kutumia maji ya bomba. Baada ya hapo inakuwa ni ama water pump au thermostat failure ambazo pia husababishwa na hiyo kutu. Zaidi ya hapo labda itakuwa ni serpentine belt kuchakaa kiasi kuwa haizungushi pump sawasawa.

Mie mbona siku zote natumia maji ya bomba mwendo mdundo na engine ipo fiti kalikiti?
 
Mie mbona siku zote natumia maji ya bombs mwendo mdundo na engine ipo fiti kalikiti?
injini haiko fiti hito; itakufa haraka kabla ya muda wake. Pole pole itajaa kutu na baadaye matundu ya kupoozea yataanza kuziba na injini kuwa ya spana mkononi. Kuna wakati utakuwa unatakiwa kuongezea maji mara kwa mara badala ya kujaza mara moja na kusahahu hadi wakati wa serive nyingine. Ndiyo hiyo ilivyokuwa kwa madereva wa daladala kutembea na geleni la maji!!
 
Mkuu habari.
Nimechunguza pale nikifungua mfuniko wa Radiator kutu imejaa. Natumia maji ya bomba kwa muda mrefu.

Je inawezekana maji yote yakaondolewa na system nzima ikasafishwa kutu yote inaondoka? Nataka nianze kutumia Coolant ama nishachelewa/haiwezekan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…