Naomba kujua walipo waimbaji wa kwaya ya Ulyankulu Bara barabara ya 13

Naomba kujua walipo waimbaji wa kwaya ya Ulyankulu Bara barabara ya 13

Hivi hiyo Album imetoka mwaka gani.?
Kinachofanya nizipende hizi nyimbo Mama alikua anapenda sana kuimba akiwa anatuogesha au akitwanga muhogo huo wimbo wa viumbe vyote. Kwaya nyingine ni ile ya kasulu waliimba Mke mwema..sijui wako wapi. Na wale wa Tabata waliimba sipati picha sijui walipotea wapi
View attachment 1404431
Ilitoka miaka ya 90 katikati huko, Ilivumaga sana kwa kweli,
Ndio zilikuwa nyimbo bora za wakati huo
 
Hii kwaya ni kiboko. Album yangu ya nyimbo za dini za muda wote ni " Katika Viumbe Vyote".

Na kuna wimbo wao mmoja unaitwa " Bwana Alizaliwa" Nimejaribu kuutafuta siupati ninaupenda sana.

Pia nasikia wale waimbaji wengi walikua ni wakimbizi toka Burundi walisharudi huko kwao.
Jaribu kucheki YouTube
 
Kwangu mpambano uwe

Mapigano ulyankulu barabara ya 22

Vs

kwaya ya Unlyahulu barabara ya 13

Ingawa kwangu wote wakati mnoooo

Ilinichukua miaka mingi Sana kutofautisha hizi kwaya, Ni mwaka huu tu ndo nimejua kutofaitisha.

Binafsi nawakubali MAPIGANO na albam zao za MWENYE MAMLAKA, FAHARI YA VIJANA, MICHEZO, SISI NI BARUA n.k
 
Ilinichukua miaka mingi Sana kutofautisha hizi kwaya, Ni mwaka huu tu ndo nimejua kutofaitisha.

Binafsi nawakubali MAPIGANO na albam zao za MWENYE MAMLAKA, FAHARI YA VIJANA, MICHEZO, SISI NI BARUA n.k

Hata mimi ilikuwa ngumu sana kuzitenganisha . Hata kwangu mimi mapigano ulyankulu nawakubali mnoo

Aisee ni kweli,kujua hizo nyimbo lazima uwe kwenye familia ya utumishi au anamjua Mungu,enzi hizo nilikuwa nazunguka na mzee kwenye mikutano ya Injili,usiku kuanzia saa moja nawasha jenereta naweka tapes za hizo nyimbo halafu mida ya saa mbili mkanda wa Mateso ya Yesu au Samson & na delila tunaweka,l.

Basi watu wanajaa,pale kwenye mateso ya watu wanaanza kulia na kutubu.
Ningeweka hapa nyimbo yao moja,naona app imenikatalia kuattach....All in all ukisikia kijana anazijua hizo nyimbo jua ni dalili bila shaka amekulia nyumba ya watu wenye kumjua Mungu au ni familia ya watumishi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilitoka miaka ya 90 katikati huko, Ilivumaga sana kwa kweli,
Ndio zilikuwa nyimbo bora za wakati huo
Sidhani kama ni mid 90s,

Sababu ipo video youtube mzee mmoja kati ya wale walioimba kwaya anaeleza.nyimbo ya katika viumbe vyote imetungwa mwaka 1979,na eneo lilipokuwa kanisa pamekuwa pori.so album kama ilichelewa sana itakuwa ilitoka 1982-1985.
 
Thanks
 
Hii kwaya ni kiboko. Album yangu ya nyimbo za dini za muda wote ni " Katika Viumbe Vyote".

Na kuna wimbo wao mmoja unaitwa " Bwana Alizaliwa" Nimejaribu kuutafuta siupati ninaupenda sana.

Pia nasikia wale waimbaji wengi walikua ni wakimbizi toka Burundi walisharudi huko kwao.
Wale walikuwa wanajua kuimba
Pia kuna wale wa Arusha mjini miaka ile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kwanya iliundwa na wakimbizi kutoka burundi waliokua wakiishi ulyankuru tabora, mwanzoni mwa miaka ya 2000 serikali iliwahamisha na kuwapeleka kambi za kigoma ikiwemo nduta, kanembwa na nyarugusu, baadhi walipata nafasi za kwenda ulaya, australia na amerika kupitia unhcr na wengine kurudi kwao burudi, nilikua nafanya biashara na baadhi yao na bado tunawasiliana hata baada ya kwenda majuu, huwa wananitumia hela nawanunulia bidhaa kama nguo, dagaa na vyombo vya nyumbani, unaweza kushangaa kusikia mtu yuko us ila ananunua nguo na vyombo afrika ila ndio hali halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kwaya Ilivumaga sana miaka ya 90 huko, Nyimbo zao maarufu ni pamoja na
Samson na Delilah, Katika viumbe vyote Ayoub.

Hii kwaya ilijipatiaga umaarufu sana enzi hizo, naomba kujua kama hawa waimbaji bado wote wapo hai? Na wengine wapo wap leo hii?

Asante
Kwenye youtube pia wapo
 
Back
Top Bottom