Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,409
- 13,262
Wakuu naomba kwa yeyote anayejua anisaidie namna ya kuhama kutoka kuwa mtanzania wa Tanzania bara na kuwa mtanzania wa Zanzibar yaani kuwa mzanzibari
Nataka kuwa mzanzibari wa kuhamia ili niwe na haki ya kumiliki ardhi kule na Tanzania bara pia, kugombea uongozi kule na nafasi za Muungano kama utais lakini pia niweze kugombea ubunge kule ili niweze kuteuliwa kuwa waziri katika wizara za muungano na zisizo za muungano kama ilivyo kwa Makame Mbarawa anayeongoza wizara isiyo ya muungano ambayo ni ya Tanzania bara lakini kwa mtu kutoka Tanzania bara hawezi kuteuliwa kuongoza wizara Zanzibar.
Nikiwa mzanzibari naweza kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya Zanzibar au Tanzania bara kama ilivyo kwa Shaka ambaye ni DC huku Tanzania bara lakini hakuna mtanzania bara anayeweza kuwa Sheha, DC au RC kule Zanzibar.
Nataka kuwa mzanzibari kwakuwa wazanzibari wanajitambua sana linapokuja suala la nchi yao na uraia wao tofauti na watanganyika waoga hawataki kuwepo kwa Tanganyika yao utadhani ikiwepo watakufa wote. Ni watu waoga sana na hawaipendi asili na nchi yao kama wazanzibari. Naombeni meongozo wa kuachana na Tanganyika nimechoka kuionea aibu nchi yangu bora nihame kabisa. Kumbukeni KILA MZANZIBARI NI MTANZANIA LAKINI SI KILA MTANZANIA NI MZANZIBARI. Naombeni wazanzibari mnipoker nije kushirikiana nanyi kuipigania Zanzibar