Naomba kujulishwa taratibu za kubadili uraia kutoka kuwa mtanzania bara na kuwa mzanzibari

Naomba kujulishwa taratibu za kubadili uraia kutoka kuwa mtanzania bara na kuwa mzanzibari

Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye uraia mmoja tuu!. Uzanzibari ukaazi sio uraia, ni utambulisho tuu. Jinsi ya kuupata Uzanzibari ukaazi, uwe umekaa Zanzibar kwa miaka 15 mfululizo, unapewa kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar kama alivyoeleza Dr. mambo jambo.
Karibu.
P.
Wao kuwa na Ukaazi wa Bara inawachukua muda gani? Kwanini kuna hii double standard?
 
Wao kuwa na Ukaazi wa Bara inawachukua muda gani? Kwanini kuna hii double standard?
Bara hakuna ukaazi ni uraia wa JMT. Kwa vile Tanzania ni nchi moja yenye uraia mmoja, kila raia wa Tanzania, ana haki zote za Utanzania, bila kujali ni mbara au Mzanzibari. Hii maana yake Tanzania ni ya wote na A,Utanzania ni wa wote, ila Uzanzibari ni kwa Wanzanzibari wakaazi pekee.
P
 
Back
Top Bottom