Naomba kujuzwa gharama za msingi kwa nyumba ya ghorofa moja

Hayo ni makadirio tu haitaji watu kuogopa, shida nae kapoga picha ramani picha imefifia hata vipimo havionekani
 
Nguzo napandiaha 12mm tu,na chini ya nguzo naweka base zilazi nguzo
 
Nanunua material nampatia fundi anajenga,yakipungua nanunua namletea tu,simpi pesa mkononi ya material.
 
Hakunaga Engineer anayejenga, Engineer huwatumia hao hao mafundi Maiko, tofauti ni kuwa yeye anafatilia ratios na hesabu vizuri
 
Ni kweli chuma iko juu Sana, Ila 50M ni mbali Sana mkuu. Hiyo ramani yake hata sio kubwa kivile.
Nimejenga msingi mkubwa kuzidi huo kwa size na ugumu wa mazingira. Ila umekula around 22M, tena ni mkoa wenye vitu bei juu zaidi.
Unaweza kunikadiria yangu mkuu. Ina upana wa 17' na marefu 21 eneo pia ni tambarare...hadi sasa tayari nimeshakusanya Nondo mm 16 Tani 2; Nondo MM 8 ziko 100, Mchanga CBM 70, Kokoto nene CBM 50, Tofali 6' ziko 2,500, Misumari nchi 3 na 4 kigunia kimoja kimoja, binding wire roller moja na marine boards ziko 10. Mkuu hapo nimebakiza nini ili nikamilishe msingi peke yake hadi hatua ya kufuta kiti na kuachia matoleo ya nondo. Plani yangu nataka nimtumie Fundi Maiko. Tafadhali naomba makadirio yako...hizi BOQ nimegundua zimekuwa zinadanganya sana... Tafadhali
 
Ungetoa mchoro tungesaidia, mpaka Sasa Nina uzoefu kiasi flani
 
Hakunaga Engineer anayejenga, Engineer huwatumia hao hao mafundi Maiko, tofauti ni kuwa yeye anafatilia ratios na hesabu vizuri
Haya bhana, Inaonekana wewe ni expert mkubwa wa ujenzi.
Bahati nzuri mhusika alishaelewa, ni wewe tu ndiye hujanielewa mpaka sasa.
 
Sitatoa mchanganuo sababu Kuna vitu tayari umeshaviandaa. Ila roughly andaa Kati 22M mpaka 26M kwa kila kitu. Ila sababu baadhi ya vitu tayari unavyo, mzigo utapungua.
Kifupi ongeza nondo za 12mm ili zitumike kwenye plinth beam.
Hizo 16mm tumia kwenye columns. Hizo 8mm lazima zitadai sababu beams ni nyingi.
Sogeza mawe hapo site kabisa(ikibidi).
Mchanga, kokoto, tofali na misumari vinatosha na kubaki kabisa.
NB. Kesho jioni nakutumia mchanganuo in details kabisa.
 
Unajenga GHOROFA?
 
Swali lako ni gumu,.
Maana kuna cement, nondo,mafundi, vibarua n k
Hauwezi kukadiria kienyeji gharama zake.
 
Mkuu hongera sana,kwenye list yako naona kuna pungufu ya BRC na turubai jeusi,na sumu ya mchwa kwa maeneo yenye mchwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…