Naomba kujuzwa suluhisho la Uvimbe kwenye Ovary

Naomba kujuzwa suluhisho la Uvimbe kwenye Ovary

Pole sana my young sisy...endelea kutafuta ushauri wa kitaalamu...dunia ya sasa imejaa maradhi jamani..sijui ni chakula au ni nini walai...
 
Pole, nadhani tatizo lako litaisha. Tahadhari. Watu wa dunia ya sasa hawana huruma na unapokuwa na shida wanaweza kukufilisi. Uwe na tahadhari sana kwa hawa watu wanajifanya kuwa na ujuzi wa dawa za asili. Wengi ni matapeli. Kama unataka kujaribu basi uwe na tahadhari na usikubali kulipa fedha nyingi. Ikiwezekana mwambie akupe utumie na ukipona ndiyo ulipe. Matapeli wengi wana maneno mengi sana na ahadi tamu tamu huku wakitoza gharama kubwa.
Asante
Nalijua Hilo mpenzi matatizo yakoni fursa kwa wengine watu wanajali pesa
 
Habari zenu ndugu zangu.

Mimi ni binti wa miaka 26, sijaolewa na Sina mtoto.

Mwaka Jana nilisumbuliwa sana uvimbe kwenye mayai mpaka ikapelekea kufanya upasuaji nikiwa na matumaini nimepona.

Ila sasa umerudi tena, na unakua kwa kasi, sasa nna uvimbe wa Centimeter 10, daktari wa wanawake amenambia nifanye tena upasuaji.

Sasa kama nilifanya umerudi nahofia utarudi tena,

Kama Kuna mtu anajua suluhisho ya hili naomba msaada hata wa tiba za asili.
Cha kwanza uzae maana hapo last option huwa ni kutoa uzazi.
 
Na unadhani usipojali afya yako, nani atajali mwingine..?
Hakuna wa kujali
Unajua wakati mwingine ukifatilia Sanaa jambo linakuwa kubwa Sanaa akili zetu huwa zinaunda matatizo hata ambayo hayapo. Ajaribu kuzaa ikishindikana ndo arudi hapa apewe ushauri mwingine lasivyo atafanyiwa operation za kutosha mwisho wamtoe na kizazi chenyewe
 
duuuh,,unatumia njia gani ya uzazi wa mpango!?,,ingawa sio wote ila wengi vidonge vimewasababishia uvimbe....na mbaya zaidi unatabia ya kujirudia,, mamangu wamemtoa mara mbili tayar na kaambiwa umeanza tena,,na yanakua kama kiumbe hai aseeee.
 
Shida inaanzia hapo.

Nenda kwenye hospitali kubwa usiishie zahanati ,kwenye level ya zahanati kwa settings zilizopo hicho kipimo hawafanyi .

Ukifika hospitali kubwa sidhani kama kuna daktari at skip ku order kipimo cha hormone panel test (Hormone Assay) ili ku rule out hormone imbalance.
Mara ya mwisho nimeonana na gynaecologist hospital kubwa tuh hapa dar na hajasema chochote
 
duuuh,,unatumia njia gani ya uzazi wa mpango!?,,ingawa sio wote ila wengi vidonge vimewasababishia uvimbe....na mbaya zaidi unatabia ya kujirudia,, mamangu wamemtoa mara mbili tayar na kaambiwa umeanza tena,,na yanakua kama kiumbe hai aseeee.
Sijawahi kutumia uzazi wa mpango
 
Back
Top Bottom