Hebu twende taratibu! Hao jamaa shule kichwani ipo au ni wale unaoweza kuwadanganya kiboya boya tu na wakaamini?
Kwa kuangalia maelezo yako, hao Watuhumiwa wanonekana kama Mambwiga fulani hivi wasiojua chochote ndo maana ulipowatajia habari za polygraph, wakaogopa! Kama ndivyo, then fanya yafuatayo!
Mosi... hakuna cha polygraph wala nini lakini kv inaonesha wanaogopa hiyo kitu, basi nenda polisi kisha afande atakayekabidhiwa kesi impe stori mzima jinsi jamaa walivyokuwa wamechachawa waliposikia habari za polygraph, kisha mpange Afande mufanye polygraphing fake!
How to make it happen?!
Kuwe na polisi mmoja, fake polygrapher mmoja na doctor/fake doctor mmoja!!
Jamaa wanakuwa arrested halafu mmoja anaanza kuingizwa kwenye "chumba cha polygraph" ambacho kutakuwa na ONLY a police officer na huyo fake polygrapher.
Fake polygrapher ata-set mitambo yake tisha bwege, huku mrija mmoja ukifungwa kifuani kwa mtuhumiwa upande wa moyo, na hakikisha hiyo mirija mirija inakuwa connected kwenye kifaa cha umeme... anything like betri ya gari lakini ionekane more of power device.
Polygrapher fake akisha-connect hayo mamitambo (bila shaka hapo jamaa atakuwa kojo debe), atatulia as if kuna kitu anasubiri, kisha itokee mazungumzo kama yafuatayo:-
Police: Hey, mbona huendelei na hilo zoezi? Unajua kuna kesi zingine zinasubiri?"
Polygrapher: Sa Afande si unajua hatuwezi kufanya hili zoezi bila daktari kumpima mtuhumiwa mapigo ya mo..."
Police: Daktari daktari bhana, hebu anza kazi mara moja!
Polygrapher: Afande, hizi mashine za Kirusi ni tofauti na zile za KImarekani. Hii huwa inafanya synchronization (taja neno lolote gumu gumu) ya mapigo ya moyo kupitia mishipa mipana ya damu ya haemoglobini.
Police: Kwahiyo?
Polygrapher: Afande, kama hatujui uimara wa moyo wake, halafu ile synchronization kwenye mishipa ya damu ika-detect uongo kwenye maelezo yake, hapo hapo inaweza kutokea otorhinolaryngologism inayoweza kupasua mishipa ya damu ya kwenye pulomonari ateri.
Police: Toka... kama unaogopa nafanya mwenyewe.
Jomba, asipotaja zilizobaki zipo wapi, basi sio mimi!