Gari ni matumizi na matunzo yako mwenyewe. Hakuna gari mbaya ama rahisi kuharibika.
Ila kibongo bongo utaambiwa ni gari mbovu, haina nguvu, inasumbua, inagonga chini, ac yake haidumu. Hayo yote ni matokeo ya matunzo duni.
Utakuta mtu ana ki Passo na anakaa madongo kuinama kwenye mabonde na makorongo halafu anatarajia gari isigonge chini.
Mara ya kwanza kumiliki Passo ya cc990 piston 3 ilikuwa ni mwaka 2013. Niliinunua used ya Japan kupitia Durban, South Africa.
Niliiendesha kutoka Durban mpaka Dar bila tatizo lolote.
Niliileta maalum kwa ajili ya safari za mjini tu zaidi lami kwa lami.
Nilimuuzia rafiki yangu mwaka 2019 ikiwa full ac, haichemshi, haigongi wala kusumbua chochote.
Jamaa anaishi kimara Bonyokwa, baada ya miezi minne ile gari ilikuwa hata flyover ya Mfugale haina nguvu ya kupanda, yote sababu ya rough usage.
Narudia tena, gari ni matunzo.