Naomba kujuzwa zaidi kuhusu Toyota Passo

Passo ya cc 1290 ina piston nne. Ni nzuri haina shida. Itunze nawe itakutunza. Muda wa kuifanyia huduma ukifika basi usipitishe muda. Usipende kuibebesha mizigo kama hilux. Hiyo gari hata kama mshahara laki sita unaweza kuimudu. Ukibahatika ukaweka full tank yaani kituo cha mafuta unaenda kuomba chenji tu au kununua mafuta ya taa.
 
Nashukulu mkuu, hiv izi za 1290 cc bei zake zipoje nawezapata kwa 4M kwa mtu?
 
Mkuu mbna kama unanishawishi ninunue kapasso na mimi [emoji2][emoji2][emoji2]
 
Ndugu zangu nina Kavitz Kangu huku Tanga Mjini ..kanasaidia kwa mizunguko Ya hapa barabara za namba ,,sasa nimevuta nguvu kidogo nilitaka nipate tena gari nyengine ndogo ya kunisaidia hata nikitaka kutoka nje ya Tanga iwe Rahisi ..nimewaza nikafikiri lakin bado nipo njia panda kwenye pendekezo la gari ipi niwe nayo ..Bajeti Yangu ni hizi hizi gari zetu za mkononi Bei(5M mpaka 8M) naomba nipewe mapendekezo wana JF ..
 
Ukipata
Runx au Alex usijiulize chukua haraka,ist iko poa ila zimezidi mjin
 
Kweli kabisa, mimi ninako ka piston 4, mwaka wa nne sijawahi kufungua injini, ni oil tu na break pad,
Nimeshawahi kwenda Moshi na kurudi kwa siku moja.

Nilitoka Dar alfajiri saa11 nimefika Moshi saa5 asubuhi, saa 7 mchana nikaanza safari ya kurudi, nikafika Dar home Kitunda saa 2 usiku.

Kanafunguka mpaka 140km/h bila stress
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…