Naomba kuuliza hivi AC ya gari unapoiwasha inatumia mafuta au inatumia nini?

Naomba kuuliza hivi AC ya gari unapoiwasha inatumia mafuta au inatumia nini?

Iko hivii:-
Air conditioner ni mfumo unaohusisha vitu anuai
1. Compressor
2. Evaporator
3. Condenser
4. Capillary tube
5. Expansion valve
6. Accumulator
7. Pipes
N.k

Ndani ya compressor kuna pump yenye piston moja. Ukubwa wa hiyo pump ndio nguvu ya compressor horse power(HP)

Compressor ina pulley ambayo huvishwa belt (fan belt) kupitia pulley ya alternator na ya fan hadi kwenye pulley ya ingine.

Ukiwasha engine inazungusha fan, alternator na compressor iliyo free (haiizungushi piston)

Wakati huo ndipo engine hubeba mzigo ambao ni Gear box na differenture (dif) na body offcourse plus mizigo utakayopakia.

Mizigo hiyo uzito wake hupungua kadri gari inavyoongeza mwendo i.e kutoka gear kubwa kuja ndogo (N.B the bigger the number the lower the gear)

Hapa uta experience matumizi ya kawaida ya gari yako.

Unapowasha switch ya A/C unakuwa umeiunga piston ya compressor (by induction manner) kwa mfumo kama wa clutch na pulley inayozungushwa na fan belt kutoka kwenye engine.

Piston ya compressor hu pump gas iliyoko kwenye system inayokuwa composed na nilivyovitaja kwenye orodha 1 - 7.

Kwenye system ya air-conditioner gas huwa sealed na haipaswi kuwa na leakage,

Gas inakuwa na matabaka mawili, pressure na liquid, compressor inapokuwa Idol, gas/liquid hu settle kwenye low pressure side of the system (unapaswa kuelewa system ya valve ya piston ina tabia gani pia)

Pump ya compressor huanza kusukuma gas pressure na liquid kwa mgandamizo mkubwa! Kitendo hiki huhitaji nguvu kubwa kuizungusha pump ya compressor ambapo kwa mzigo huo automatically piston hutakiwa kuchoma mafuta ya ziada kukabiliana na uhitaji wa nguvu inayodaiwa na compressor ya air-conditioner.
Fuel pump huongeza pressure ya fuel towards combustion chambers na ndivyo huli empty tank lako.

Nimejaribu kufanya short-cut kidoogo ili nisikuchoshe.
Kama una swali uliza hapa hapa.
Sijibu pm hata moja.
Hivi na zile AC za YUTONG kule juuu nazo vipi, maaan ule mufindi c wa nchi hiiii
 
Ishu ipo ivi. tujaalie gari iko idling. Rpm ya idling tuseme ni 750rpm, hii ndio normal engine idling, below that it means no sufficient power coming from the engine to power alternator enough. Sasa unapowasha Ac inaiongezea mzigo engine, mzigo ule unapoongezeka rpm itashuka toka 750 mpaka tuseme 400rpm, this is not good for an engine, kwa sababu itakuwa haitoi nguvu inayotakiwa kuifanya gari iwe normal, kwahio ECU itaamrisha mafuta yaongezwe na hewa iongezwe kidogo ili engine isizidiwe nguvu, hivyo basi ili kupatikane enough power to make effect engine ita command ivo na utaona rpm inazidi toka ile ya kawaida bila ya ac kupanda juu walau 850 ivi au hata 900, sasa hapa ndio unywaji huo wa mafuta unapotokea.

Sijui kama nimefahamika. Au labda niseme ivi, ikiwa engine inahitaji lita moja ya mafuta na hewa nusu lita (sijui hewa inatumika kipimo gani), ili kuanza kutembea bila ya ac, ukiwasha ac itabidi engine ipate lita 1 unusu na hewa lita moja kuzalisha nguvu ile ile ambayo ilizalishwa bila ac
 
Uzuri wa JF kuna ma mtu hapa hata hajui gari lakini atajitia mjanja kujibu
 
ahaaa kwa hiyo hata gari likiwa halina fuel unaweza ukatumia AC?? so Ac haina uhusiano na mafuta wala engine?
Unavyowasha AC means umeongeza load kwenye compressor that mean you need more fuel to operate Ni sawa na kubeba mzigo kwenye gari pia ulaji wa mafuta unaongezeka
 
labda teknlojia imenipita ila navyojua a/c inawezeshwa na gas compressor ambayo hua driven na crankshaft ya engine(hutumia mafuta ku run), cool-air blower ndo zinatumia umeme
Hili ndiyo jibu la swali la mtoa mada.
 
AC ya gari inatumia umeme Wa gari . unaweza ukawasha Ac ya gari pasipo injini ya gari ikiwa imewaka hapo inakuwa inatumia umeme kutoka kwenye betri. Ila ukifanya hivyo betri yaweza kuishiwa chaji. Kwa hiyo ukiwasha gari AC itaanza kutumia umeme toka kwenye alternator ambayo ndiyo hufua umeme Wa gari. Kadri alternator inahitajika kufua umeme kiwango cha matumizi ya mafuta huongezeka.

Hapana baba, AC haitumii betri; kinachotumia betri hapo ni ile blower (FAN) inayo puliza hewa ndani ya gari, hiyo siyo AC yenyewe. Kinachoendesha AC yako kupoza hewa ni compressor ambayo imefungwa karibu sana na alternator kwenye engine ikiwa inaendeshwa na mikanda (serpentine belt) kutoka kwenye crankshaft: hiyo inatumia mafuta ya gari.
 
AC ya gari inatumia umeme Wa gari . unaweza ukawasha Ac ya gari pasipo injini ya gari ikiwa imewaka hapo inakuwa inatumia umeme kutoka kwenye betri. Ila ukifanya hivyo betri yaweza kuishiwa chaji. Kwa hiyo ukiwasha gari AC itaanza kutumia umeme toka kwenye alternator ambayo ndiyo hufua umeme Wa gari. Kadri alternator inahitajika kufua umeme kiwango cha matumizi ya mafuta huongezeka.
Mkuu umetudanganya sana.

Ipo hiv Compressor ya AC inaendeshwa na Crankshaft (main Engine) unapowasha button ya ON/OFF Moja kwa Moja inatuma signal kwny compressor. Umeme huwa unaendesha zile blower za ndan tu. Ukitaka ujiridhishe zima gar press button ya ac then uje utupe majibu.

Kumbuka
Ac inatumia kias kidogo sana cha mafuta.
 
Unavyowasha AC means umeongeza load kwenye compressor that mean you need more fuel to operate Ni sawa na kubeba mzigo kwenye gari pia ulaji wa mafuta unaongezeka
shukrani mkuu kwa ufafanuzi [emoji106][emoji106]
 
AC ya gari inatumia umeme Wa gari . unaweza ukawasha Ac ya gari pasipo injini ya gari ikiwa imewaka hapo inakuwa inatumia umeme kutoka kwenye betri. Ila ukifanya hivyo betri yaweza kuishiwa chaji. Kwa hiyo ukiwasha gari AC itaanza kutumia umeme toka kwenye alternator ambayo ndiyo hufua umeme Wa gari. Kadri alternator inahitajika kufua umeme kiwango cha matumizi ya mafuta huongezeka.
Acha maneno ndugu..
 
Back
Top Bottom