Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

tatizo beatrice huwa hujibu replies

najua utarudi ili tulisongeshe ili gurudumu.
 
Inawezakana Mkuu kwa kujua labda kinachomsumbua hawezi kukishinda.
Nilichojifunza ni kuwa wagonjwa wengi wanaojua siku zao za kufariki ni wale wa kansa. Huenda naye anasumbuliwa na kansa. Ila wapo wanaopona na kupita tarehe wanazopangiwa na madaktari. Mkuu jipe imani kuu
 
Hii tabia ya madaktari kuwaambia wagonjwa wao wana miezi mitatu au sita ya kuishi siipendi kusema kweli inawaongezea hofu wagonjwa ndugu, jamaa, familia na marafiki wa karibu. Miaka kama mitano iliyopita jirani yangu mama yake alikuwa anasumbuliwa na kansa kwa kipindi kirefu. Basi ile 2016 wakamwambia mwanae mgonjwa ana miezi sita tu ya kuishi.

Basi jamaa akajiandaa ule mwezi wa sita alioambiwa mama yake atafariki hakufariki alichukua likizo ya mwezi ikakatika. Akarudi kazini lakini huku akitegemea mama yake atafariki wakati wowote lakini yule mama aliishi kwa miaka mingine miwili na nusu ndiyo akafariki. Hii tabia ya kumwambia mgonjwa ana muda fulani wa kuishi madaktari wangeachana nayo.

Nilichojifunza ni kuwa wagonjwa wengi wanaojua siku zao za kufariki ni wale wa kansa. Huenda naye anasumbuliwa na kansa. Ila wapo wanaopona na kupita tarehe wanazopangiwa na madaktari. Mkuu jipe imani kuu
 
Hii tabia ya kumwambia mgonjwa ana muda fulani wa kuishi madaktari wangeachana nayo.
Ni tabia ya hivyo kabisa, imeanza kipindi hiki cha miaka ya karibuni.

Mwanzoni haikuwepo, mgonjwa alikuwa anapewa matumaini mpaka siku yake ya mwisho.
 
Madaktari wanalipwa fedha nyingi na serikali hii kwa kupredict vifo vya watu

Walimu wanalipwa fedha kidogo kwa kuwapa watu matumaini mapya, waione kesho yao yenye fursa na waondoe ujinga

Sasa kupanga ni kuchagua, madaktari sio shida; shida ni muajiri wao anaowalipa fedha nyingi ili waendelee kuwatabiria watu misiba (U-undertaker).
 
Inasikitisha na kuumiza kusoma ulichoandika hasa kuhusu hatima ya wewe kuendelea kuishi.

Swali ni je, unaumwa kweli au unatupima tu?
Mkuu kama yupo regency, atakuwa anaumwa kweli.

Regency kwa sasa kuna wagonjwa wengi sana wa covid 19, kiasi kwamba kupata tu kitanda pale na kuwa admitted nayo ni bahati,
kwa uandishi aloleta nahisi kabisa kama anaumwa basi itakuwa ni hiyo covid, ndo wagonjwa wanakuwa timamu kabisa hata kucheka na kuongea hata kufanya baadhi ya shughuli kama uandishi wakiwa kwenye oxygen, shida yao kubwa inakuwa kupumua naturally.

Nimeuguza wagonjwa watatu wa aina hii, wawili walifariki.
 
Nilichojifunza ni kuwa wagonjwa wengi wanaojua siku zao za kufariki ni wale wa kansa. Huenda naye anasumbuliwa na kansa. Ila wapo wanaopona na kupita tarehe wanazopangiwa na madaktari. Mkuu jipe imani kuu
Hata wagonjwa wa covid, ukishakaa kwenye ventilator zaidi ya wiki mbili, na oxygen level haipandi, ni wakati muafaka wa kuaga.
 
Usiwe na wasiwasi Kamanda. Sisi utakao tuacha, tutaipigania mwanzo mwisho. Na iwapo tutaondoka kama wewe unavyotaka kutuacha, vizazi vyetu navyo vitaipigania tu!

Tena natamani wawe na ujasiri zaidi kuliko sisi wazazi wao ambao kiukweli tumeshikiliwa tu masikio na hivyo kushindwa kufurukuta, na huu mzimu unaoitwa CCM.

Pole sana Kamanda. Kuna safari nyingine huwa hazikwepeki. Unakuta Madaktari wanakuambia kabisa ufanye maandalizi. Kama kuna wosia, nk.
 
Mkuu taja tatizo kuna dawa na watu wa kusaidia pia
Unaufahamu ugonjwa unaoitwa Kansa? Huo ukisambaa mwilini, basi kinacho fuata ni kufanya tu maandalizi. Tena unaweza ukaambiwa kabisa mpaka siku za kuishi hapa duniani.

Achilia mbali huu ugonjwa wa Wachina, toleo la tatu.
 
Dah nimesikitika sana. Nakuombea Mungu Mwenyezi akuponye.

Nafeel maumivu makubwa uliyonayo.

Eeh Mungu wa Mbinguni, Mponye ndugu Beatrice ili aje alitangaze jina lako katikati ya watu na mataifa walikanalo jinaa lako. Amen.
 
Haisee...
Shida nini mummy wangu? pengine tutoe ushauri mbadala...!
::I have got tele heal power tukuombee
 
Japo umekata tamaa amini MUNGU wetu ni mkuu sana akasimame na wewe ktk hili ili uje kumrudishia utukufu[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Pole Beutrice kwa kufikia ukomo kwa kuamini ktk katiba kuwa ndio pekee inayoweza kuliweka taifa salama🤔! Ungepata muda zaidi ungegundua jinsi ulivyokuwa umepotea kimtazamo baada ya kugundua kuwa siyo katiba mpya itakayoiweka Tz salama bali nguvu tofauti kabisa😜! Hapana rudi tuendelee kujadiri i see😜!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…