Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

Tafuta pesa tu haya mambo ya siasa yataku pasua kichwa

Ova
 
Naam, Mimi ni mwanachama wa muda mrefu hapa kwenye ukurasa wa Siasa. Nimetoa mchango wangu kwa umoja huu kupitia ukurasa huu. Nimerekebisha baadhi ya mambo kutokana na hoja zangu na niseme tu nimekuwa nikifarijika sana pale ninaposhauri au kutoa hoja ikaleta positive impact kwenye jamii.

Nimefika kikomo cha kushiriki nanyi, nimefika wakati ambao bila ridhaa yangu nawajibika kukaa pembeni bila kuandika Wala kuona chochote kuhusu hata wale watakaosoma ujumbe huu. Nafika ukomo na nauona ukomo wangu.

Ninapoaga leo hapa tarehe 23/06/2021 saa 23: 15 usiku naaga kwa uchungu mkubwa kwamba moja ya Jambo nililopigania kwenye jukwaa, kwenye jamii na kwenye mitandao ya kijamii halijafanikiwa kutokea na naamini sitoweza kushuhudia likitokea. Jambo ilo si jingine Bali ni KATIBA MPYA YA JMT.

Nilitamani nimshirikishe Mwalimu Nyerere juu ya hatua hii huko alipo endapo ningekutana naye lakini nasikitika kwamba sitoweza kumwambia chochote juu ya agenda hii. Ni maumivu makubwa.

Niliipigania Katiba baada ya kuona kwamba mfumo wakusimamia haki nchini haupo Tena kwenye mategemeo ya sheria za nchi. Mfumo huo toka enzi ya Mkapa hadi leo hii awamu ya sita umebaki kutawaliwa na maamuzi ya mtu mmoja ambayo ni maamuzi ya Mkuu wa nchi.

Niliipigania Katiba mpya baada ya kuona taifa langu linazidi kuongeza Kinga za kushtakiwa kwa kundi la wanasiasa na Watumishi wa umma. Mkakati huu wakutochukuliwa hatua za kisheria kwa viongozi utaliua taifa na ndipo nilipoona natakiwa kusimia hoja ya Katiba mpya itakayotamka na kutekelezwa kwa amri au takwa la binadamu wote wapo sawa chini ya sheria.

Nilijaribu na naondoka bila kuiona, naamini waliobaki watazidi kuisimamia hii na itapatikana kabla Taifa halijapoteza kabisa imani miongoni mwa wananchi na kuanza kusambaratika.

Ninaponyamaza na nikiwa katika maumivu makubwa nimepata nguvu yakuuandikia ulimwengu kwamba Tanzania inahitaji katiba mpya.

Kwa Mhe. Rais, kwa Hali ilipofikia Sasa, maendeleo pekee unayoweza kuwarithisha Watanzania wakiwemo watoto wako na wajukuu ni katiba mpya. Jenga barabara, vivuko nk lakini tambua kiu ya umma wa Watanzania inahitaji katiba inayotokana na kizazi kilichopo Sasa.

Wasaidie Watanzania, wape katiba mpya. Anzisha mchakato, la sivyo kelele na mwangwi wa kilio cha Watanzania kitaambatana nawe Kama kinavyoambatana na mzee Kikwete hata baada ya kustaafu. Naondoka mie, nakuomba Jambo naamini sitoiona katiba hiyo ila wape wananchi katiba mpya.

Niwashukuruni sana na niwaombe msisite kuendelee kumkumbusha kuhusu maumivu yangu juu ya Tanzania mpya. Endapo lolote litatokea may be ntarudi ila nimefika ukomo. Mwenyenzi Mungu mtoa maarifa na njia akawajaze ufunuo na maono ya mwisho mwema Kama Mimi. Mkaondoke mkiwa kwenye toba na siyo mkiwa dhambini.

Naitwa Beatrice Kamugisha (nick name), naandika kutoka Regency Dar es salaam Tanzania.
Mkuu, why unakata tamaa kisa kuumwa, kuumwa sio kufa Kama siku zako za kuishi zipo, aliekuleta Dunian ndie ajuaye Saa na wakati wako kuondoka duniani

Kweli wenda upo katika maumivu makali, ila sio passport kwamba unakufa ,

Nimatumain yangu hayo maumivu makali, yatakauka, dawa uzitumiazo zitafanya kazi Mara dufu kupitia yeye, na imekua mkuu uwe mzima kuanzia Sasa,
 
Pole Bea,
Wewe ni mwanaharakati mwenye uelewa na upeo mkubwa sana wa mambo. Sijawahi kujuta kukukubali. Kama unaumwa Mungu akupe nafuu maana bado jukwaa linakuhtaji.
 
Rais herself alisema msubiri kidogo,sio sana,,hivyo mtegemee baada ya miaka mitatu hadi mitano mchakato unakuja,,hawezi mtu kukaa ikulu miezi 3,utegemee baada ya mwezi akupe katiba mpya..
Wow! Ahadi nzuri sana hii. Nilikuwa sijaipata mkuu.
 
Pole sana, nchi hii inatia hasira sana! Unajiuliza hivi ambao hawaitaki katiba mpya wana agenda gani ya siri?


Wao wanajifanya hamnazo kutokutengeneza nchi ya haki yenye mifumo imara wanabaki kuegemeza akili zetu kwa whites kila kukicha ingali hao wenyewe wamejiwekea mifumo safi, ajabu sana hii.


Yaani wewe hutaki haki halafu unaomba msaada kwa mtu anaependa haki kwa nini?

Wewe hutaki katiba yenye usawa isiyojali makundi ya watu halafu unatembeza bakuli kila uchao kwa wenzako waliojiwekea katiba safii na wanailinda kwa ajili ya vizazi vyao, hii akili nayo ina chongo kama sio kengeza.

Watala wetu kuanzia juu mpaka chini sio wazalendo kabisa bali wapo pale just kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Mungu akutie nguvu.
 
Mkuu tatizo ni nini? Hapo Regency unasumbuliwa na nini kwa muda gani? Nakuomba utubu mazambi yako yote kama unahisi upo katika hatua za mwisho za kufariki. Sisi wote njia yetu moja,ni suala la muda tu
Kwanza tuanzie hapa.....!!!! Regency IPI kwa maana hata Migombani panaitwa hivyo..,
 
Pole sana mkuu, hiyo hospitali kuna uhaba mkubwa wa vitanda, umepata kitanda kweli?
Kwani ni Hospital.....!!! Siyo ile ya Migombani mkuu.....!!!??? Nadhani Bitrice anaumwa ugonjwa unaoitwa KATIBA....na usipouangalia unaweza kuuondoa maisha kwani wengi wameumwa ugonjwa bila Mafanikio
 
Mama Koku pole sana yaliyokupata.
Maudhui zako zilikua nzuri na zenye mantiki. Ni moja tu niliyokupinga kwa hoja.
Pole sana. Nakuja pm
 
This is very bad. Last seen ya@Beatrice Kamugusha ni 11:34pm ambo kweli ndiyo muda alipost hii thread yake. Mungu mpiganie apone. We still need her badly. Mungu mnusuru Beatrice. Nimesikitika mno 😭😭😭
 
Back
Top Bottom