Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

Naomba kuwaaga rasmi Wana JF, nikipona tutakuwa pamoja tena

Mbona Kuna uzi nimeuona hapa jukwaani kwamba amefariki usiku wa kuamkia leo?
This is very bad. Last seen ya@Beatrice Kamugusha ni 11:34pm ambo kweli ndiyo muda alipost hii thread yake. Mungu mpiganie apone. We still need her badly. Mungu mnusuru Beatrice. Nimesikitika mno [emoji24][emoji24][emoji24]
No no no jamani. Mungu naomba isiwe kweli
Uzi kweli uliwekwa lakini naona umefutwa. Apumzike kwa amani [emoji51][emoji1545][emoji1545]

Screenshot_20210625-132338.jpg
 
Pole sana mkuu, Mwenyezi Mungu mweza wa yote akawe faraja yako kuu na yote yawe heri kwa mapenzi yake, Amina.
 
Hii tabia ya madaktari kuwaambia wagonjwa wao wana miezi mitatu au sita ya kuishi siipendi kusema kweli inawaongezea hofu wagonjwa ndugu, jamaa, familia na marafiki wa karibu. Miaka kama mitano iliyopita jirani yangu mama yake alikuwa anasumbuliwa na kansa kwa kipindi kirefu. Basi ile 2016 wakamwambia mwanae mgonjwa ana miezi sita tu ya kuishi.

Basi jamaa akajiandaa ule mwezi wa sita alioambiwa mama yake atafariki hakufariki alichukua likizo ya mwezi ikakatika. Akarudi kazini lakini huku akitegemea mama yake atafariki wakati wowote lakini yule mama aliishi kwa miaka mingine miwili na nusu ndiyo akafariki. Hii tabia ya kumwambia mgonjwa ana muda fulani wa kuishi madaktari wangeachana nayo.
Tabia hiyo iko sana ulaya, nakumbuka siku moja nilitembelea hospitali moja inayojihusisha na tiba ya magonjwa ya tropiki ikiwemo kifua kikuu. Nilichokiona huko na kusikia kutoka kwa wagonjwa wenyewe huwezi kuamini kuwa katika bara la ulaya bado kuna "Concentration Camps" zinazoendeshwa kihalali kabisa.

Hii inaweza kuwa sababu kuu ya watu kunyemelewa na mawazo ya kutaka kujiua. Hapa kwetu pia katika siku za hivi karibuni fani ya udaktari imepwaja sana kiasi cha kutokujali maadaili ya kazi zao na hivyo kutoa siri za wagonjwa kirahisi rahisi tu.

Maadili ya kazi na hasa viapo vya kitaaluma havizingatiwi sana siku hizi.
 
kuna wengine wawiali ambao sikumbuki majina yao zaidi ya hao uliowataja. Mmoja alisema ukweli kuwa alikuwa diagnosed na kansa, na akapita makaburini pale kinondoni kuangalia sehemu atakapozikwa; huyu alikuwa mkweli na wala maneno yake hayakuwa yamepinda. Yule mwingine alikuwa anatoa lawama sana na kutishia kujiua kumbe kweli akajiua kweli kweli; hakueleweka kwa watu wengie mpaka baada ya kuwa amejiua.
Wa makaburini alikuwa na pancreatic cancer stage 4..nami nimemsahau jina..
 
Pole Sana Beatrice! Mola akusimamie upone kwa haraka! Lkn humu jamvini watu wanaweza kukusaidia tiba Beatrice, usikate tamaa!
 
Pole sana Mkuu...

Mungu wa upendo na huruma akusimamie urejeshe afya yako.
 
Mkuu umesahau kuandika namba yako ya simu, Sasa utapaje huo uteuzi, Maana umetumia akili kubwa kupata attention.
 
Back
Top Bottom