Naomba mamlaka zinazo husika kushughulikia hii changamoto ya watoto kwenda vijiweni

Naomba mamlaka zinazo husika kushughulikia hii changamoto ya watoto kwenda vijiweni

Je ni sahihi watoto kwenda vijiweni kucheza draft,bao na michezo mwingine kama hiyo???

  • Walimu, wazazi na jamii

    Votes: 0 0.0%
  • Walimu,wazazi na jamii

    Votes: 0 0.0%
  • Ke na me

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    0
Joined
Jan 7, 2025
Posts
7
Reaction score
9
Tunapo waacha watoto kudhurura na kuwapa uhuru ulopitiliza bila kujali kesho yao ndo chanzo cha watoto kuwa wazembe na kushindwa kujifunza vitu vya msingi kama masomo hii ndo sababu wanavuna ziro huko mashuleni. Wazazi chukuweni hatua stahiki ✍️✍️
 
Ni ushauri ambao naamini utasaidia jamii na kuwasaidia vijana kufikia ndoto zao, tukumbuke kuwa wao wakati mwingine wanakuwa hawaelewi madhara ya hiyo michezo ✍️✍️
 
Jukumu la malezi ya mtoto linaanzia nyumbani, kwa mzazi/mlezi wa mtoto.
U-busy, uzembe na kutojali kwa wazazi/ walezi ndio kunapelekea watoto kujilea wanavyotaka. Kitu muhimu watu wazae pale wakiwa tayari kubeba jukumu la malezi na wazae kwa uzazi wa mpango.
 
Wazazi ambao mna watoto wanasoma Day hasa kwa jiji la Dar mjitahidi sana kuwafatilia.
Watoto wa shule za msingi na sekondari wanacheza Michezo ya hela(vibati),
Wanacheza vindege(aviator)
Wanaachiwa bodaboda dayworker
Wanafanya vitu kibao ambavyo ni vya juu ya umri wao,
Jitahidin jamani muwafatilie watoto wenu.
 
Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom