Sahihi mkuu!Mkuu upo sahihi kabisa tena 100% dini inamwezesha mtu kuishi kwa upendo ambapo ndo golden rule ya kumfikia Mungu. Wanatheolojia wote hutamani waamini watumie akili zao ili kusolve changamoto za kimaisha na kama itashindikana ndo nguvu ya Kimungu ifanye kazi. Cha ajabu waamini wamekuwa waraibu wa dini. Huku mtaani tumezika mtoto wa miaka 7 baada ya kung'atwa na nyoka mama yake ni mlokole alianza kukemea eti toka shetani. Bila kujua snake venom husambaa faster kwenye damu.
Siwabezi washika dini. Lakini hebu tuangalie huo uraibu wa kidini husababishwa na nini?Mkuu upo sahihi kabisa tena 100% dini inamwezesha mtu kuishi kwa upendo ambapo ndo golden rule ya kumfikia Mungu. Wanatheolojia wote hutamani waamini watumie akili zao ili kusolve changamoto za kimaisha na kama itashindikana ndo nguvu ya Kimungu ifanye kazi. Cha ajabu waamini wamekuwa waraibu wa dini. Huku mtaani tumezika mtoto wa miaka 7 baada ya kung'atwa na nyoka mama yake ni mlokole alianza kukemea eti toka shetani. Bila kujua snake venom husambaa faster kwenye damu.
mkuu uraibu wa kidini weng wamefuata mkumbo wamekuwa watumwa wa dini zao wakiogopa ukiacha dini unachomwa moto siku ya mwishoSiwabezi washika dini. Lakini hebu tuangalie huo uraibu wa kidini husababishwa na nini?
Imani inathibitishwamkuu uraibu wa kidini weng wamefuata mkumbo wamekuwa watumwa wa dini zao wakiogopa ukiacha dini unachomwa moto siku ya mwisho
Umeweka jibu shortly but loudly clear mkuu.Kwa maoni yangu, Dini ni mifumo ya mwanadamu ili kucontrol.
Imani ni sehemu ya mwanadamu, ndo inatengeneza matumaini. Kila binadamu ana imani.
Dini zinajikita zaidi kwenye control kuliko uhitaji wa inachotaka imani. Hata serikali inazitumia sana dini ikitaka jambo lake.Umeweka jibu shortly but loudly clear mkuu.
Tuje kwenye uhalisia.
Je kuunganisha dini na imani kunasaidia au kubomoa vipi sudi ya mlengwa?
Mhusika mwenye imani.Je nani anapaswa kuitenganisha dini na imani?
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Yaani imani peke yake haitoshi; lazima ionekane katika matendo."Hakika wale walioamini na wakatenda mema..." (Qur'an 2:25 na sehemu nyingi nyingine)
Na pia:"Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu." (Qur'an 3:19)
Kwa hiyo, katika Uislamu, imani ndiyo msingi, dini ndiyo njia ya kuiishi hiyo imani. Kuzitenganisha ni kama kutenganisha roho na mwili; kila kimoja kinampunguzia kingine maana yake."Leo nimekukamilishieni dini yenu, nimekutimizieni neema Yangu juu yenu, na nimewaridhia Uislamu uwe dini yenu." (Qur'an 5:3)
Mkuu
Nimezaliwa na kulelewa dini ya Kikristo kama wanavyoita.
Nilikuja kugundua kuwa Yesu alitaka wote wamuaminio wawe Wanafunzi wake. Lakini pale Antiokia enzi za Mitume walianza kujiita Wakristo yaani wafuasi wa Kristo.
Baada ya Wanamatengenezo wa kwanza kuamua kujitenga na dini ya ulimwengu yaani Katoliki, waliitwa Protestants yaani WAASI wa KIDINI/ IMANI. Ambapo ndani yake zipo dini nyingi zinazojiita za Kikristo. Hapo ndipo sasa tunaona Walokole, Waanglikana, Menonite, Wafuasi wa Luther (Waluteri) na kadhalika.
Yesu alifanya huduma yake kila mahala. Aliingia hadi misikitini (Madinagogi) ambapo ushahidi ni yule mgonjwa aliyeshushwa kitanda chake na kamba akiwa sinagogini na akamponya. Leo mwambie mlokole kuwa aende msikitini Ijumaa akavune ngano ya Bwana, atakutoa pepo maana ataona huu ni wazimu.
Dini inabagua
Dini inaweka masharti
Dini inamiliki utashi binafsi
Dini inadogosha Imani halali kwa Muumba
Na pia:"Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu." (Qur'an 3:19)
Kama dini ingekuwa ni kifungo cha wanadamu, kwa nini Mwenyezi Mungu aseme Ameikamilisha na kuiridhia?"Leo nimekukamilishieni dini yenu, nimewatimizieni neema Yangu, na nimewaridhia Uislamu uwe dini yenu." (Qur'an 5:3)
Kuhusu Yesu, ni kweli aliingia masinagogini kwa sababu hayo yalikuwa sehemu za ibada za Mayahudi, nao alikuwa ametumwa kwao. Biblia yenyewe inamnukuu akisema:"Wala msiwe miongoni mwa wale walioigawa dini yao na wakawa makundi." (Qur'an 30:31–32)
Hivyo kuingia kwake sinagogini hakumaanishi kwamba mipaka ya ibada haipo, bali alikuwa anawahubiria watu aliotumwa kwao."Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli." (Mathayo 15:24)
Mwenyezi Mungu hakumlazimisha mtu kuamini. Anamwonyesha njia, kisha mtu anachagua."Hakuna kulazimisha katika dini." (Qur'an 2:256)
MkuuUmezungumzia historia ya Ukristo na madhehebu yake, lakini hitimisho lako kwamba "dini inadogosha imani" si lazima liwe sahihi.
Kwa mtazamo wa Uislamu, dini si adui wa imani; dini ndiyo mwongozo wa imani.
Qur'an inasema:
Na pia:
Kama dini ingekuwa ni kifungo cha wanadamu, kwa nini Mwenyezi Mungu aseme Ameikamilisha na kuiridhia?
Ni kweli watu wanaweza kugawanyika kwa madhehebu, lakini hilo si kosa la dini bali la wanadamu. Qur'an ilionya mapema:
Kuhusu Yesu, ni kweli aliingia masinagogini kwa sababu hayo yalikuwa sehemu za ibada za Mayahudi, nao alikuwa ametumwa kwao. Biblia yenyewe inamnukuu akisema:
Hivyo kuingia kwake sinagogini hakumaanishi kwamba mipaka ya ibada haipo, bali alikuwa anawahubiria watu aliotumwa kwao.
Katika Uislamu, Msikiti umefunguliwa kwa kila anayetaka kujifunza kwa heshima. Watu wengi wameingia misikitini kama wageni, watafiti au waandishi wa habari bila kuzuiwa. Lakini kila dini ina utaratibu wa ibada zake; hilo si ubaguzi bali ni utaratibu.
Mwishowe, si sahihi kusema dini inamiliki utashi wa mtu. Qur'an inasema wazi:
Mwenyezi Mungu hakumlazimisha mtu kuamini. Anamwonyesha njia, kisha mtu anachagua.
Kwa hiyo tatizo si dini ya Mwenyezi Mungu; tatizo ni pale wanadamu wanapoibadilisha, wanapoigawa au wanapotanguliza matakwa yao kuliko ufunuo. Imani bila mwongozo inaweza kumfanya kila mtu ajitengenezee "ukweli" wake. Ndiyo maana Mwenyezi Mungu aliteremsha dini ili imani iwe na msingi, mwelekeo na mipaka ya haki.
Mkuu
Umeelezea kwa kina kuhusu dini ambapo mlengo wako umeelekeza kumpa dini Mwenyezi Mungu.
Unaweza kunidadavulia kuhusu IMANI hususan chimbuko na urari wake? Refference zituelimishe Imani.
Dini baki nayo, maana Islam ni dini based society, sasa twende kwenye imani.
Na Mtume Muhammad ﷺ alipoulizwa kuhusu imani alisema:"Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waumini pia. Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake na Mitume Wake..." (Surah Al-Baqarah 2:285)
Hivyo chimbuko la imani katika Uislamu ni wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, si falsafa wala mawazo ya wanadamu."Imani ni kumuamini Mwenyezi Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake, Siku ya Mwisho na kuamini Qadar, kheri yake na shari yake." (Sahih Muslim)
Hivyo imani ya Kiislamu imejengwa juu ya elimu, ushahidi na ufunuo."Sema: Hii ndio njia yangu; ninamwita kwa Mwenyezi Mungu kwa elimu ya yakini..." (Surah Yusuf 12:108)
Kwa hiyo hata Biblia inasema chanzo cha imani ni Neno la Mungu, si utamaduni wala jamii."Basi imani chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo." (Warumi 10:17)
Lakini Waebrania haikusema mtu aamini bila msingi; ndiyo maana Warumi 10:17 ikaeleza kuwa imani huja kwa kusikia Neno la Mungu."Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana."
Hii inaonyesha kwamba imani ya kweli si kukiri kwa mdomo tu bali lazima iambatane na utiifu kwa Mungu."Wewe waamini kwamba Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao wanaamini na kutetemeka." (Yakobo 2:19)
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu." (Yohana 14:15)
Wewe una maelezo gani kuhusu imani maana maelezo yako kuanzia dini mpaka imani umeangukia kwenye mtego wa kudandia maelezo ya watu ambao nao walitafuta maana wakatuletea kwa tafsiri zao.Umeuliza kuhusu imani, si dini. Sawa, tuangalie kwa kutumia maandiko.
Kwanza, imani si hisia wala maoni ya mtu. Imani ni kumwamini Mungu na kuamini yale aliyoyafunua.
Kwa mtazamo wa Uislamu:
Qur'an inafafanua imani wazi kabisa:
Na Mtume Muhammad ﷺ alipoulizwa kuhusu imani alisema:
Hivyo chimbuko la imani katika Uislamu ni wahyi (ufunuo) kutoka kwa Mwenyezi Mungu, si falsafa wala mawazo ya wanadamu.
Pia Qur'an inasema:
Hivyo imani ya Kiislamu imejengwa juu ya elimu, ushahidi na ufunuo.
Sasa tuangalie Biblia.
Biblia nayo haisemi kwamba imani ni mawazo ya mtu. Inasema:
Kwa hiyo hata Biblia inasema chanzo cha imani ni Neno la Mungu, si utamaduni wala jamii.
Waebrania 11:1 inasema:
Lakini Waebrania haikusema mtu aamini bila msingi; ndiyo maana Warumi 10:17 ikaeleza kuwa imani huja kwa kusikia Neno la Mungu.
Hata Yakobo anasema:
Hii inaonyesha kwamba imani ya kweli si kukiri kwa mdomo tu bali lazima iambatane na utiifu kwa Mungu.
Sasa kuhusu swali lako la urari wa imani.
Katika Uislamu, imani na dini haviwezi kutenganishwa.
Imani ni msingi.
Uislamu (matendo ya dini) ni matokeo ya imani.
Ihsan ni ukamilifu wa ibada.
Ndiyo maana Hadith ya Jibril ilitenganisha kwa ufafanuzi:
Imani
Uislamu
Ihsan
Lakini zote ni sehemu za dini moja.
Hata katika Biblia Yesu alisema:
Hivyo hata kwa mafundisho ya Yesu, imani ya kweli lazima ionekane kwa utiifu.
Kwa hiyo si sahihi kusema "tuache dini tubaki na imani", kwa sababu maandiko yote mawili yanaonyesha kuwa imani ndiyo mzizi na dini (utiifu kwa Mungu) ndiyo tunda. Ukikata mzizi, tunda haliwezi kuwepo; na ukidai una tunda bila mzizi, nalo haliwezi kudumu.
Wewe una maelezo gani kuhusu imani maana maelezo yako kuanzia dini mpaka imani umeangukia kwenye mtego wa kudandia maelezo ya watu ambao nao walitafuta maana wakatuletea kwa tafsiri zao.
Usituingize kwenye falacy zilizoshindwa. Dini imejengwa kwenye misingi ya udhibiti, kupoka uhuru wa fikra ba ubaguzi unaotokana na kujithaminisha kwa jamii moja dhidi ya jamii nyingine.
Ufundi wa kukariri aya za misahafu siyo dalili ya ufahamu bali ni bondage ya kuhairisha uhuru wa kufikiri ili kujenga uelewa.
Uje na hoja yako yenye kireflect uhalishia wa tunayoyaishi
Haya njoo na hoja mkuu.Nimegundua huna hoja ya kujibu, ndiyo maana umekimbilia maneno kama "fallacy", "bondage" na "uhuru wa kufikiri" bila hata kuyafafanua.
Unasema dini ni mfumo wa udhibiti. Huo ni msimamo wako, si hoja iliyothibitishwa. Uthibitishe kwa ushahidi, si kwa kauli za jumla.
Unasema kukariri maandiko si ufahamu. Sawa. Lakini wewe unaleta madai bila hata chanzo kimoja cha kuthibitisha unachokisema. Tofauti ni kwamba mimi ninanukuu msingi ninaousimamia, wewe unanukuu maoni yako mwenyewe kana kwamba ndiyo ukweli wa mwisho.
Unadai dini imejengwa juu ya ubaguzi. Basi eleza kwa hoja: je, falsafa, utaifa, ujamaa, ubepari na hata ukafiri havijawahi kujenga ubaguzi au kumwaga damu? Kama jibu ni ndiyo, kwa nini unailaumu dini peke yake? Hiyo ndiyo inaitwa double standard.
Pia unasema nitumie "uhalisia tunaouishi". Ukweli wa kitu haupimwi kwa hali ya jamii bali kwa ushahidi. Zamani watu waliishi wakiamini dunia ni tambarare; uhalisia wao haukuifanya iwe tambarare.
Mwisho, unazungumzia "uhuru wa kufikiri", lakini kila unapokutana na aya au ushahidi kutoka kwenye maandiko unaukataa bila kuujibu. Huo si uhuru wa kufikiri; huo ni uhuru wa kukataa ushahidi usiokubaliana na msimamo wako.
Kwa hiyo acha maneno makubwa yasiyo na maudhui. Kama una hoja, ijibu hoja kwa hoja. Kama huna, usijifiche nyuma ya maneno kama "fallacy", "bondage" na "critical thinking". Maneno hayo hayashindi hoja; ushahidi ndio unaoshinda hoja.
Umemaliza kila kitu. Niongezee kuwa maisha bila imani huwezifanya chochote. Kila kitu unachofanya kinaanzia katika imani. Unapaswa kuamini katika kila unachokifanya, na kuamini katika wewe hata kama hakuna anayeamini njia zako. (Hapa ndipo ilipolala nguvu ya imani).Imani ni kukubali au kuamini jambo kuwa la kweli, hata kama ushahidi wake hauonekani moja kwa moja.
Dini ni mfumo uliopangwa wa imani, ibada, maadili, na desturi unaounganisha waumini katika namna fulani ya kumwabudu Mungu au kueleza maswali ya msingi kuhusu maisha. Dini mara nyingi huwa na maandiko, viongozi, na taasisi.
Mtu anaweza:
• Kuwa na imani ya kiroho bila kufuata dini yoyote.
• Kufuata dini lakini imani yake iwe dhaifu au ya mazoea.
• Asiwe na dini wala imani ya nguvu kuhusu mambo ya kiroho.
Watu wengi, imani huwapa maana ya maisha, matumaini, na msingi wa maamuzi ya kimaadili
Dini inaweza kutoa utambulisho wa kijamii, mshikamano, mfumo wa maadili, ibada, na utamaduni wa pamoja. Hata hivyo, inaweza pia kutumiwa vibaya kwa udhibiti wa kisiasa au kijamii, jambo ambalo limeonekana katika vipindi mbalimbali vya historia
Imani ni kukubali au kuamini jambo kuwa la kweli, hata kama ushahidi wake hauonekani moja kwa moja.
Dini ni mfumo uliopangwa wa imani, ibada, maadili, na desturi unaounganisha waumini katika namna fulani ya kumwabudu Mungu au kueleza maswali ya msingi kuhusu maisha. Dini mara nyingi huwa na maandiko, viongozi, na taasisi.
Mtu anaweza:
• Kuwa na imani ya kiroho bila kufuata dini yoyote.
• Kufuata dini lakini imani yake iwe dhaifu au ya mazoea.
• Asiwe na dini wala imani ya nguvu kuhusu mambo ya kiroho.
Watu wengi, imani huwapa maana ya maisha, matumaini, na msingi wa maamuzi ya kimaadili
Dini inaweza kutoa utambulisho wa kijamii, mshikamano, mfumo wa maadili, ibada, na utamaduni wa pamoja. Hata hivyo, inaweza pia kutumiwa vibaya kwa udhibiti wa kisiasa au kijamii, jambo ambalo limeonekana katika vipindi mbalimbali vya historia