Imani ni katika ulimwengu wa kiroho + kisaikolojia. Ulishakuwa nayo ipo. Labda sasa uulize ni vitu gani vinamfanya mtu akuze au kufifisha imani yake.ni kweli dini inadhibiti je haisaidii kumfanya mtu kuwa na utambuzi na itikadi kwenye fikra zake?
Je kipi kinamfanya mtu kuwa na imani?
Haya njoo na hoja mkuu.
Nisikukwaze kwenye uhuru wa fikra.
Imani ni katika ulimwengu wa kiroho + kisaikolojia. Ulishakuwa nayo ipo. Labda sasa uulize ni vitu gani vinamfanya mtu akuze au kufifisha imani yake.
Wana falsafa wana kitu wanahitab"mysticism" or intuition. Ndio ile katika ulimwengu wa kiroho wanasema ufahamu wa ndani. Ndio maana wanasema kila mtu ana roho inayomuongoza ndani yake.
Hiyo roho au ufahamu ndio unaomfanya mtu ajue kitu hata kama hajapata kufundishwa, au hata akifundishwa kuna ufahamu wa ndani unamwambia hiki ni kweli au sio kweli.
Kwa mfano; mtu akisema Simba ni mnyama hatari kwa mwanadamu. Hata kabla hujathibitisha aidha kwa kuona au kwa kusikia kuna spirt ya ndani itakwambia kitu. Kwa maana mtu au kiumbe chochote kama wanyama au ndege akiona na kitu cha hatari kuna sprit ya ndani inamharifu. (Ni psychology but also spritual).
Imani inakuzwa kutokana na real life experiences, matukio tunayokutana nayo aidha kwa kushuhudia au kwa kuambiwa. Lakini pia reasoning inaweza kukusaidia uamini au husiamini
Hujaelewa wewe. Nimekwambia kile ambacho spritually tunahita ufahamu wa ndani, mwanapsychology atakwambia kuhusu intuition, mwanafalsafa atakwambia kuhusu mysticism. Wote wanaelezea dhana moja katika lugha tofauti.Umechanganya dhana nne tofauti: imani, intuition (hisia ya ndani), psychology na mysticism, halafu ukaziita zote "imani." Huo si ufafanuzi, ni kuchanganya maneno.
Kwanza, intuition si uthibitisho wa ukweli. Watu wawili wanaweza kuwa na intuition zinazopingana, lakini ukweli hauwezi kuwa pande mbili. Kwa hiyo hisia ya ndani haiwezi kuwa kipimo cha mwisho cha ukweli.
Pili, ukisema kila mtu ana roho inayomwambia ukweli, mbona kuna wanaoamini Yesu ni Mungu, wengine si Mungu, wengine hawaamini Mungu kabisa, na wote wanasema "roho yangu imeniongoza"? Je, roho hizo zote zinatoa ukweli mmoja au zinapingana? Kama zinapingana, basi intuition si kipimo cha ukweli.
Tatu, mfano wako wa simba si mfano wa imani bali ni instinct ya kujilinda. Mtoto mdogo anaweza kumuendea simba bila hofu, na watu wanaofuga simba huishi nao. Hiyo inaonyesha kwamba unachokiita "roho ya ndani" mara nyingi ni uzoefu, mafunzo au silika ya kimaumbile, si uthibitisho wa ukweli wa kiroho.
Nne, umesema imani inakuzwa na uzoefu na reasoning. Hapo ndipo nakubaliana nusu. Lakini kama reasoning ni muhimu, basi imani lazima ikubali kuchunguzwa kwa hoja na ushahidi. Haiwezi kusema "hii ni kweli kwa sababu roho yangu imenambia."
Kwa hiyo swali langu ni rahisi:
Ni kipimo gani cha kutofautisha intuition ya kweli na intuition ya uongo?
Kama huna kipimo cha nje ya hisia zako, basi unachokiita "imani" kinabaki kuwa maoni binafsi, si maarifa yanayoweza kuthibitishwa.
Imani ya kweli haiogopi hoja. Inaweza kupimwa kwa mantiki, ushahidi na ufunuo. Lakini intuition peke yake haiwezi kuwa hakimu wa mwisho wa ukweli, kwa sababu hisia za wanadamu zinaweza kudanganya.
Umechanganya dhana nne tofauti: imani, intuition (hisia ya ndani), psychology na mysticism, halafu ukaziita zote "imani." Huo si ufafanuzi, ni kuchanganya maneno.
Kwanza, intuition si uthibitisho wa ukweli. Watu wawili wanaweza kuwa na intuition zinazopingana, lakini ukweli hauwezi kuwa pande mbili. Kwa hiyo hisia ya ndani haiwezi kuwa kipimo cha mwisho cha ukweli.
Pili, ukisema kila mtu ana roho inayomwambia ukweli, mbona kuna wanaoamini Yesu ni Mungu, wengine si Mungu, wengine hawaamini Mungu kabisa, na wote wanasema "roho yangu imeniongoza"? Je, roho hizo zote zinatoa ukweli mmoja au zinapingana? Kama zinapingana, basi intuition si kipimo cha ukweli.
Tatu, mfano wako wa simba si mfano wa imani bali ni instinct ya kujilinda. Mtoto mdogo anaweza kumuendea simba bila hofu, na watu wanaofuga simba huishi nao. Hiyo inaonyesha kwamba unachokiita "roho ya ndani" mara nyingi ni uzoefu, mafunzo au silika ya kimaumbile, si uthibitisho wa ukweli wa kiroho.
Nne, umesema imani inakuzwa na uzoefu na reasoning. Hapo ndipo nakubaliana nusu. Lakini kama reasoning ni muhimu, basi imani lazima ikubali kuchunguzwa kwa hoja na ushahidi. Haiwezi kusema "hii ni kweli kwa sababu roho yangu imenambia."
Kwa hiyo swali langu ni rahisi:
Ni kipimo gani cha kutofautisha intuition ya kweli na intuition ya uongo?
Kama huna kipimo cha nje ya hisia zako, basi unachokiita "imani" kinabaki kuwa maoni binafsi, si maarifa yanayoweza kuthibitishwa.
Imani ya kweli haiogopi hoja. Inaweza kupimwa kwa mantiki, ushahidi na ufunuo. Lakini intuition peke yake haiwezi kuwa hakimu wa mwisho wa ukweli, kwa sababu hisia za wanadamu zinaweza kudanganya.
Unasema kuhusu watu kusema Yesu ni Mungu, imani yao inawatuma hivyo. Kuna wengine pia waliamini Mungu wao ni mti, kuna wanadamu walijihita mungu etcHujaelewa wewe. Nimekwambia kile ambacho spritually tunahita ufahamu wa ndani, mwanapsychology atakwambia kuhusu intuition, mwanafalsafa atakwambia kuhusu mysticism. Wote wanaelezea dhana moja katika lugha tofauti.
Wewe umefanya tu kudadavua zaidi. Hisia za ndani na akili ya ndani, si ndio ufahamu wa ndani?
Ufahamu wa ndani koroho tunaambiwa kuna roho mtakatifu, alipo roho mtakatifu na shetani huingia pia. Roho mtakatifu akikwambia kuua ni mbaya, kuna roho mwingine atakwambia kuua ni kawaida. Pamoja na huo ukinzani kuna ile hali ya ndani ambayo inakufanya uchague upande mmoja wewe mwenyewe. Sio lazima kwamba nyote mchague upande sawa. Kote kunahubiriwa kwamba kuua ni kubaya baada ya maubiri na maandiko, au sheria wewe ndani yako unahisi nini kuhusu kuua?
Wanaofuga Simba nyumbani, kwahiyo wakimfuga ndio basi wamedhihirisha kuwa Simba sio mkali kwa mwanadamu? Yupo wapi huyo mtoto mdogo mwenye ujasiri wa kucheza mbele ya Simba wakati akiona senene tu anakimbia!
Nilimalizia kwa kusema masuala ya imani yanachagizwa pia na real life experiences aidha kwa kuona au kusimuliwa. Imani sio kitu unachofeza kukiona kwa macho wala kukigusa. Kwa mantiki hiyo tegemea opinionss tofautitofauti.
Hujaelewa wewe. Nimekwambia kile ambacho spritually tunahita ufahamu wa ndani, mwanapsychology atakwambia kuhusu intuition, mwanafalsafa atakwambia kuhusu mysticism. Wote wanaelezea dhana moja katika lugha tofauti.
Wewe umefanya tu kudadavua zaidi. Hisia za ndani na akili ya ndani, si ndio ufahamu wa ndani?
Ufahamu wa ndani koroho tunaambiwa kuna roho mtakatifu, alipo roho mtakatifu na shetani huingia pia. Roho mtakatifu akikwambia kuua ni mbaya, kuna roho mwingine atakwambia kuua ni kawaida. Pamoja na huo ukinzani kuna ile hali ya ndani ambayo inakufanya uchague upande mmoja wewe mwenyewe. Sio lazima kwamba nyote mchague upande sawa. Kote kunahubiriwa kwamba kuua ni kubaya baada ya maubiri na maandiko, au sheria wewe ndani yako unahisi nini kuhusu kuua?
Wanaofuga Simba nyumbani, kwahiyo wakimfuga ndio basi wamedhihirisha kuwa Simba sio mkali kwa mwanadamu? Yupo wapi huyo mtoto mdogo mwenye ujasiri wa kucheza mbele ya Simba wakati akiona senene tu anakimbia!
Nilimalizia kwa kusema masuala ya imani yanachagizwa pia na real life experiences aidha kwa kuona au kusimuliwa. Imani sio kitu unachofeza kukiona kwa macho wala kukigusa. Kwa mantiki hiyo tegemea opinionss tofautitofauti.
Kama hisia za ndani zingetosha, kwa nini Yohana aseme zijaribuni roho?"Msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu."
(1 Yohana 4:1)
Kwa hiyo Biblia yenyewe haifundishi kwamba hisia za ndani ndizo kipimo cha mwisho cha ukweli."Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote."
(Yeremia 17:9)
U
Unasema kuhusu watu kusema Yesu ni Mungu, imani yao inawatuma hivyo. Kuna wengine pia waliamini Mungu wao ni mti, kuna wanadamu walijihita mungu etc
By the way ipo hivi. Ukisoma biblia kwa mfano na maandiko mengi kuhusu masuala ya dini na kiroho ndipo akili inaanza kufunguka. Mtu hawezi kupata utambuzi wa ndani kama yeye mwenyewe hajaamua kufikia hatua hiyo.
Ndio maana unasikiaga wachungaji wanasema ulikuwa umifungwa sasa umefunguliwa, sasa upate kuijua kweli na kweli ikuweke huru. Kama mtu hajafikia level ya kutambua kweli hawezi kuijua kweli. Ukweli haupo kwa kila mtu bali anayeutafuta ataupata.
Waefeso 5:8
"Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru"
Waefeso 4:23
"na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu;
And be renewed in the spirit of your mind"
Kwa maana mtu ambaye bado amefungwa kwenye maandiko ya kidini, ile spirit ya ndani ya kweli haifanyi kazi kikamilifu. Mpaka mtu awe na utambuzi.
WE unadhani ni nini kinawafanya watu wakubaliane na masuala ya Mungu tangu kisa cha Mussa, richa ya kwamba hawakuwepo tangu enzi hizo? Mafundisho yapo wapo wanaopinga, ila bado mtu anachagua kuamini kuwa ni kweli Mungu yupo.
Kuhusu reasoning haijawai kuzuiwa
"Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu."
(1 Yohana 4:1)
"Kwa maana hata Shetani hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru."
(2 Wakorintho 11:14)
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu."
(Yohana 14:15)
"Wakayachunguza Maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo."
(Matendo 17:11)
Hatuna kinachoweza kuthibitisha imani moja kwa moja. Ndio maana inaitwa imani.Asante kwa maelezo yako. Lakini bado hujajibu hoja yangu kuu; umeeleza jinsi mtu anavyoweza kuamini, hujaeleza jinsi ya kuthibitisha kwamba anachoamini ni kweli.
Unasema mtu akisoma Biblia na maandiko ya kiroho "anafunguliwa." Sawa. Lakini Mhindu atasema akisoma Veda amefunguliwa. Mbudha atasema akisoma mafundisho ya Buddha amefunguliwa. Mwislamu atasema akisoma Qur'an amefunguliwa. Je, wote wamefunguliwa kwenye ukweli mmoja, au kila mmoja amefunguliwa kwenye dini yake?
Kama jibu ni "hapana", basi "kujisikia umefunguliwa" si kipimo cha ukweli, kwa sababu watu wa dini zinazopingana wote wanadai jambo hilo.
Umenukuu Waefeso 5:8 na 4:23. Hakuna tatizo na aya hizo. Lakini hazisemi kwamba kila mtu anayehisi amepata utambuzi basi hitimisho lake ni kweli. Ndiyo maana Biblia hiyo hiyo inaonya:
pia:
Kama kila anayehisi "amefunguliwa" angekuwa yuko sahihi, kwa nini Biblia ionye kuhusu roho za uongo na Shetani anayejifanya malaika wa nuru?
Umeniuliza kwa nini watu wanaamini habari za Musa ingawa hawakuwepo.
Jibu ni rahisi: kuamini jambo si uthibitisho kwamba jambo hilo ni kweli.
Watu wanaamini dini tofauti, falsafa tofauti na hata nadharia zinazopingana. Kitendo cha kuamini hakifanyi imani zote ziwe za kweli kwa wakati mmoja.
Yesu mwenyewe alisema:
Hakusema, "Mtasikia tu ndani yenu." Aliwataka watu wapime madai kwa mafundisho yake.
Na Mitume wa Beroya walifanya nini?
Hawakusema, "Tumefunguliwa, kwa hiyo hatuhitaji kuchunguza." Walichunguza kwanza.
Kwa hiyo reasoning haijazuiwa, nakubaliana nawe. Lakini reasoning ikitumika ipasavyo, lazima ikubali kuuliza swali hili:
Kwa nini nikubali kwamba "utambuzi wa ndani" wa Mkristo ni wa kweli, lakini "utambuzi wa ndani" wa Mwislamu, Mhindu au Mbudha si wa kweli, wakati wote wanadai wamefunguliwa kiroho?
Mpaka upate kipimo cha kutenganisha hizo "tambuzi", bado unabaki kueleza uzoefu wa kuamini, si uthibitisho wa ukweli.
Kimsingi kabisa, mungu ni cheo. Hata wewe unaweza kupata uungu. Jamii nyingi zimetengeneza misingi ya imani kwenye miungu, wakihisi kwamba ulimwengu lazima uliletwa na "muumba" flani.Nakumbuka nilimuuliza marehemu baba yangu (ambaye baada ya kustaafu alikuwa mchungaji wa kanisa lake) kuhusu uwepo wa majina ya Mungu kwenye makabila yetu. Nikihoji kuhusu Waafrika kuitwa wapagani, makafiri wasio na imani.
Alibaki kushangaa maana majina hata ya watoto kiafrika yanathibitisha uwepo wa Mungu.
Hizi dini ni bangi za watu kuwavuna kiakili wanajamii na kujimilikisha limitation ya kufikiri, kuhoji hata kupokea mawazo mapya
Dini imemeza taasisi huru ya familiaKimsingi kabisa, mungu ni cheo. Hata wewe unaweza kupata uungu. Jamii nyingi zimetengeneza misingi ya imani kwenye miungu, wakihisi kwamba ulimwengu lazima uliletwa na "muumba" flani.
Kwahiyo kama wachagga walimuabudu "Ruwa" haimaanishi mungu huyo ni sawa na "Yahweh" wa wakristo.
Usidhani kwamba kama imani fulani ina mungu, basi itakuwa sawa na yako yenye mungu pia.
Wazungu hawakusema tumekosa imani, bali walituita "heathens" yaani washamba, tusio na imani sahihi.
Dini ni muhimu! Ni lazima ziwe na mabavu! Dini zingewezaje kuzipa dhamana taasisi nyeti kama ndoa na familia bila kuwa na mamlaka? Wote tungeruhusiwa kufuata chochote tunachokiamini kungekuwa na migogoro kiasi gani?
Hapana, familia unayoijua wewe ya wazazi wawili na watoto(nuclear family) imeundwa na kupewa dhamana na dini ya kikristo.Dini imemeza taasisi huru ya familia
Hatuna kinachoweza kuthibitisha imani moja kwa moja. Ndio maana inaitwa imani.
Uwepo wa dini/madhehebu tofauti ni kutokana na tafsiri tofautitofauti kulingana na mapokeo. Nimesoma Quaran na Biblia, binafsi naona ni vitabu vinavyosisitiza jambo moja juu ya Mungu mmoja richa ya tofauti zinazoweza kuwemo. Unajua hivyo vitabu havikuandikwa na malaika wala havikushuka kutoka mbinguni, kwahiyo tafsiri za wanadamu pia zimechukua nafasi katika kuelezea neno la Mungu.
Hatuwezi kuthibitisha imani, ila imani huwa inazungumzia kitu ambacho kilitendeka. Suala la kuamini kama ni kweli au si kweli ni another case, na ndio dhana ya imani huchukua nafasi.
Mwanadamu amepewa hiari, na utashi. Kwa maana hiyo kila mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua upande wake.
Hakuna sehemu nimesema imani ya mkirsto ni bora kuliko imani ya mtu mwingine. (Sijasema popote). Imani ya mtu mmoja ni moja kati ya imani nyingine nyingi.
Ile ufahamu wa ndani niliokuwa nausemea mimi ni ule unaomuongoza mtu kuchagua upande. Kwa mfano kuna maandiko kuhusu kisa cha Yusufu, kisa cha Mussa, na kisa cha malaika walioshuka chini wakawafundisha wanadamu maarifa. Kuna anayesoma au kusimuliwa akakubali, na mwingine akakataa (ndani lazima nafsi izungumze kwamba hii kweli au si kweli). Hatukuwepo wakati Mungu anamuumba Adam but we choose to believe bila mashaka kabisa.
Kuhusu suala la imani tofautitofauti, ipo wazi "mimi ndiye Mungu wako husiabudu miungu mingine".
Hii kauli inathibitisha kuwa kuna miungu mingine, na vitabu vya historia vinathibitisha kulikuwa na miungu mingi sana ambayo mingine ilihishiwa nguvu, mingine watu watu wanaamini. Wewe unafikiri ni nini kinamuongoza mtu kuchagua upande?
By the way masuala ya imani ni subjective, tunaweza kukesha kwa sababu kila mtu anatetea anachokiamini.
Mawazo yangu yanatetea imani yangu, ila sio kupingana na imani ya mtu mwingine.
"Mtaifahamu kweli, nayo kweli itawaweka huru."
(Yohana 8:32)
"Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima."
(Yohana 14:6)
"Usiwe na miungu mingine ila mimi."
"Sisi twajua ya kuwa sanamu si kitu duniani, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu."
(1 Wakorintho 8:4)
Ninajuaje kama anayeniongiza ni Mungu, au ni upande mwingine? Very nice question.
Kutokana na maandiko niliyosoma kupitia baadhi vitabu vinavyogusia masuala ya dini inasemekana kuwa Mungu alipomuumba mwanadamu alimpatia maarifa, baada ya mwanadamu kuanza kuishi Mungu yapo mambo aliyokuwa akiyagundua zaidi kuhusu mwanadamu. Alituma pia malaika watoe maarifa "kitabu cha Enoko, sura ya 8", na hata Mwanzo, lakini pia Qur'an (Al-Baqarah). Maarifa haya yalihishi vizazi ha vizazi, mpaka leo.
Kwahiyo imani yangu inatokana na mkusanyiko wa maandiko mbalimbali.
Kupitia maandiko haya nimefunzwa kuwa Mungu anamtaka mwanadamu atende yaliyo mema kwa mfano; kufadhiriana, kupendana, kuhurumiana, nk. Na kuacha tamaa, hila, kiburi, chuki, nk
Nimefundishwa kuwa roho mtakatifu ananiongoza kutenda mema kama nilivyoyataja. Hivyo kulingana na miongozo niliyopewa napata kujua lipi jema na baya (utambuzi wa ndani pia ni sehemu ya kinachoniogoza kuthibitisha lipi jema au baya).
Ndio maana sijawasikia mtu amebaka, kuiba, kuua, akasema roho mtakatifu ameniongoza kubaka. Labda wewe umewaisikia?
Sijawai sikia mtu amenusurika ajali akasema shetani kaniokoa! We umewaisikia.
Baada ya hapo (spiritual faith) pengine inaweza isitosheleze kuelezea lakini inafanya sambamba kabisa philosophy (logic/reasoning), psychology.
Intuition: unahisi nini ndani yako baada ya kufanya jambo fulani?
Myticism: unafikirije ndani yako kuhusu ulilolifanya?
Spirt: Unaamini nini ndani yako?
Ndio maana wanasema baadhi ya injili zinathibitisha kuwa ufalme wa Mungu upo ndani yako wewe mwenyewe.
So, binafsi huwa naamini kutokana na namna nimepokea mafundisho.
"Watakuja saa ambayo kila mtu atakayewaua atadhani ya kuwa anamtolea Mungu ibada." (Yohana 16:2)
"Kwa habari ya bidii, naliwatesa Kanisa." (Wafilipi 3:6)
"Nalifanya hivyo kwa ujinga katika kutokuamini." (1 Timotheo 1:13)
Kama "kujisikia ndani" kungetosha, basi Yohana asingeagiza roho zipimwe."Msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu." (1 Yohana 4:1)
Tulipigwa na kitu kizito. Atheist hapa.Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Ahsante. Sasa umeeleza vizuri zaidi msimamo wako, lakini bado kuna tatizo la kimantiki na la kibiblia.
Kwanza, umesema unajua ni Roho Mtakatifu kwa sababu anakuelekeza kutenda mema. Lakini hilo halitoshi kuwa uthibitisho wa Roho Mtakatifu.
Kwa nini?
Kwa sababu hata mtu asiyeamini dini yoyote anaweza kuamini kwamba kuua, kuiba na kubaka ni vibaya. Je, hiyo ina maana kila mtu mwenye maadili mema anaongozwa na Roho Mtakatifu?
Ukisema "ndiyo", basi hata wasiomwamini Yesu wanayo Roho Mtakatifu.
Ukisema "hapana", basi maadili mema peke yake si kipimo cha Roho Mtakatifu.
Pili, umesema hujawahi kusikia mtu akisema "Roho Mtakatifu ameniongoza kubaka."
Lakini Biblia yako inaonyesha watu walifanya maovu wakidai wanamtumikia Mungu.
Yesu alisema:
Kwa hiyo Yesu mwenyewe alionya kwamba mtu anaweza kuamini kwa dhati kuwa anatenda mapenzi ya Mungu, kumbe amekosea.
Na Paulo kabla hajawa Mkristo alisema:
Na tena anakiri:
Paulo alikuwa na dhamiri safi, aliamini anamtumikia Mungu, lakini alikuwa amekosea.
Hiyo inaonyesha kwamba uaminifu wa mtu hauthibitishi ukweli wa anachoamini.
Tatu, umetaja Kitabu cha Enoko.
Lakini Kitabu cha Enoko si sehemu ya Biblia inayokubaliwa na makanisa mengi ya Kikristo. Kwa hiyo ukikitumia kuthibitisha mafundisho, tayari unatoka kwenye msingi wa Biblia uliokuwa unatetea mwanzo.
Nne, umesema intuition, mysticism na spirit vinafanya kazi pamoja.
Sina tatizo na hilo kama maelezo ya uzoefu wa mwanadamu. Lakini bado swali langu halijajibiwa:
Ukikutana na mtu wa dini nyingine ambaye naye anasema:
Nimesoma maandiko yangu.
Nimeongozwa kutenda mema.
Nina amani moyoni.
Nina utambuzi wa ndani.
Utamwambia kwa kipimo gani kwamba yeye amekosea na wewe uko sahihi?
Kwa sababu hadi sasa kipimo ulichotumia ndicho anachotumia pia.
Ndiyo maana Biblia inasema:
Kama "kujisikia ndani" kungetosha, basi Yohana asingeagiza roho zipimwe.
Kwa hiyo nakubaliana na wewe kwamba uzoefu wa ndani unaweza kumfanya mtu achague kuamini. Lakini uzoefu huo peke yake hauwezi kuthibitisha kwamba kile alichokiamini ni kweli. Hapo ndipo tofauti yetu ilipo.
Mungu pia anaagalia moyo wa mtu, aangalii mafundisho uliyonayo kichwani, aangalii unahuzuria mara ngapi kanisani, aangalii unatoa fungu la kumi. Anaagalia moyo wa mtu, nia na matendo yake.Sasa si ndio nilichosema.
Mungu yupo kwa wote wanaoamini na wasioamini β
Nafsi ya ndani kila mtu anayo, ila inaathiriwa na mazingira. Unajua ukielezea human nature kuna (Nature & Nurture) hivyo vitu vinainteract katika kumuongoza mwanadamu.
So intuition ya ndani haiwezi kujitosheleza kuthibitisha ila ni moja wapo ya factors.
Roho mtakatifu huenda ni lugha tu. Nitajie dini gani isiyosisitiza kuhusu ufahamu wa ndani. Ukisema Budha ndio hao kila siku wanaeleza kuhusu meditation.
Lakini pia, mimi mtu hawezi akaja na mti,dori, nk akanambia huyu ndio Mungu. Huo mti umeumbwa na nani? Huo mti ndio umeumba ulimwengu na watu wote?
Dhana ya Mungu wa juu the higher power imeshika nguvu katika ulimwengu wote. Hiyo nguvu inatoka wapi?
Kuna miungu mingi hata mi kijijini nimeshuhudia lakini mingi imepotea sahivi sioni.
Maandiko yanasema Mungu alimuumba pia Ibilis, lakini yeye alihasi na kutoa mafundisho ya uongo watu wakayashika wakaendana nayo. Ndio maana Mungu mwenyewe akashuka kuja kudhihirishia juu ya nguvu yake. Shetani hajaja kupinga adharani kuhusu haya madai, ila amedhihirisha anapanbana na huo upande. Which means ni vitaya falme. Kwa sababu wengi huoji kuhusu Mungu, lakini vipi kuhusu Shetan?
Mi nakumbuka shuleni watu wakishikwa mapepo ukikemea kwa jina kwa jina la Yesu, yanatoweka hata kama yakirudi tena. Waislam nao huomba kwa namna yao.
Yapo mengi ambayo nikitafakari, nafsi ya ndani inahitimisha kwamba huku ndo kwenyewe.
Mambo ya kiroho mwanadamu hawezi kuelezea kwa utimilifu. Lakini trust me kuna watu wamefunuliwa (richa ya kuwa kuna matrpeli pia). Ulishawai kusikia au kuona mtu kwamba amefunuliwa macho ya nafsi?
Ulimwengu wa kiroho una mambo mengi, kama hujafikiwa huwezi elewa. Lakini ufunuo wa Yoana wanasema, ukiushindakmtihani wa ulimwengu utafunuliwa na utayajua yale ambayo wanadamu wamekuwa wakibabaika nayo siku zote. Lakini lazima uhushinde huo mtihani.
Mambo mengine bila wisdom from above hutoboi. The higher power within someone.
Naimba tuhitimishe maisha yaendelee π
Masuala ya imani hayawezi kuwa universally proved with a single reality
Sasa si ndio nilichosema.

"Je, hawataitafakari Qur'an?" (Qur'an 4:82)
"Na wala usifuate jambo usilokuwa na elimu nalo." (Qur'an 17:36)
"Leo nimewakamilishieni dini yenu..." (Qur'an 5:3)
"Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'an, na hakika Sisi ndio tutakaoilinda." (Qur'an 15:9)