Kufunuliwa kwa kiroho hakutegemei dini wala dhehebu.Ahsante kwa majibu yako. Nimefurahi kwamba sasa umekubali jambo muhimu ulilokuwa umelikataa mwanzo, kwamba intuition au hisia za ndani peke yake hazitoshi kuthibitisha ukweli, bali ni factor mojawapo. Hapo tayari tumekubaliana.
Lakini hapo ndipo Uislamu unaweka msingi tofauti.
Qur'an haimwambii mwanadamu afuate hisia zake tu. Inamwambia atumie akili, ushahidi na wahyi kwa pamoja.
Kwa hiyo Uislamu hausimami juu ya "nilihisi", bali juu ya dalili (burhan), akili ('aql), na wahyi.
Umesema dini nyingi zinaongelea meditation na ufahamu wa ndani. Ni kweli. Lakini hiyo ndiyo hoja yangu.
Kama dini zote zina uzoefu wa kiroho unaofanana, basi uzoefu huo hauwezi kutumika kuthibitisha kwamba dini moja ndiyo sahihi.
Lazima kuwe na kipimo kingine kinachoweza kutenganisha ukweli na makosa.
Umesema pia huwezi kuabudu mti kwa sababu umeumbwa.
Nami nakubaliana kabisa na hilo.
Lakini sasa swali linaendelea:
Kama Muumba ni mmoja, kwa nini tumwamini kupitia mafundisho yaliyobadilika na yenye migongano, badala ya wahyi unaodaiwa kuhifadhiwa?
Qur'an inasema:
Na pia:
Hivyo Uislamu hauombi watu waamini kwa sababu ya ndoto, maono au hisia. Unawataka wachunguze wahyi wenyewe.
Umesema pia watu wamefunuliwa.
Nina swali moja tu:
Tukikubali kwamba kuna watu wa Kikristo, Kiislamu, Kihindu na Kibudha wote wanaodai wamefunuliwa, basi ufunuo wa nani ndiyo wa kweli?
Kama hakuna kipimo cha nje ya uzoefu wao, kila mmoja atasema "nimefunuliwa".
Ndiyo maana katika Uislamu hata mtu akiona malaika au akaota ndoto, ndoto hiyo haifanyi sheria wala haipingani na Qur'an. Wahyi ndiyo unaohukumu uzoefu, si uzoefu unaohukumu wahyi.
Umetaja pia mapepo kutoka kwa jina la Yesu.
Lakini hilo peke yake haliwezi kuthibitisha Ukristo kuwa wa kweli, kwa sababu hata Waislamu wanasoma Qur'an na ruqyah, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mapepo huondoka pia.
Hivyo tukitumia matukio ya kiroho kama kipimo, kila dini italeta ushuhuda wake.
Mwisho kabisa umesema masuala ya imani hayawezi kuthibitishwa universally.
Hapo ndipo ninatofautiana kidogo.
Si kila kitu kuhusu Mungu kinaweza kuthibitishwa kisayansi, lakini madai ya dini yanaweza kuchunguzwa kwa mantiki na ushahidi.
Swali si "nani amehisi zaidi?" bali ni:
Ni nani analeta wahyi uliohifadhiwa, usio na migongano, unaolingana na tauhidi ya Mitume wote kuanzia Adamu, Nuhu, Ibrahim, Musa na Isa (Yesu), na unaomwelekeza mwanadamu kumuabudu Mungu Mmoja bila mshirika?
Mimi nilipochunguza swali hilo bila kufuata hisia pekee, nikakuta Uislamu ndiyo unaojibu kwa uthabiti zaidi.
Tofauti huwa zinaletwa na tamaduni za watu wa maeneo husika tu. Mfano Qur'an iliathiriwa na tamaduni za waharabu, biblia pia imeathiriwa na tamaduni za warumi, wagiriki, na waingereza. Bado pia maandiko haya yana tafsiri za wanadamu. Ndio maana wanasema usome uelewe yale ya msingi, ila ukikalili na kumeza kila kitu kama kilivyo utatoka nje ya misingi.Kufunuliwa kwa kiroho hakutegemei dini wala dhehebu.
Watu walofunuliwa ndani yao wanatambua kwamba wakiristo, waislam, wajudah wanamuamini Mungu mmoja. Wale ambao hawaamini katika Mungu huyu wa Abraham/Ibrahim nao waje na facts zao sasa.
Mimi navyojua mtu anafunuliwa akitambua kweli na akaifikia kweli bila kujali kapitia njia gani ilimradi kafika.
Lakini ili ufunuliwe lazima upitie miongozo sahihi, miongoni mwa miongozo ni maandiko ya vitabu mbalimbali vya kiroho.
Kwa maana imeandikwa Hossea 4:6 "Watu wangu wanaagamia kwa kukosa maarifa". Maybe watu wengi hawajui masuala mengi kwa sababu hawana maarifa, na maarifa inabidi wayatafute.
Waefeso 5:8
"Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru"
Huenda wapo bado gizani 😂
Kufunuliwa kwa kiroho hakutegemei dini wala dhehebu.
Watu walofunuliwa ndani yao wanatambua kwamba wakiristo, waislam, wajudah wanamuamini Mungu mmoja. Wale ambao hawaamini katika Mungu huyu wa Abraham/Ibrahim nao waje na facts zao sasa.
Mimi navyojua mtu anafunuliwa akitambua kweli na akaifikia kweli bila kujali kapitia njia gani ilimradi kafika.
Lakini ili ufunuliwe lazima upitie miongozo sahihi, miongoni mwa miongozo ni maandiko ya vitabu mbalimbali vya kiroho.
Kwa maana imeandikwa Hossea 4:6 "Watu wangu wanaagamia kwa kukosa maarifa". Maybe watu wengi hawajui masuala mengi kwa sababu hawana maarifa, na maarifa inabidi wayatafute.
Waefeso 5:8
"Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru"
Huenda wapo bado gizani 😂
"Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja." (Marko 12:29)
"Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na nyinyi; kwamba tusimuabudu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote." (Qur'an 3:64)
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa."
"Leteni ushahidi wenu ikiwa nyinyi ni wakweli." (Qur'an 2:111)
Tofauti huwa zinaletwa na tamaduni za watu wa maeneo husika tu. Mfano Qur'an iliathiriwa na tamaduni za waharabu, biblia pia imeathiriwa na tamaduni za warumi, wagiriki, na waingereza. Bado pia maandiko haya yana tafsiri za wanadamu. Ndio maana wanasema usome uelewe yale ya msingi, ila ukikalili na kumeza kila kitu kama kilivyo utatoka nje ya misingi.
"Hakika Sisi tumeiteremsha Qur'an, na hakika Sisi ndio tutakaoilinda." (Qur'an 15:9)
"Hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mtoaji wa habari njema na mwonyaji." (Qur'an 34:28)
Kwenye dini unaamnini kwanza halafu ndiyo una-prove. Kwenye Sayansi, unaprove kwanza halafu ndiyo unaamini.Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Kwenye dini unaamnini kwanza halafu ndiyo una-prove. Kwenye Sayansi, unaprove kwanza halafu ndiyo unaamini.
Kwenye dini, ukiona kuwa kile ulichokiamini hauwezi kuki-prove; ujue umekosea; umepotea. Ni bora ukaachana kabisa na dini. Dini iliyo sahihi ni lazima ifikie mahali i-prove kile unachokiamini na ikishindwa, ujue hiyo siyo dini ya kweli!
Sio kila mwenye imani ana dini na sio kila mwenye dini ana imaniImani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
TakatakaNimegundua huna hoja ya kujibu, ndiyo maana umekimbilia maneno kama "fallacy", "bondage" na "uhuru wa kufikiri" bila hata kuyafafanua.
Unasema dini ni mfumo wa udhibiti. Huo ni msimamo wako, si hoja iliyothibitishwa. Uthibitishe kwa ushahidi, si kwa kauli za jumla.
Unasema kukariri maandiko si ufahamu. Sawa. Lakini wewe unaleta madai bila hata chanzo kimoja cha kuthibitisha unachokisema. Tofauti ni kwamba mimi ninanukuu msingi ninaousimamia, wewe unanukuu maoni yako mwenyewe kana kwamba ndiyo ukweli wa mwisho.
Unadai dini imejengwa juu ya ubaguzi. Basi eleza kwa hoja: je, falsafa, utaifa, ujamaa, ubepari na hata ukafiri havijawahi kujenga ubaguzi au kumwaga damu? Kama jibu ni ndiyo, kwa nini unailaumu dini peke yake? Hiyo ndiyo inaitwa double standard.
Pia unasema nitumie "uhalisia tunaouishi". Ukweli wa kitu haupimwi kwa hali ya jamii bali kwa ushahidi. Zamani watu waliishi wakiamini dunia ni tambarare; uhalisia wao haukuifanya iwe tambarare.
Mwisho, unazungumzia "uhuru wa kufikiri", lakini kila unapokutana na aya au ushahidi kutoka kwenye maandiko unaukataa bila kuujibu. Huo si uhuru wa kufikiri; huo ni uhuru wa kukataa ushahidi usiokubaliana na msimamo wako.
Kwa hiyo acha maneno makubwa yasiyo na maudhui. Kama una hoja, ijibu hoja kwa hoja. Kama huna, usijifiche nyuma ya maneno kama "fallacy", "bondage" na "critical thinking". Maneno hayo hayashindi hoja; ushahidi ndio unaoshinda hoja.
Jaribu kusoma kisha mbeleni wapo waliotoa maelezo ya kina zaidi ya nilichoandika.SIJASOMA MAELEZO YOTE YA PoST YAKO LAKINI NAOMBA NIKUJULIDJE KUWA PREMISES ULIZOANZA NAZO TAYARI ZINAONYESHA KUWA UNAJI-CONTRADICT. DHANA (HYPOTHESIS) NA IMANI (BELIEF) NI VITU VIWILI TOFAUTI LAKINI WEWE UNASRMA HYPOTHESIS NDIYO BELIEF, KITU AMBACHO SIYO KWELI.
DHANA HUWA INAZALIWA KUTOKA KWRNYE SUSPICION KWAMBA POSSIBLY A INAWEZA IKAWA Z, WAKATI IMANI NI FACTS ZIINAZOJULIKANA TAYARI AMBAZO SIYO LAZIMA ZIWE NA UWEZO WA KUWA PROVED KWA KUTUMIA INSTRUMENTS ZA KISAYANSI, NA XIKO INDEPENDENT OF THE KNOWLEDGE OF THE KNOWER. KWAMBA KWA MFANO, WEWE KUWA NA IMANI KUWA MUNGU YUPO, HAKUMFANYI AKAWA YUPO KAMA HAYUPO, NA VILE VILE WEWE KUWA NA IMANI KUWA MUNGU HAYUPO, HAKUMFANYI AKAWA HAYUPO KAMA YUPO
AKILI ni uwezo wa KIUMBE kupokea taarifa,kisha kuichakata na kutoa maamuziFikiria hali inayoitwa 'akili'. Tunaposema akili au tunapoongea juu ya neno 'akili' tunarejelea nini, hali gani?
Akili ya binadamu kwa mfano, akili ya wanyama, ya mimea; au akili ya mitambo, ni hali gani? Ni nini? Je! Ni ufahamu? Ni utambuzi? Ni uelewa? Ni kujua?
Imani ni hali ya kiakili inayopita ufahamu na utambuzi wa kawaida wa akili ya binadamu. Kimsingi ni uelewa wa hali ya juu au kina wa mambo na elimu ya vitu, jinsi mambo yalivyo.
Kuhusu dini. Cha kwanza ni uelewa, 'kujua' ukweli kuhusu dini. Halafu hufuata kupenda, 'upendo'. Watu ambao hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu wanaweza kudanganywa na hivyo kupotoshwa au kupotoka kuhusu ukweli kuhusu dini.
Huwezi kutenganisha imani na kujua au na kuelewa.IMANI ni kuchagua kukubali kwamba kitu fulani kipo bila ya kuwa na UTHIBITISHO wowote
DINI ni IMANI, watu wameamua kuamini kwamba Mungu yupo na ametupa muongozo wa kufuata tunapoishi
fallacyTakataka
Kitu kikijulikana kinakua ni FACT………..Fact huwa ni MOJA TU haina LONGOLONGOHuwezi kutenganisha imani na kujua au na kuelewa.
Mtu ambaye hajui, ambaye haelewi hawezi kusema ana imani na jambo hilo.
Mfano wako wa kikombe cha babu wa Loliondo na maji ya Mwamposa ni ushahidi kuwa watu hao (watanzania wengi) hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu.Kitu kikijulikana kinakua ni FACT………..Fact huwa ni MOJA TU haina LONGOLONGO
Kikombe cha Babu wa Loliondo au maji ya upako ya Mwamposa ni IMANI huwezi ku prove inaponya……. Lakini Dawa mseto ya Malaria ni FACT inatibu Malaria, you can prove it
IMANI sio KUJUA au KUELEWA jambo…….. ni kukubali kuwa jambo lipo bila UTHIBITISHO
Kuna IMANI za MUNGU tofauti tofauti zaidi ya 1000 duniani kote, na kila imani inaamini INAMJUA na KUMUELEWA Mungu wao ndio Mungu wa kweli……,, hii haimaanishi ni KWELI wanamjua na kumuelewa Mungu wao ila wamekubali yupo tu
Ukiachana na matangopori tuliyolishwa kuwa ukifanya hivi unakufuru ama ukifanya vile utapata dhambi na kufikiri kwa fikra huru utagundua juu ya dhima halisi ya hizi dini.Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
Mkuu hili andiko lako nimeliongeza kule juu ili waliokaza shingo kwenye kuyachambua haya mambo wakiamini tunakufuruUkiachana na matangopori tuliyolishwa kuwa ukifanya hivi unakufuru ama ukifanya vile utapata dhambi na kufikiri kwa fikra huru utagundua juu ya dhima halisi ya hizi dini.
1. Dini ni Social institutions ambazo zilibuniwa mahususi ili kumdhibiti binadamu kwa kumlisha itikadi na kumjengea hofu ili aweze kukaa kwa amani na jamii inayomzunguka. Kwa maana hiyo dini inafanya jukumu kama taasisi zingine zilizo kwenye jamii mfano; Mahakama, Shule, vyuo, Magereza na Polisi.
2. Imani ni zao la utamaduni, mafundisho ama experience ya maisha juu ya jambo, mtu, kitu ama tabia. Kwahiyo imani imejengwa katika msingi huo kwa maana imani inatokana na dhana ya kuamini.
3. Kwa muktadha wa sasa Dini inatumika kama chombo cha kubebea imani. Ni kama vile makahama ambayo ni social institution inavyotumika kutafsiri sheria ambayo ni mafundisho jambo sahihi na lisilo sahihi kwa mujibu wa taratibu za jamii husika. Kwahiyo mahakama na sheria ni vitu viwili tofauti ila vinafanya kazi kwa pamoja.
HITIMISHO:
Dini na imani ni vitu viwili tofauti ila vinavyofanya kazi kwa pamoja. Dini ni chombo kinachotumika kubeba imani.
Vyote kwa pamoja vilibuniwa na watu wenye akili nyingi sana kwa lengo la kumdhibiti Binadamu kifikra, kimatendo na kutengeneza ustaarabu kwenye jamii. Hutumia njia njia ya mafundisho, kujenga hofu na uwoga, pamoja na ahadi za adhabu na tuzo kwa wanaotenda kwa mujibu wa mafundisho na wale wanaoenda kinyume. Dhana kama vile dhambi, kukufuru ni nyezo kuu za kudhibiti uwezo wa Binadamu kuwa na hofu ya kuhoji mamlaka zilizoasisi imani hizi na mapungufu ambayo kwasasa yanadhihirika katika imani hizi