Hii ndio CHANGAMOTO kubwa sana ya watu wa IMANI kwa kila mmoja kuona IMANI ya mwenzake sio SAHIHI ila anachoa jua na kuAMINI yeye.Mfano wako wa kikombe cha babu wa Loliondo na maji ya Mwamposa ni ushahidi kuwa watu hao (watanzania wengi) hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu.
Jambo hilo la kikombe cha babu au maji ya Mwamposa sio mambo ya imani wala hayahusiani na imani kwa sababu hayana sifa hizo.
Imani sio kukubali bila kuwa na uelewa au kujua jambo unalolikubali. Kwa sababu kukubali kitu ambacho hukijui(hujui) ni kukubali kufanya makosa isipokuwa kama jambo hilo ni la kweli.
Kuhusu imani kutoka kwa Mungu (faith). Hii inahusu na inaeleza 'kweli za kiakili'. Jinsi mambo yalivyo.
Kutothibitika kisayansi kwa 'kweli za kiakili' hakuelezwi kuwa jambo hilo halipo. Kunaweza kuwa kwa sababu za maarifa au huruki ambazo zinapita uelewa wetu wa sasa.
Mkuu sio sahihi kubishana. Yafaa kujiuliza na kufuatilia (kuchunguza): hapa tulipo ndio mwisho wa kila kitu?Mkuu The likes of Kikombe na maji ya upako havijaanza TZ vipi Dunia nzima toka enzi na enzi na vitaendelea kuwepo…… sio issue ya waTz kukosa uelewa…….. ni issue ya kwamba IMANI haitaki LOGIC ndio maana kila mmoja anamuona mwenzake hana uelewa
Inawezekana vipi kusema kitu fulani kipo wakati HAKITHIBITIKI kwa namna yoyote ile?
Wewe ulizijuaje hizo kweli za akili halafu wengine washindwe kuzijua, ulitumia metrics/criteria zipi kujua jambo ambalo “limepita uelewa wetu”?………. Kama UMELIJUA basi halijapita uelewa wetu
Wengi watakukosoa lakini umeandika jambo zuri na muhimu.Mfano wako wa kikombe cha babu wa Loliondo na maji ya Mwamposa ni ushahidi kuwa watu hao (watanzania wengi) hawana uelewa wa kina wa mambo na elimu ya vitu.
Jambo hilo la kikombe cha babu au maji ya Mwamposa sio mambo ya imani wala hayahusiani na imani kwa sababu hayana sifa hizo.
Imani sio kukubali bila kuwa na uelewa au kujua jambo unalolikubali. Kwa sababu kukubali kitu ambacho hukijui(hujui) ni kukubali kufanya makosa isipokuwa kama jambo hilo ni la kweli.
Kuhusu imani kutoka kwa Mungu (faith). Hii inahusu na inaeleza 'kweli za kiakili'. Jinsi mambo yalivyo.
Kutothibitika kisayansi kwa 'kweli za kiakili' hakuelezwi kuwa jambo hilo halipo. Kunaweza kuwa kwa sababu za maarifa au huruki ambazo zinapita uelewa wetu wa sasa.
AKILI ni uwezo wa kiumbe kupokea taarifa, kisha kuchakata na kutoa maamuzi……….. mchakato huu ndio AKILIMkuu sio sahihi kubishana. Yafaa kujiuliza na kufuatilia (kuchunguza): hapa tulipo ndio mwisho wa kila kitu?
Akili ya binadamu ni halisi?
Imani ni nini? Sayansi ni nini?
Imani inatoka wapi na sayansi inatoka wapi? Uthibitisho maana yake ni nini? Tunajuaje? Na tunajuaje kuwa tunajua?
Kwa nini tunajua?
Na mwisho kabisa vitu vyote vilivyopo maana yake ni nini? Nini maana ya mambo haya?
Pamoja na kasoro zinazoweza kuwepo za uelewa, za utamaduni lakini hiyo haimanishi kuwa kuna 'Kweli' mbili au nyingi. Ukweli ni mmoja tu na unawahusu watu wote popote. Kuuwa, wizi, uzinzi, uharibifu wa mazingira, kupenda miungu, uongo, kutoheshimu wakubwa, kushindwa kuwajibika kufanya hivyo kwa sababu zozote zile ni kosa dhidi ya akili.
Kwa sababu hiyo ni wajibu wa kila mtu katika umri wake wa kuanza kutumia akili kutafuta na kujua ukweli hasa ukweli kuhusu dini.
Mkuu IMANI au DINI zina UKWELI upi ambao watu wanashindwa kuukabili?Wengi watakukosoa lakini umeandika jambo zuri na muhimu.
Shida ya wengi ni kuukabili ukweli.
1.Mkuu IMANI au DINI zina UKWELI upi ambao watu wanashindwa kuukabili?
Kwa ufahamu wangu IMANI zipo nyingi sana…..,,, Lakini IMANI ya Maker aka Mungu inatekelezeka zaidi kupitia DINI1.
Imani ni njia sahihi ya mtu kuwa karibu na Maker wake. Lakini ni Hiyari kuifuata
2.
Dini ni ujanja, ghiliba na hadaa na inalazimishwa kufungamana na Imani. Lengo kuu ni kupindisha ukweli, kumiliki hiyari na kuhodhi mamlaka, uweza na Omnipotence ya Maker
Watu wote wa nyakati zote tuko chini ya sheria moja (universal laws). Kile ambacho ni kosa dhidi ya akili kinawahusu watu wote wa nyakati zote.Akili inatoa maamuzi kutokana na ilivyolishwa kulingana na Mila, Tamaduni,Imani na nyakati…….
Native Chinese, Afaghanistan, Jews, Masai, Adzabe……. Hizi jamii zinatafsiri tofauti kabisa kuhusu uzinzi, mazingira, Miungu nk
Wewe unaona hayo mambo ni kosa dhidi ya akili sababu Dunia hivi sasa imestaarabika na kuset standard(human rights) inayofanya uone ni kosa la kiakili…….. soma historia ya dunia uone Dunia ilikopitia mkuu,
Au unadhani miaka 5000 nyuma mitazamo iko sawa na sasa?
Maana hii ya akili inamweka mtu kundi moja na wanyama wengine which is somehow correct.AKILI ni uwezo wa kiumbe kupokea taarifa, kisha kuchakata na kutoa maamuzi……….. mchakato huu ndio AKILI
Binadamu ni sawa na viumbe vingine kwa msingi huu, wote wanatoka kwa chanzo kimoja. Lakini hadhi yao ni tofauti.Binadamu hana tofauti yoyote na panzi au samaki au kunguru au kiumbe kingine chochote kile linapokuja swala la MAISHA
Atazaliwa,atapambana kuishi, atazaliana kisha atakufa……… HAKUNA maana zaidi ya hiyo.
Wakati unapambana kuishi unaweza kuamua kutafsiri vyovyote upendavyo kudhani hilo ndio kusudi lako la maisha
Viumbe vyote Duniani vinaishi kulingana na Sayansi
Sayansi haina maajabu yoyote…….. ni logics tu ambayo mtu yeyote akijua anafanya na tokeo linakua moja tu
Imani na hapa namaanisha imani kutoka kwa Mungu ni uelewa wa kina au wa hali ya juu wa mambo na elimu ya vitu (kujua). Kwa lugha rahisi ni jinsi mambo yalivyo, ukweli.IMANI/dini na mambo ambayo binadamu ameyaibua pale anaposhindwa kujua baadhi ya mambo.
Kinacho tushughulisha sana binadamu dhidi ya viumbe wengine ni kwamba tuna intelligence kubwa sana kuliko viumbe wengine na ndio maana tunahangaika kutafuta maana ya kila kitu jambo ambalo linatufanya tunazidi kuvumbua mambo mapya kisayansi(sio IMANI)kila leo kusaidia kurahisisha mapambano ya maisha
Hii sentensi inadhihirisha namna upuuzi unaoitwa DINI ulivyofanikiwa kuua independent thinking capability ya wengi kwenye jamii zetu.Kwa ufahamu wangu IMANI zipo nyingi sana…..,,, Lakini IMANI ya Maker aka Mungu inatekelezeka zaidi kupitia DINI
Mimi siamini katika Mungu, uchawi, shetani nk nk…….. Mimi nasimama na Sayansi(logic)Hii sentensi inadhihirisha namna upuuzi unaoitwa DINI ulivyofanikiwa kuua independent thinking capability ya wengi kwenye jamii zetu.
Endelea kushika dini ambao imekuja baada ya IMANI
Mkuu Akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine…… zinatofautiana uwezo tuBinadamu ni sawa na viumbe vingine kwa msingi huu, wote wanatoka kwa chanzo kimoja. Lakini hadhi yao ni tofauti.
Panzi ana akili ya utambuzi. Tofauti na akili ya binadamu panzi hawezi kufikiri na kufanya uchunguzi na kujua na kujua kuleta au kuunda vitu vingine vipya kwa kutumia vitu vya asili vilivyopo, uvumbuzi na ugunduzi.
Jinsi hii ya akili ya binadamu inaeleza zaidi ya uzoefu wa kawaida. Kile ambacho maarifa ya binadamu yametupatia na yanatupatia na kutusaidia kuelewa kwa undani kuhusu ulimwengu ni hali ambayo haiwezi kuwa tu mchezo wa vitu usio kuwa na lengo.
Kwa sababu hata katika shughuli za kila siku za mtu hakuna wazo wala tendo ambalo linafanyika bila kuwa na sababu au lengo.
Wewe ulijuaje family tree yenu?Mimi siamini katika Mungu, uchawi, shetani nk nk…….. Mimi nasimama na Sayansi(logic)
Wewe hizo taarifa za DINI imekuja baada ya IMANI umezitoa wapi mkuu?……….. Hivi kwanini watu wa IMANI mnapenda kuforce unacho AMINI wewe ndio SAHIHI?
Nimetoa mfano, aliye mtengeneza Allah ndio aliutengeneza na Uislam
Kuukataa Uislam maana yake ni kumkataa Allah………. Wewe unatoa wapi uhalali wa kumkataa Mungu wa wenzako kupitia DINI na uka muhalalisha Mungu wako uliyemtengeneza wewe ambaye hataki DINI?
IMANI yoyote ile ikiwemo Dini, Mungu ni vitu ambavyo havitaki matumizi sahihi ya AKILI na ndio vinaongoza kuua independent thinking capacity
Acha mimi, hata babu yangu hajui vizazi vitano tu nyuma yake, anamjua babu yake tu, baba mzaa babu yake anamsikia sikia tu kwambali, wanyuma yake hanataarifa zake kabisaaaWewe ulijuaje family tree yenu?
Huwezi kusema akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine na hapo hapo unakiri kuwa binadamu ana uwezo wa juu sana wa akili.Mkuu Akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine…… zinatofautiana uwezo tu
Binadamu ana uwezo wa juu sana kiakili
Huu ni uelewa wako. Na hii ndio inafanya tofauti kati ya wanyama (utambuzi) na mnyama mwenye busara (akili).Hakuna tofauti yoyote kati ya anaye anaye amini katika imani na asiye amini ila wote wana lengo mmoja wamejikuta wamezaliwa, watapambana kuendelea kua hai, watazaliana kisha watakufa………. IMANI haitawaongezea chochote wala haita punguza chochote labda uwe kiongozi wa kiimani na utumie sadaka kama means yako ya kipato( mapambano ya kuishi)
wewe ukishaona kuna mambo mengi yapo tu hata binadam hajui yalifanyikaje jua IPO Nguvu yenye mamlaka zaidi ya chochote. We unaona jua lina toka Mashariki kwenda magharibi na hakuna wa kubadilisha hilo;Imani haina tofauti na itikadi. Imani inakupa mwelekeo wa kusimamia masuala yanayohusu utawala usioonekana kwamba ndiyo unaotawala fikra na hisia kuhusu uwepo, uumbaji na yanayodhanika kujiri baada ya nafsi na roho kuachana na mwili. (Hii ni tafsiri yangu)
Dini, ni utaratibu uliobuniwa na unatumika kudhibiti aina ya imani ambayo mtu anapaswa kufuata. Dini inasajiliwa lakini Imani haisajiliki.
Basi nimeona wazimu sana kuwa mwanadamu amelazimisha Imani na Dini vifungamane na kwenda pamoja ilihali kimoja ni bangi kingine ni kitakatifu.
Haya, wanazuoni akina Mzito Kabwela na wengineo, mnaweza kunielimisha beyond hayo madhanifu yangu kwenye Imani na Dini?
UPDATE
Binafsi naheshimu sana mtu anayetambua kua “ANA AMINI KUNA MUNGU”Sisi tuna amini kuwa, hiyo Nguvu ni Mungu mmoja tu mwenye mamlaka yote, ambaye hana mshirika, haja zaa wala hajazaliwa na hafanani na kitu chochote.