Naomba mnielimishe umuhimu wa Imani na Dini

Huwezi kusema akili ya binadamu ni kama akili za viumbe wengine na hapo hapo unakiri kuwa binadamu ana uwezo wa juu sana wa akili.

Yaani kwa lugha rahisi maelezo yako yanakinzana.
Hata binadamu tu tunatofautiana uwezo wa kiakili sembuse itakua viumbe vingine mkuu?

Akili za viumbe vyote akiwemo binadamu ni kupambana na mazingira ili kuishi as long as possible ili kuzaliana.

Binadamu hana umaalumu wowote dhidi ya viumbe wengine…….. anaweza akatoweka na Dunia ikaendelea fresh tu( tena in fact the World is better palace kwa mazingira na viumbe wengine without us).

Tofauti na watu wa IMANI mnao AMINI tumeumbwa MAALUMU kwenye Ulimwengu na tuna wajibu wa kumtafuta Muumba au kutafuta “kweli za akili” au sijui kutafuta lengo la maisha wakati maisha ni mafupi sana na ni mapambano ku survive na unakufa wakati wowote either wakati unazaliwa, ukiwa mdogo au mtu mzima the same kwa viumbe wengine
 
Huu ni uelewa wako. Na hii ndio inafanya tofauti kati ya wanyama (utambuzi) na mnyama mwenye busara (akili).
Mkuu hiyo ni FACT na sio uelewa wangu……… unless upinge kwa hoja.

Sina shaka tunakubaliana Lengo baada ya kujikuta umezaliwa ni kupambana uendelee kuishi as long as possible, kisha fursa utazaliana ili existence ya binadamu iendelee kuwepo Duniani utakapo kufa

Sasa nje ya LENGO hilo ambalo analo Panzi, Samaki, Kunguru na viumbe wengine wote……… ni nini IMANI inafanya haswa kwenye MAISHA ya Binadamu.
Tofauti ya Baadhi ya Wachina wasio AMINI na Wakristo au Waislam au Wewe wenye IMANI ni nini KIMAISHA?
 
Hata binadamu tu tunatofautiana uwezo wa kiakili sembuse itakua viumbe vingine mkuu?

Akili za viumbe vyote akiwemo binadamu ni kupambana na mazingira ili kuishi as long as possible ili kuzaliana.
Kutofautiana huko ndio kunafanya binadamu awe mnyama na binadamu awe mtu mwenye busara(intellect).
 
Hata wewe umeelewa ulichoandika?

Soma heading na passage uelewe. Hayo uloyoyaandika hayahusiani na lengo la mada.
 
Unajua unatamani kujenga hoja lakini unashindwa kuelewa unalosimamia.

Haujaweka precedence yeyote inayotupa uthibitisho kuwa IMANI ithibati yake ni dini.

Dini ni nini
Imani ni nini

Tafakari
 
Unajua unatamani kujenga hoja lakini unashindwa kuelewa unalosimamia.

Haujaweka precedence yeyote inayotupa uthibitisho kuwa IMANI ithibati yake ni dini.

Dini ni nini
Imani ni nini

Tafakari
Kwa lugha rahisi kabisa ipo hivi

IMANI ni kukubali jambo ambalo Halithibitiki

DINI ni utaratibu na muongozo wa utekelezaji wa IMANI fulani………..mara nyingi ni IMANI ya MUNGU

DINI haiwezi kusimama peke yake bila IMANI…….. DINI zote msingi wake ni IMANI

IMANI zipo nyingi sana, Ila IMANI ya MIUNGU inatekelezeka zaidi kupitia DINI.
85% ya watu Duniani wana AMINI Mungu kupitia DINI, na Religiously Unaffiliated ni chini ya 7% ya watu wote Duniani

Watu wengi ambao ni Religiously unaffiliated ni watu ambao mwanzo waliamini Mungu kupitia DINI, lakini kwakuwa DINI zinaongozwa na Binadamu wenye Madhaifu mengi wakaachana na kumuhushanisha Mungu na DINI na wakabaki wana IMANI ya Mungu kwa namna anayoina inafaa yeye(jambo ambalo ni gumu kidogo)

Precedence yangu kuhusu ithibati ya IMANI ya Mungu ni DINI ni hii

1, ASILI YA BINADAMU
Binadamu ni social animals wanaoishi kwa pamoja na kufanya mambo yao yote kwa uumoja na utaratibu maalumu(sheria, kanuni, Mila, Tamaduni nk)……… kwahiyo hata NADHARIA ya Mungu ilipoibuka ni rahisi zaidi wao kuwa na utaratibu na miongozo ya kumuadhimisha Mungu wao kwa pamoja ambayo ndio DINI yenyewe……… Ni ngumu kudhani labda Wamasai kila mmoja alianza kuabudu Mungu wake lakini ni rahisi zaidi kudhani kwamba IMANI ilipo ibuka viongozi walitoa muongozo wa namna ya kumuadhimisha Mungu wao ambao ndio DINI yenyewe.

MITUME na MANABII
Ukiachana na DINI za kale, DINI zote zilizoletwa na watu wanaodai wametumwa na Mungu ndio hao hao waliileta IMANI hiyo kupitia DINI.
Mfano Mudi na Fundi selemara wao walidai wametumwa na Mungu kuleta Miongozo ambayo ndio DINI zenyewe…………. Hapo inakua ngumu kutenganisha IMANI ya Mungu na DINI

ZAMA HIZI
Kwa karne yetu hii tunaijua IMANI ya Mungu kupitia DINI za wazazi/walezi/jamii zetu……….. HAKUNA anaye anza na IMANI ya Mungu tu bila kupitia DINI.

Ni ngumu kidogo kuwa na IMANI ya Mungu tu bila DINI(miongozo) kwasababu Dini(miongozo) ndio hutoa misingi ya kusimama na IMANI ya Mungu

Sio rahisi kwa “makosa ya kiakili” kumpa kila mmoja muongozo wa IMANI ya Mungu inataka nini kwasababu tupo tofauti sana, kuna watu wana mawazo na fikra za ajabu huwezi kuamini, na wao akili zao zina watuma wako sahihi kabisa bila tone la mashaka.
 
Hapa umemaliza kila kitu mkuu. Hii ni miradi ya watu kuvuna sadaka za kondoo wao (cf Mwamposa) huku kondoo wakidhibitiwa wasihoji kitu chochote. Kuna watu wanaijua biblia au korani barabara lakini ukiwachunguza vizuri utagundua hawana imani. Wanaichukulia dini kama kazi zingine zinazowaingizia kipato.
 
Siwabezi washika dini. Lakini hebu tuangalie huo uraibu wa kidini husababishwa na nini?
Uraibu wa kidini hutokana na imani iliyopitiliza inayovuka akili ya kawaida ya mwanadamu. Yaani mtu unakuwa kama umeshikiwa akili.
 
Your browser is not able to display this video.
 
nimeyajibu maswali yako yote hapa karibu.


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…