Mbona hata wewe inaonesha ni mzoefu na mwerevu kabisa.
Member hawezi kufuta uzi bali anaweza kufuta maandishi ya uzi wake (contents), moderators pekee ndio wanaweza kuufuta uzi wote na comments zake.
Hakuna function ya kublock bali unaweza ukamuweka member(s) kwenye ignore list, kwamba hutakuwa unaona vitu anavyoandika abadani...
Hii sijawahi ichunguza, ila naamini anayeanzisha uzi ana uwezo wa kufanya hivyo.
Katika kuandika kwangu nyuzi sijawahi kuhangaika kuweka madoido kama heading iwe ya bold, italics au iwe na emoji n.k
Duniani kitu pekee cha siri ni kile kilichopo moyoni mwako...(Nadhani kwa lugha hii utakuwa umenielewa)