naomba mnisaidie kujua tabia za wanaume wa kigoma(waha)

naomba mnisaidie kujua tabia za wanaume wa kigoma(waha)

Ni watu wa maendeleo sana. Hawataki mwanamke mzembe katika maisha. Uwe na adabu na mpenda dini. Ila wana kau dictator kidogo,
 
Kama unataka kuishi maisha ya mateso milele oana na huyo kijana. Utakuja kuelewa usemi wangu baada ya miaka mingi

Jamani si kweli kwamba wanaume wote waha wana matatizo. Makabila yote ameyaumba Mungu mwenyewe. Mimi nasema mtu akiwa anajuwa kuwa mke /mume mwema mtu hupewa na Bwana basi hatasumbuka sana kuwauliza watu bali atamuuliza Mungu wa Mbinguni. Mimi nakushauri kwanza muulize Mungu kwa kufunga na maombi atakujibu.

ILA MIMI MDOGO WANGU AMEOLEWA NA MHA NA HUYO MWANAUME ALIMBADILISHA DINI KUTOKA DINI YAKE YA KIKRISTO AKAENDA USLAMU. YAANI ALIMSILIMISHA. LA AJABU MDOGO WANGU HANA FURAHA KWENYE NDOA AMEKUWA AKIPIGWA NA KUPATA MAJERAHA MPAKA YA KWENDA KUHUDUMIWA HOSPITALI. YAANI SHIDA ALIYOKUWA NAYO ANAHESABIWA AMETUMIAJE MPAKA CENTI YA MWISHO NA AMEMKUTA ANA MTOTO HUYO MTOTO HAMHESHIMU MDOGO WANGU HATA KUMSALIMU HAMASALIMU NA MUMEWE HAJALI KABISA. MIMI NI DADA MKUBWA WA HUYO MDOGO WANGU HATA SIMU YA KUSALIMIWA WALA KUULIZWA NINA HALI GANI
NI KIBURI NA JEURI NA ALIMWACHISHA KAZI ALIYOMKUTA NAYO KWA WIVU WA KIPUMBAVU NA KISHA ANAHESABU CENTI IMETUMIKAJE ANAPORUDI KAZINI ANATAKA AJUWE KILA KITU.
 
Acheni ujinga wa kusingizia tabia fulani kwa kabila fulani.Tabia ni ya mtu binafsi bila ya kujali alipozaliwa au kabila. Acha mara moja ujinga huu. Mimi ni mngoni lakini nina tabia zangu mwenyewe binafsi.
 
Kwanza wanapenda kuitunza familia kwa chakula
.
Pili hawako wazi kumshirikisha mke mipango ya maendeleo

Tatu wanaalika bila aibu ndugu zao kwa wingi bila aibu hata kama ndoa imefungwa Jana tu,

Nne wanapenda kuzaa mpaka yai la mwisho liishe.

Tano, wanapenda kuvaa nguo mpya wakati WA sikukuu zaidi.

Sita wabishi hamna mfano.

Saba uongo ni kama kunywa chai.

Hayo kidogo mengine baadae

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wanajisikia sana hasa wakienda shule hata kama ni kadgree kamoja tu. Ili ufit naye wewe uwe chini sana, yaani uwe mtu wa 'ewala bwana'!.
 
ahahahah hapa ni nouma sana kama mtu ni boyfriend wako halafu hamjafanya
maamuzi mazuri ni kimeo
 
wewe huna mapenzi ya dhati kwake. labda kuna ulicho mpendea coz si chaguo lako.
Mimi ninacho jua, mapenzi hayachagui rangi, kabila, dini, urefu au ufupi. Kitu Muhimu ni je wampenda na unarizika na mapenzi yake?. (mengine yote tupa kule by Husninyo). mia
 
Last edited by a moderator:
Wababe, wabishi, wanajifanya wanajua kila kitu, wana maneno mengi, waongo sana. Ila kama ana hofu ya Mungu, ameokoka tabia zote nilizozitaja hatakuwa nazo. Wewe je tabia zako zikoje, una hofu ya Mungu? Toa kwanza boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako.
 
nina boyfriend wangu ni muha naomba mnisaidie kunifahamisha tabia za wanaume wa kiha kiundani.

Hehehhe....kimbia aisee lazima ukukule 0713.....kama unapenda kugegedwa 0713 usimwache.
 
nina boyfriend wangu ni muha naomba mnisaidie kunifahamisha tabia za wanaume wa kiha kiundani.

Ni wabishi, wanajifanya wanajua sana, wanapenda imani za kishirikina, Kwa ujumla bado ni primitive sana, wakwe ni wasumbufu sana usipokua makini wanaweza kuitawala nyumba yako.Mimi nimeoa kwao walinisumbua mwanzoni ilinibidi nitumie ubabe wa kikurya kuweka mambo sawa. Ila si wote cha msingi muombe Mungu awe mmoja kati ya wachache.
 
Back
Top Bottom