Naomba mnisaidie kupendekeza jina zuri na 'unique' la mtoto wa kiume wa Kiislam

Malik ni sifa ya Mungu binadam ataitwa AbdulMaliQ
Hata kumuita Malik pia yafaa sababu Malik maana yake ni "Mfalme" na wafalme wanaadamu wapo. Kisichofaa ni kujiita au kumuita mwengine "Mfalme wa Wafalme". Sababu Mfalme wa Wafalme ni Allah tu.
 
Wanabodi salaam! Nimefanikiwa kupata mtoto wa kiume, sasa kwa jinsi nilivyokuwa na furaha na ujio wake natamani nimpe jina zuri na la kipekee. Najua humu ndan kuna wajuvi wengi so karibuni sana
Sikusudii kukuudhi wala kudharau ila...

Muite MUHAMMAD
Narudia tena muite mwanao (mpe jina la) MUHAMMAD

Kama upo serious lakini

Nitarudi!
 
Hongera sana.
Mpe jina kati ya haya;
Gadafi
Sadam
Osama.
 
Asante sana kwa somo zuri shekh wangu
 
Mtume amesisitiza sana katika wanao hakikisha miongoni mwa wa kiume watatu basi hakikisha mmoja anaitwa MUHAMMAD. Hakuishia hapo bali akatoa ruksa hata mtu kuitwa jina la baba yake au ndugu yake wa kuzaliwa (mfano baba MUHAMMAD na mtoto MUHAMMAD au baba na watoto wake zaidi ya mmoja wote kuitwa jina moja))

Watu (waislam) wengi utasikia. Wanakimbilia majina ya waarabu tena bora hata wapate basi muongozo kwa wenye kujua juu ya majina hayo lakini utakuta mtu anajiokotea tu huko ilimradi lijina anampachika mtoto. Nimeshuhudia mtoto anaitwa Rajim sasa kweli unamuita mwanao hivyo!? Mwingine nae ni wa kiume lakini eti nikakuta anaitwa Faraja (yaani ni sawa na Salimu umuite Salama)

Halafu hii mambo ya kusema jina unique sijui ni nani alianzisha hata maana kila mtu utasikia nitafutieni jina ambalo ni la kipekee kabisa kwa mwanangu. Hivi huo upekee unatoka wapi? Labda uunde lugha yako mpya ili kupata jina la kipekee sasa
 
Tatizo lako hauna vibe, [emoji3]
Huwezi kutuelewa wazazi wa dar
 
Imamu malicky?

Sent from my SM-G955F using JamiiForums mobile app
Imam Malik jina lake kamili anaitwa Abdullah-Malik ibn Anas kumuita malik ni mazoea ila ni makosa Malik ni miongoni mwa majina ya mwenyezi Mungu maana yake ni (mmiliki) kwakua yeye ndo mmiliki wa kila kitu ila kwa binadam ni lazima iongezewe Abdul maana ya Abdul ni (mja/kiumbe) kwahiyo AbdulMaliQ maana yake (mja wa mmiliki)
 
Tuendelee

Junaid - maana yake shupavu/soldier

Tareef - maana yake kitu ambacho ni adimu na kizuri)

Sawad - maana yake mwenye utajiri wa afya,huruma,upendo (na hata mali inshaAllah)

Au geukia ya asili
Mpili, Akilimali, mbwiga wa mbwiguke, Nishai mtombangile kitwango , au palamagamba.
 
Majina nje ya kiswahili na kilugha ni utumwa wa kifikra
 
Ukimuita Abubakary tu basi ujue kashakuwa gaidi coz magaidi wengi majina yao yanakuwaga aboubakary.

Ukimuita Naseeb Hawa wanakuwaga na bahati saana maishani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…