begi la pesa
JF-Expert Member
- Apr 11, 2019
- 1,833
- 2,878
Ukiendekeza sana hii mentality mwanamke anatumia watoto kukutawala, Wapende Wanao ila kwa mipaka na mipaka yenyewe ni kwamba kamwe usije kumuonesha huyo mwanamke wako kwamba huwezi kuishi bila watoto wakohuwezi susa watoto wako sababu ya mwanamke hilo halikubaliki
Migogoro ya wazazi ya mara mara kwa mara inaathiri watoto kisaikolojia,kimasomo pia wanakuja kuwa watu wa ajabu hapo baadae.Inaathiri watoto kivipi wanasoma wanakula na wanaishi sehemu nzuri fafanua tafadhali ?
š Elezea kiongozUkishazalishwa, Kuna 0.1% ya kuolewa
Sentensi imekamilika hy mkuuš Elezea kiongoz
Migogoro ya wazazi mbele ya watoto lakini kwa mwanaume halisi ana himaya ambayo mtoto atakuwa vizuri regardless mahusiano yake na mkewe. Kama unahudumia familia na unatumia muda wewe na mwanao haya mambo hautayasikia hata kama mkeo akimjaza sumu mwanao. Tatizo wanaume wengi muda wetu wa ziada tunautumia sehemu za starehre na sio na watotoMigogoro ya wazazi ya mara mara kwa mara inaathiri watoto kisaikolojia,kimasomo pia wanakuja kuwa watu wa ajabu hapo baadae.
Mtoto kupata chakula , kuishi sehemu nzuri ni maamuzi ya wazazi, hata mkitengana wanaweza kupata vyote hivyo kama mtaamua kuweka ubinafsi wenu pembeni.
Bado ina mafundo fundoSentensi imekamilika hy mkuu
Pole šBado ina mafundo fundo
Be a man bro. Una mamlaka na hekima simama kwenye nafasi yakoMambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?
Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
Dah, hatari sanaWANAWAKE mnafanya sana maamuzi Kwa mihemko sn, afu mnawapa wengine misalaba
Nna dada angu nae hivo hivo aliondoka Kwa mumewe (na mimba changa bila mumewe kujua) Kwa ugomvi mkubwa na akamblock mumewe laini zake zote.
Nilipiga Sana KELELE, iki mnachomshauri sista hakifai, Hadi mama zangu wadogo wakataka kunipa laana. Wamemkumbatia TU sista,wanasubiri shemej eti mpk aje awaombe msamaha. (Shemej kauchuna kimya more than 7months)
Miez ya kujifungua ilivokaribia, ndugu nao washaanza kumchoka, anakaa Kwa huyu, kesho anahamia mwingine, Basi sista nahs akayamiss maisha ya ndoa yake na kuamua kurudi Kwa mmewe ili kujifungulia uko.
Mumewe kashangaa kuona mkewe aliondoka flat,anarudi na kitambi. Ile mimba jamaa kaikataa katakata na siku Ile ile akaenda mahakaman kufanya mpango WA talaka Hata mtoto hajazaliwa Bado.
Tunavoongea saivi, dada angu keshajifungua na Yuko divorced na anahangaika na maisha
Duuh mbona hatarii hii, LolMama ndiyo inabidi afikirie uamuzi wake unavyo affect watoto. Kuondoka na watoto na mimi kuwahudumia ni kuchezea hela. Kama hapa hapafai kwa watoto kuishi basi huko anakwenda na watoto panafaa zaidi. Akiona huko nje pagumu arudi hapa kwangu.
Kweli KabisaUbinafsi
Mambo yake amuachie mwenyewe...
Hatunwachiiii tumegomašMambo yake amuachie mwenyewe...
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...Hatunwachiiii tumegomaš
Kweli mkuu?Mwambie asepe mm nina sister angu kila baad ya miak miwili anakuj amebeb mimba sas hv anawatot 5 kila mtot na babake anaker san