Naomba mnishauri kuhusiana na huyu dada yangu mkubwa

Kwani umemuuliza wewe binafsi akakwambia nini kimejiri?? Ushauri wangu, mfuate dada yako, muulize na mwambia asikufiche hata chembe juu ya nini kimejiri baada ya kupata ABC zake ndio uje hapa tushauri kama utashindwa peke yako. Binafsi naogopa kushauri bila kujua shiida nini maana ndoa zinamengi na ni Kati ya watu wawili.
Soma post no 18 nimelijibu hili mkuu
 
Amewekwa chini akaulizwa changamoto zinazomkabili kwa mumewe binafsi nimeona ni za kawaida tu kwa wanandoa.
1.Mume anamgombeza sana tena mbele za watoto na dada wa kazi.
2.mume anaweza akamkasirikia hata mwezi mzima kwa kosa dogo tu.
3.sijui mume mkali sana.
4.mume kamwambia asifanye shughuli yoyote akae nyumbani tu.
5.Recently ndio mume kaanza pia kumpiga.
Kwackifupi me sijaona zito la kukimbia hapo.
Mwambie aombe kikao na mumewe pamoja na watu wazima wa hapo nyumbani kwenu

Huenda wote wamekuwa wakifanyiana makosa, hivyo mkikaa nao katika kuwapatanisha wanaweza kuwekana sawa na kuokoa mahusiano yao

Ungekuwa una urafiki na Dada yako/mmezoeana kiasi cha kuishi kama marafiki nina amini anaweza kukushirikisha mambo mengi ya Siri

Hasira za mumewe/ukali husababishwa na mambo mengi ila kubwa ni mume kunyimwa unyumba
 
Mambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?

Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
Mtafute shemeji yako muulize tatizo nini mbona ndugu yako karudi nyumbani.
Muulize msimamo wake huyo shem wako, kama yuko tayari kusamehe na maisha yaendelee basi. Kama yuko tayari nenda kaongee na dada yako, mchane live ya kwamba maisha ni magumu na anahatarisha mstakabali mwema wa watoto atapata shida.
 
Shem yeye anasema hawezi kuhudumia watoto ambao hawakai nyumbani kwake,kama Mama yao amewachukua that means wana baba yao mwingine.
Hapo busara inapaswa kutumika ila naona shemeji anaendeshwa na mihemko. Watoto wako unapaswa no matter what!
 
Mambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?

Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
Huyo dada yako punguani, miaka 8 anaondokaje kipumbavu namna hiyo? Sheria ni miezi sita tayari mke wa ndoa huyo. Afuate taratibu za kuondoka ila kama ni Malaya suluhu ni ngumu maana ataaibika.
 
Mkuu wewe ni mwananume kama itawezekana utenge Session tatu za mazungumzo na hao wagomvi

1.Kaa na shemeji muongee umdadisi ujue hasa chanzo cha ugomvi wao.
2.Fanya kama hapo juu kwa dada pia ujue kinaga ubaga.
3.Chambua maelezo ya kila mtu kisha toa maamuzi kama mtoto wa kiume ambapo lazima 90% Iwe kuwarudisha pamoja

NB:Hongera kwa kumpenda na kumjali sister😍😍
 
Kuolewa kwa sheria ni miezi 6 ya kukaa pamoja mfululizo.
Hata kibarua au ukiajiriwa probation period ni miezi 3, ikiisha hujaambiwa kitu ajira ya kudumu tayari.
Sasa kuna mtoto wa watu amekaa na jamaa miaka 8 😂 h sio ndoa tuu, hapa wameshaanza hadi kufanana
 
Mambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?

Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
Ongea na wakubwa wa kwenye familia(babu, mjomba, baba mkubwa n.k) wawaweke kikao yeye na mumewe wafikie muafaka
 
Sasa kuna mtoto wa watu amekaa na jamaa miaka 8 😂 h sio ndoa tuu, hapa wameshaanza hadi kufanana
Una Nini lakini 😂
Kufanana sio tatizo, tatizo ni nyanyaso hasa ukiwa golikipa...

Kuomba Kila kitu kwa mume sio rahisi kama unavyodhani...
Kwanini hataki afanye kazi?

Tatizo lilianzia hapo...

Ubabe ndo naona kwa huyo mume
 
Chunguzeni kinachomsibu ndani ya ndoa kuna makubwa. Msije lazimisha mtu mkaambulia kuokota majivu yake shambani
 
Mwambie apambane na hali yake tu.
Maisha haya unakuaje na utitiri wa watoto wote hao?

Kikwetu wala huongei na huyo dada, Ni fimbo Ile ya kuchungia ng'ombe mtindo mmoja akiwa na mazagazaga yake kichwani na watoto wake hadi kwa mumewe then unarudi unapitia kibanda umiza kujipongeza na rafiki zako halafu usiku unapata usingizi moroooooro
Nao wanajua Hilo hivyo huwa hawa test mitambo kindezi hivyo hata siku moja
 
Mambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?

Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
Kutakuwa na sababu mkuu mbili 1. Akikaa kwa mme wake anakosa uhuru wa kugongwa na mchepuko wake.

2. Jamaa atakuwa amemfumania au kajua anagawa nje na kakaa kimya. Hapo dada Yako hawezi endelea kuishi na huyo jamaa maana ana hofu kubwa mno.

Kinsingi hayo ndiyo maisha aliyoyachagua, kuweni tayari kumsaidia kifedha.
 
Back
Top Bottom