Naomba mnishauri kuhusiana na huyu dada yangu mkubwa

Jaribuni kumdadisi kwa kına usikute kuna masaibu mazito ambayo hua anayapitia kwa mume wake huyo.

Yeye sio mjinga wa kiwango cha kuamua kutoka kwenye mji wake kWa namna hiyo kama kweli alikua anaishi vizuri kwa mume wake.
Unawajua wanawake au unawasikia? Hapo kashashikwa masikio na mashoga zake wapumbavu kwa akili yake anaona anamkomoa mwanaume kuhusu watoto,sasa acha ile kwake.
 
WANAWAKE mnafanya sana maamuzi Kwa mihemko sn, afu mnawapa wengine misalaba

Nna dada angu nae hivo hivo aliondoka Kwa mumewe (na mimba changa bila mumewe kujua) Kwa ugomvi mkubwa na akamblock mumewe laini zake zote.

Nilipiga Sana KELELE, iki mnachomshauri sista hakifai, Hadi mama zangu wadogo wakataka kunipa laana. Wamemkumbatia TU sista,wanasubiri shemej eti mpk aje awaombe msamaha. (Shemej kauchuna kimya more than 7months)

Miez ya kujifungua ilivokaribia, ndugu nao washaanza kumchoka, anakaa Kwa huyu, kesho anahamia mwingine, Basi sista nahs akayamiss maisha ya ndoa yake na kuamua kurudi Kwa mmewe ili kujifungulia uko.

Mumewe kashangaa kuona mkewe aliondoka flat,anarudi na kitambi. Ile mimba jamaa kaikataa katakata na siku Ile ile akaenda mahakaman kufanya mpango WA talaka Hata mtoto hajazaliwa Bado.

Tunavoongea saivi, dada angu keshajifungua na Yuko divorced na anahangaika na maisha
 
Kwa uzoefu wangu wa maisha, dadako ana mchepuko unampa kiburi. Anajiona kapendwa na mchepuko na ameondoka kwa mumewe ili awe huru kuchepuka.

Mchepuko utamtelekeza halafu atarudi kuomba radhi kwa mumewe.
 
Hata km, bas afuate taratibu za ndoa, ili huyo mumewe aweze kuwajibika nae, sasa kuondoka holela huoni anakua mzigo kwa ndugu? Watoto wateseke akati baba yao yupo na uwezo wa kuwatunza anao? Waachane wao wazazi, watoto wapate stahiki zao km kawaida.
Taratibu za ndoa vip tena wakati huu kashazaa ,mwanaume kwenye ndoq anahitaji watoto tu .Ana watoto utamwambia tena kuhusu ndoq.
 
Hapo ndugu yangu, huyo Dada yako kapata Kibwana kinamsumbua huo ndio ukweli, sasa hao ndugu waliomshauri pamoja na yeye mwenyewe ndio watahusika, nyie wengine kaeni pembeni, wenzake wakitaka kuondoka kwenye mahusiano ya namna hivyo huwa wanakuwa wamechuana yeye anaondoka kindezi hivyo ngoja jua limuwakie na mvua imnyeshee
 
Sasa we unatarajia kila baya anaweza kukwambia? Je kama jamaa alikua anamla Dada yako jicho la tatu sahivi Dada yako kachoka unategemea atakwambia kuwa huwa anapakwa washeli mafuta? Au wali kuku wa shemeji umekulevya unawaza utakula wapi tena kuku?

We kausha mwambie akae kwenye hiyo nyumba ya urithi ila mahitaji ya ada za watoto wake ajitegemee mwenyewe , unachoweza kumsaidia ni Issue za dharura tu kama maradhi na kadhalika ila ratiba zake za maisha ya kila siku ahakikishe anajihudumia.
 
Ahsante kwa kukumbushia mkuu
 
Kisheria ni hivyo ila mume anaweza kujitetea ,maana dating za kisasa mtu anapigwa mimba hata 3 ila kwa mume anaenda na krudi kwao.

Sio rahisi kumkamata mtu hapo hat kama wameishi miaka 10 , wengine wana ndoa zao za halali wanaficha na dating inaendelea ... Wanawake wao wajitathmini katika maamuzi yao sio kuzaa bila ya mpango.
 
Halafu inakuwaje huyo shemeji yako agome kuwalipia watoto wake ada kisa amegombana na mke wake? Hili pekee linaonyesha huyo jamaa ana matatizo.
Mkuu, hiyo ni hatua muhimu kuhakikisha watoto wanarudi kwake (mume). Ni kama vile No Reform, No election
 
Hata km, bas afuate taratibu za ndoa, ili huyo mumewe aweze kuwajibika nae, sasa kuondoka holela huoni anakua mzigo kwa ndugu? Watoto wateseke akati baba yao yupo na uwezo wa kuwatunza anao? Waachane wao wazazi, watoto wapate stahiki zao km kawaida.
Yaan watoto nalea wakiwa kwangu, ukijifanya unawabeba utawahudumia mwenyewe...

Yaan ulete jeuri yakuondoka nao alafu huwezi kuwahudumia
 
Mbona unachukulia poa sana matatizo ya watu wengine....kama huna uhakika ya kiini ch mgogoro...kama kimyaaa!
 
hawa wake ambao ni mama wanyumbani ambao wamepata bahati ya kuolewa na baba bora si bora baba yani wanaume wanaojali familia zao kwa kuzipa heshima na mahitaji yote hawa wanawake huwa wanatabia yakutafuta ugovi au visababu Ili waonekane wanateswa nakunyanyaswa Yani anaweza kumfunga mizigo kurudi kwao kwa sababu ya ajabu hata mkikaa baraza na wazee mkaanza tatua mgogoro wakisikiliza hoja zake na wazee wakamuona amekosea anaanza kulia na kuona apendwi mfano anaweza kusema ningeondoka kwa sababu baba loveness anakunywa sana pombe

Wazee wanamuuliza akija amelewa anakupiga jibu hapana
Wazee wanamuuliza ada za watoto mahitaji atoi jibu anatoa
Wazee wanamuuliza mambo ya ndoa yani tendo atimizi jibu anatimiza
Wazee wanamuuliza nyumba mnaoishi ile ya kisasa mmpanga jibu hapana nyumba tumejenga na lile gari ni letu tumenunua

Wazee wanamuuliza shida nini sasa mpaka umeondoka jibu watu wanasema tu mumewangu mlevi na anisikilizi kwa sababu miye ni mama wa nyumbani sina kazi ndio maana ananidharau
 
Mindset za wazee wa siku za leo. Mnaomgoza kuvunja ndoanza watoto wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…