Naomba mnishauri kuhusiana na huyu dada yangu mkubwa

Yaan watoto nalea wakiwa kwangu, ukijifanya unawabeba utawahudumia mwenyewe...

Yaan ulete jeuri yakuondoka nao alafu huwezi kuwahudumia
Mzee wa Hall V em waza kivingine bas, je km watoto ni wadogo? Au bado wanahitaji ulinzi na ulezi wa mama?

Maisha hayako hivyo bhana
 
Taratibu za ndoa vip tena wakati huu kashazaa ,mwanaume kwenye ndoq anahitaji watoto tu .Ana watoto utamwambia tena kuhusu ndoq.
Ko watu wanaoa ili wapate watoto? Je hawa wasio oa na wana watoto pia ikoje?

Kuwa serious
 
Mwambie dada yako aache utoto arudi kwa mumewe, asitegemee Tena kulishwa ameshakua Mzee 😁 Tena mwambie umeshakua Mzee dada

Umri inazidi kwenda unataka kukaa hapa kwa ajili Gani wewe mtafute shemej yako kisha mwambie aje kumchukua dada yako we muombe msamaha ila arudi kwa mumewe
 
Knawezekana 38 bado umri unaruhusu, bado kijana huyo mkuu.!. Si watu wanapenda mashangazi chief??
 
mambo ya ndoa kama huna hekima ni ngumu sana kushauri,watu wanapitia mambo mazito sana na hakuna mwenye akili timamu akabeba watoto kutoka kwenye nyumba yake bila sababu ya msingi kuna vitu ukute amepitia mpk shetani mwenyewe anaogopa,isiwe tabu kisa unamsaidia ela za matumizi kama uwezo unao kaa nae chini umuulize malengo yake ikiwezekana mwezesheni kwa mtaji maisha mengine yaendelee kuhusu mumewe sishangai maana wako wengi tunaishi nao hata ndani ya nyumba na hamna chochote wanachochangia ila nyuma ya keyboard ni wazuri sana kutoa maneno ya shombo,watoto watatu unataka nani akusaidie kutunza na unajua fika ni watoto wako kama sio utahila me nawaambiaga tu wenye mawazo kama haya fainali uzeeni......
 
Mkuu hizi siyo changamoto za kawaida. Mimi ni mwanaume lakini nakuhakikishia pasi na shaka yoyote kuwa hizi ni changamoto mbaya sana na zinaweza kusababisha hata kifo.
 
Ila maisha haya
Mdogo mtu anawaza gharama anazoenda kutumia kumtunza dada yake na watoto wake kuliko yanayomkuta dada yake kwenye ndoa

Ninavyojua hakuna mwanamke anayeamua kuondoka kwenye ndoa yake ya miaka nane bila sababu za msingi
Nampa pole dada yako kwa kuwa na ndugu kama wewe
 
Kuna jambo wote wanalificha

Dada ako anaogopa Kufa baada ya kushikwa kwa usaliti kaamua kukimbia

Au kuna watoto alimbambikizia mume wake na ameanza kuonyesha wasiwas

Ameahidiwa atapewa ajira na sponsor wake
Hilo unasema kwa kubuni tu hauna uhakika
 
hakuna mwenye akili timamu akabeba watoto kutoka kwenye nyumba yake bila sababu ya msingi kuna vitu ukute amepitia mpk shetani mwenyewe
Hata mimi zamani nilikua nina mtazamo huu, ila yaliponikuta ndio nikajua kumbe ndivyo sivyo, sivyo ndivyo!.
Vingine huwa wanafanya makusud ili kuipa uzito sababu za kijinga zilizowafanya kuchukua uamuz waliochukua.

Mwanamke kabisa apitie magumu na akae kimya,wee!! Labda sio wanawake hawa leo.
 
medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Duuh,dada kavumilia mengi....
 
Wee kuna mijanamke mijinga ujue
 
Jaribuni kumdadisi kwa kına usikute kuna masaibu mazito ambayo hua anayapitia kwa mume wake huyo.

Yeye sio mjinga wa kiwango cha kuamua kutoka kwenye mji wake kWa namna hiyo kama kweli alikua anaishi vizuri kwa mume wake.
Kabisa mkuu ndani ya ndoa huwa kuna mengi sana sema nivile tu wengi wetu huwa tunakimbilia kutazama ya nje yanayoonekana.
 
ni kweli,kwenye msafara wa mamba na kenge wamo si wote wanakua wamefanyiwa mabaya saa nyingine wanawake wenyewe tunazingua ila ni jukumu lako kama mume,baba wa familia kuhakikisha familia yako inakaa kwenye mstari hasahasa ukiwa na watoto ila yakikataa yote unabaki kulea watoto wako,huwezi susa watoto wako sababu ya mwanamke hilo halikubaliki
 
Kabisa mkuu ndani ya ndoa huwa kuna mengi sana sema nivile tu wengi wetu huwa tunakimbilia kutazama ya nje yanayoonekana.
Sana,sana...wake kwa waume huvumilia kwa sababu ya watoto na mwishowe huchinjana na kuwaacha hao watoto
 
Pole mkuu, kwakweli Wanawake Mungu pekee ndo anawajua, la Msingi ongea na dada Yako mpe uhalisia wa anachokikimbilia na anachokiacha, baada ya kumpa fact kuhusu uhalisia kuhusu maisha jiridhishe pia upande wa pili wa huyo mmeo, kama Kweli hajamfukuza, kitakachokuwa kimebaki ni kumuacha dada aamue mwenyewe juu ya anachokitaka kwani baada ya ushauri huo naamini hawezi kuwa mzigo kwenu kwani ushauri wako utakuwa kama Kinga ya yeye kuchukua tahadhari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…