Naomba mnishauri kuhusiana na huyu dada yangu mkubwa

Mzee wa Hall V em waza kivingine bas, je km watoto ni wadogo? Au bado wanahitaji ulinzi na ulezi wa mama?

Maisha hayako hivyo bhana
Hahahaha SASA Eng watoto wadogo, wewe mama Yao si unajua kwann usumbue nikufukuze,

Kama unauchungu watoto ni wadogo Acha kusumbua, behave ulee watoto wako wadogo jamani...

Inshort,
Watoto watakuwa tuu, awalee mama Yao au mama wakambo...

Anyway Eng,
Kwann utake kuondoka na watoto?? Na huwezi kuwapa mahitaji
 
Kwa sasa nani ambae amekabidhiwa nyumba na ni nani ambao wanaishi pale. Halafu je wazazi wenu walisema nini kuhusu nyumba waliowaachia ?
 
Nimeshangaa sana, Vipi huyo baba watoto angefariki wasingemsaidia dada yao?

Hapo wanawaza nyumba ya urithi tu, akikaa na watoto wake watakosa kodi or watashindwa kuuza.

Kama imefikia hatua dada yako ameona imetosha huko kwa mumewe ni kumsapoti tu mpaka asimame kwa miguu yake..

Ndugu wa siku hizi sio mchezo.
 
Dah wanawake wanakurupuka sana aisee
 

Ni kama roho mbaya hivi
 
Ko watu wanaoa ili wapate watoto? Je hawa wasio oa na wana watoto pia ikoje?

Kuwa serious
Dada mtu kashatoa yote ya kwenye ndoa, mtamshawishi vip tena jamaa akatoe mahari..Hapa wanawake wanakosea sana.
 
Wewe muache sehemu ya kujistiri na watoto wake si ipo, huwezi jua akili yake ukiguswa kumsaidia toa msaada, kama huna muache na maisha yake...
Mambo ya ndoa wanajuana wanandoa wenyewe
Ya ngoswe muachie ngoswe
Ukimbana akikwambia shemeji yako ameniharibu matako nimechoka utafanyaje?
Wewe waache utashangaa mume mwenyewe anakuja kuchukua familia yake au anarudi kwa mumewe ndoa zinamapito mengi..
Relax fanya yako achana na mambo ya dada yako.
 
Unataka arudi kwa mumewe kwakua unahisi ataishi mazingira magumu na msalaba utawaangukia nyinyi?

Angekua anajimudu usingetaka arudi?

Huyo jamaa ingawa amesema watoto asihusishwe kwa chochote bado sheria inamtaka alee watoto wake. So asidhani hayo maneno ni kinga.

Kwa uzoefu wangu katika ishu ya wanandoa au wazazi usichukue stori hapa na pale kwa kila mmoja kwa wakati wake. Usiwe na prejudice kabisa, futa kila unachotaka kichwani halafu sikiliza hizo scenarios na zitumie kufikia uamuzi
 
Sema huyo jamaa nae kauzu sio poa.
Huyo jamaa yuko sawa 100%, huwezi kufudumia familia ambayo haipo nyumbani kwako. Kwanza ni kuongeza bajeti ya matumizi na kuleta umasikini, pili ni kuhudumia na watu wasiostahili katika familia, tatu mwanamke anapotoka kwako na watoto unaowahudumia vizuri yawezekana anauwezo wa kuwahudumia vizuri zaidi yako hivyo muache afanye hivyo.
 
Jaribuni kumdadisi kwa kına usikute kuna masaibu mazito ambayo hua anayapitia kwa mume wake huyo.

Yeye sio mjinga wa kiwango cha kuamua kutoka kwenye mji wake kWa namna hiyo kama kweli alikua anaishi vizuri kwa mume wake.
Hata apitie masaibu gani,hii dunia kama huna kitu wewe si mtu. Angejipanga aidha kazi au biashara. Hakuna kitu kibaya kama kuwa na kiburi wakati hauna kitu. Hii ina-apply kote wanaume na wanawake. Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kutambua hauna kitu na inabidi ujitafute.
 
Umasikini mbaya sana, wanawake tutafute pesa zetu kuepuka aibu ndogo ndogo kama hizi.
Yaani hapa wote mnamshauri arudi kwenye manyanyaso kisa tu hana pesa ya kulea watoto. So sad!
Mara nyingi inakuwaga mateso ya kujitakia, hapo mwanaume unakuta kajitahidi sana hata kumfungulia vibiashara lakini mwanamke unakuta kabarikiwa kichwa maji na nyota ya kunguni (kila anachogusa kinakufa) au ndio ile sampuli ya wanawake wanaopenda kuishi kama mapambo ndani yaani mume awaze ada za watoto, chakula, kodi na juu ya hapo ukute hadi vikoba vya hiyo mwanamke analipia
 
Umasikini mbaya sana, wanawake tutafute pesa zetu kuepuka aibu ndogo ndogo kama hizi.
Yaani hapa wote mnamshauri arudi kwenye manyanyaso kisa tu hana pesa ya kulea watoto. So sad!
Wewe utakuwa hujawahi kuolewa upo nyumbani kwenu au umekaa ghetto. Kaka yake mwenyewe kama shahidi anasema dada yake aliishi vizuri kwa mume wake na alihudumiwa vizuri, sasa wewe ni nani useme aliteseka? Kama ni kuteseka kaka yake angesema humu
 
Hakuna cha kukimbia as long as yeye na watoto walikuwa wanahudhmiwa.
 
Tabia nyingine za hovyo sana.
 
Kwa ushauri huu ndoa nying sana zimevunjika.
 
Huwa nawashangaa wanawake ambao wakikimbia wanakimbia na watoto ilihali huduma hawajiwezi.
Mbaya zaidi wakikimbia na watoto wanawadanganya watoto kuwa Baba kafa au hamtaki mtoto
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…