Naomba mnishauri kuhusiana na huyu dada yangu mkubwa

Sio kususa watoto, kama mwanaume unajitahidi kuhudumia vizuri familia ghafla mwanamke anaondoka na watoto sasa unahudumiaje familia mbili ikiwa hata walipokuwa nyumbani ulikuwa unapambana jasho, mateso na damu? Hapo ni kuachana nao ili kujipa muda mzuri wa kutibu majeraha uliyoyapitia na kumwagilia moyo kwa asali na maziwa
 
Dadako amewaambia anapigwa halafu unasema hujaona jambo zito! Kwahiyo aendelee kupigwa kwa sababu ninyi ndugu zake hamna uwezo wa kumsaidia yeye na watoto wake?
 
Mzee wa Hall V em waza kivingine bas, je km watoto ni wadogo? Au bado wanahitaji ulinzi na ulezi wa mama?

Maisha hayako hivyo bhana
Mama ndiyo inabidi afikirie uamuzi wake unavyo affect watoto. Kuondoka na watoto na mimi kuwahudumia ni kuchezea hela. Kama hapa hapafai kwa watoto kuishi basi huko anakwenda na watoto panafaa zaidi. Akiona huko nje pagumu arudi hapa kwangu.
 
Dadako amewaambia anapigwa halafu unasema hujaona jambo zito! Kwahiyo aendelee kupigwa kwa sababu ninyi ndugu zake hamna uwezo wa kumsaidia yeye na watoto wake?
Hiyo ni kengele yake ya kuamka aidha ajiafute kwa shule au kufanya biashara. Dunia ya sasa hauwezi kuwa mama wa nyumbani halafu ulete kiburi.
 
Kwa mila na tamaduni zangu mke akigombana na mumewe anatakiwa kwenda kwa wakwe zake na sio kurudi kwao.
 
Wewe utakuwa hujawahi kuolewa upo nyumbani kwenu au umekaa ghetto. Kaka yake mwenyewe kama shahidi anasema dada yake aliishi vizuri kwa mume wake na alihudumiwa vizuri, sasa wewe ni nani useme aliteseka? Kama ni kuteseka kaka yake angesema humu
Kuishi vizuri maana yake ni nini? Kula na kuishi nyumba nzuri? Hakuna mwanamke anaondoka mahali penye amani akaenda kupata shida. Hayupo huyo mwanamke.

Huyo kaka nae umaskini tu umemjaa, alikuwa ananufaika na visenti vya shemeji sasa anaona zinaenda kukata.

By the way nina ndoa ya miaka 18 sasa hivi mume wangu anahitaji mke wa pili, karibu tujumuike kupika na kupakua.
 
Sasa wewe upo kwenye ndoa ndio unashauri mwenzako aachike? Wewe ulipaswa kushauri waendelee kikaa pamoja kwa kuvumiliana. Kuhusu maneno niliyoyakoleza unaonekana ni mtu mwenye umri mkubwa ila akili yake haijakomaa. Soma vitabu na ukae karibu na watu wenye akili na hekima utabadilika na kuwa mwelevu
 
Hayo ni mawazo yako. Lakini haijawekwa wazi nini hasa kimemuondoa kwa mume wake..inawezekana ni sababu inayoeleweka.
Hakuna mwanamke anayetunzwa vuzuri namna hiyo na kuishi kwa amani akaondoka bila sababu, hayupo...labda kama ana matatizo ya akili. Kuna jambo halijawekwa wazi..
 
Mzee uko poa sana. Kwa hizo hoja zake hata mie naona hakuna chochote kizito cha kumkimbiza kwa mumewe. Huyo dada ako ni kiburi tu. Achaneni naye dunia imfunze.
 
Sijashauri aachike maana hata sijui nini kimemuondoa. yeye ndo anajua..na huyu anayejiita kaka yake hajaweka wazi..analaumu tu dada yake kuondoka bila kusema nini hada kimemuondoa.
Mtu asipopata amani anayoihitaji kwenye ndoa yake kama kaamua mwenyewe kuondoka aondoke haina tatizo.
Hata kama ni binti yangu nitamsapoti kama kaamua mwenyewe. Tumeshuhudia wengi wamelazimisha kubaki mwisho wa siku wamekufa kifo kibaya. Kwaajili ya nini sasa? Ndoa?
Bro..kuna mambo ya ajabu sana kwenye hizi ndoa na mengine hayavumiliki, mtu yoyote awe mume au mke akiona mambo yamekuwa hovyo aondoke mara moja. Hukuna atakayekupa tuzo ya kuvumilia upuuzi.

Naamini kabisa huyo dada angekuwa na kipato cha kueleweka usingeona hili bango hapa.
Narudia tena..ni umasikini ndo umesababisha tunaona hili bango na si jambo lingine.
 

Huna cha kufanya
 
Sosthenes Maendeleo kwasababu kama hizo kaka mtu anaona ni sawa dada yake kutendewa hivyo. Yaani kaka mtu ni katili kuliko huyo mume inashashangaza sana.

Ndio maana nikasema ni umasikini maana eti hayo ni mambo ya kawaida sana kwenye ndoa, kwahiyo mke anaolewa ili akafanyiwe hivyo na tunaona kabisa ni sawa.

Labda tujiulize mwanamke anaolewa ili iweje? Na usiseme anaolewa ili kupata heshima maana kwa hiyo listi iliyowekwa hapo sijaona heshima yoyote aliyopewa huyo mwanaume.

Acheni ukatili kwa watoto wa kike, halafu wakiathirika na huo ukatili mnawasema. Sio vizuri hata kidogo kaka yangu, kwani tumewakosea nini hadi muone kwamba tunastahili kufanyiwa hivyo tukiwa kwenye ndoa?
 
hao wa kuishi nao kwa akili hata kama ni dada yako. Ukimuuliza sababu za msingi utakuta hana. Ni ujinga ujinga tu, wanapenda kupeana ushauti wakikutana huko vikoba, na vile wana low IQ hujikuta wana upeo wa kuona mbali.

Na tatizo analo yeye ndo maana mumewe kakausha. unaweza ukakuta hao watoto sio wote wa mumewe.

Wanaume hatuna ufala wa kuacha mbachao kwa msala upitao. hua tunabeba vyote.

Akapige magoti kwa mumewe kabla hajapata mbadala wake. tena mwambie afanye chaaaap..

Over
 
Hizo zilizoorodheshwa ndio tabia za wanaume walio wengi kwa kuwa anakulisha na anasomesha watoto na. Kulipa bill za familia anaona ana haki kukufanyia hayo yote ..maana ni mtumwa wake ...
Lazima mwanamke aonekane ana matatizo na hawawezi kuliona tatizo liko wapi..
 
Sasa mimi najiuliza. Mwanamke anaolewa ili iweje? Tunapaswa kujitafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…