suluhu haitapatikana kwenye mindset ya kimasikini na ya kikandamizi kama hii ya kiafrika.Sasa tujadili ili kupata suluhu ya matatizo yote.. Kiufupi mimi naona binadamu ni wabinafsi ..Siwezi kukueleza maisha yangu ila mimi ni muhanga tena ,nimeshuhudia wazazi wakiwa wabinafsi ,nimeonja maisha ya kipumbavu zaidi ya miaka 10... Kiufupi wazazi na maisha kwa ujamla wote ni uthenge tena utapeli kabisa.
Umeambiwa mumewe ni mfanyakazi wa taasisi nyeti lakini mke mbangaizaji...Wamechokana hao ,ogopa sana binadamu hapo wa muhimu ni wanae ...Baada ya kupata watoto hamna upendo tena ,hii ni kweli kwa 100% kila mtu anajua watoto watakuja kumsaidia baadaye huko mbeleni ila ndoa washachokana.
Anayetunzwa vizuri? Amekuwa mfugo au mbwa wa kisasa?Hakuna mwanamke anayetunzwa vuzuri namna hiyo na kuishi kwa amani akaondoka bila sababu,
Most likely uchumi umebadilika kwa mshkaji ila mwanamke mentality yake ni ile ileHayo ni mawazo yako. Lakini haijawekwa wazi nini hasa kimemuondoa kwa mume wake..inawezekana ni sababu inayoeleweka.
Hakuna mwanamke anayetunzwa vuzuri namna hiyo na kuishi kwa amani akaondoka bila sababu, hayupo...labda kama ana matatizo ya akili. Kuna jambo halijawekwa wazi..
angalizo dogo...suluhu haitapatikana kwenye mindset ya kimasikini na ya kikandamizi kama hii ya kiafrika.
Watu wanalalamika ndoa za siku hizi sio kama za zamani maana zamani watu walikuwa hawajafunguka akili, hawajui haki zao.
Sasa hivi ni tofauti. Mwanamke hataki kunyanyaswa na bahati mbaya sana akili ya baadhi ya wanaume imestuck wanaamini kwamba mke anatakiwa anyanyaswe ili akutii.
Na wanawake wamefunguka zaidi wengine wanataka 50/50.
Ndoa imeingiliwa na mambo mengi na huko tunapoelekea inapoteza umuhimu.
Pole kwa majanga uliyopitia.
Ameanza kuuza nguo baada ya kuondoka kwa mume. Mume hakutaka ajishughulishe na chochote.angalizo dogo...
Mume ana pesa na anafanya taasisi kubwa..
Mke muuza nguo mitandaoni kwa kubangaiza.
Mbona tatizo liko wazi tu?
Jeep wranglerAmewekwa chini akaulizwa changamoto zinazomkabili kwa mumewe binafsi nimeona ni za kawaida tu kwa wanandoa.
1.Mume anamgombeza sana tena mbele za watoto na dada wa kazi.
2.mume anaweza akamkasirikia hata mwezi mzima kwa kosa dogo tu.
3.sijui mume mkali sana.
4.mume kamwambia asifanye shughuli yoyote akae nyumbani tu.
5.Recently ndio mume kaanza pia kumpiga.
Kwackifupi me sijaona zito la kukimbia hapo.
Tabia nyingine za hovyo sana.
Huyu mleta uzi ni kupe, anaona atakosa misaada ya shemeji
Hadi wenye watoto wanatengana ili iweje !!!
Mwambie arudi kwake.
Haya mambo ya ndoa na migogoro yake yana chaneli ama tuseme yana procedures zake.Mambo wakuu?
Nina dada yangu mkubwa ana umri kama 38yrs hivi,sasa huyu dada alikua anaishi na mwanaume wake ila hawakua wamefunga ndoa,wameishi kama miaka 8 kama sikosei.wamebahatika kupata watoto watatu mpaka sasa, mumewe ni muajiriwa kwenye shirika flani kubwa tu hapa nchini,dada yangu yeye hana kazi yoyote ni mtu wa kubangaiza tu na kuuza nguo online kwa kifupi ni mama wa nyumbani tu.
Week mbili zilizopita waligombana na huyo mumewe, dada kwa maelezo yake anasema huyo mumewe alimfukuza nyumbani kwake usiku ule pamoja na watoto wake,ila kwa uchunguzi nilioufanya mumewe hakumfukuza ila ni yeye tu aliamua kukimbilia kwa ndugu yetu mwingine na watoto wake usiku ule.
Kilichonifanya nije kuomba ushauri humu ni hiki,kuna ndugu naona kama wamemshauri dada vibaya sana,kuna nyumba yetu ya urithi tuliachiwa na marehemu wazazi wetu,ndugu wamemshauri dada aondoke mazima kwa mumewe arudi pale nyumbani kwenye nyumba ya urithi akae,kweli dada nae akachukua huo ushauri wa ndugu kaenda kwa mumewe kabeba vitu karudi nyumbani na mzigo wa watoto watatu,yule mumewe kule mpaka leo hajampigia simu yeyote nyumbani kumueleza nini tatizo yuko kimya tu,dada yeye anasema amechoka manyanyaso,sasa nimeshindwa kumuelewa dada kama nilivyosema hana kazi yoyote ni anauza tu vinguo online,ana watoto watatu wawili kati yao wanasoma shule za English medium.huko napo nasikia bwana alimuambia kama ameamua kuondoka nyumbani na watoto wake basi asikae amtafute kwa lolote lile na hao watoto amempa yeye kama zawadi.
Dada hakua na maisha yoyote magumu kwa mume wake kwani shemeji alikua anajitahidi sana kujali familia yake.
Wasiwasi wangu ni kwamba,huenda dada akaanza kuishi maisha ya shida kwa kujitakia mwenyewe na akawa msalaba kwetu sisi,kwanza kitendo cha ndugu hawa kumshauri arudi nyumbani pasipokuangalia mustakabali wake na watoto wake naona ni janga,hapa ni week ya pili tu lkn ameshaanza usumbufu wa vizinga.nawaza ada za hao watoto wa English medium atatoa wapi?
Wakuu huenda mwandiko wangu ni mmbaya but tuvumiliane.
Naomba mnishauri nifanyeje huyu mtu arudi kwa mumewe huko kwani kama nilivyoeleza soon anaenda kuwa msalaba kwetu huyu au kama kuna ushauri mwingine naukaribisha.
Yaani wewe ni bonge la phala, hayo sio matatizo makubwa?Amewekwa chini akaulizwa changamoto zinazomkabili kwa mumewe binafsi nimeona ni za kawaida tu kwa wanandoa.
1.Mume anamgombeza sana tena mbele za watoto na dada wa kazi.
2.mume anaweza akamkasirikia hata mwezi mzima kwa kosa dogo tu.
3.sijui mume mkali sana.
4.mume kamwambia asifanye shughuli yoyote akae nyumbani tu.
5.Recently ndio mume kaanza pia kumpiga.
Kwackifupi me sijaona zito la kukimbia hapo.
What a masterpiece!Haya mambo ya ndoa na migogoro yake yana chaneli ama tuseme yana procedures zake.
Kwanza tuanze na structure ya ndoa yenyewe:
Sheria za ndoa za'71 zinazotumika hivi sasa hazitambui mahusiano ya ndoa isiyo rasmi.
Ndoa zinazotambulika ni za kimila, kimadhehebu na kiserikali.
Kwa muktadha huo, dada yako hana ndoa, hakuna sheria inayomlinda kukaa na mwanaume huyo bila kujali 'wamesaga' miaka mingapi wakiwa pamoja.
Ni kitu gani kiliwazuia kufunga ndoa hata ile ya watu wanne tu ya kiserikali isiyo na gharama za sherehe?
Mikataba ya ndoa hulinda pande zote pindi migogoro kama hii inapojitokeza.
Jambo la pili: unapojitokeza mgogoro wa wanandoa, wala usiumize kichwa kumsikiliza mmoja na kutoa maamuzi ama lawama, weka mazingira ya kuwakutanisha, usikilize pande zote mbili ili upate maamuzi sahihi.
Kwa jambo hili la dada yako, jiulize: huyo shemeji yako angelifariki hao watoto nani angeliwatunza?
Je ukiwakutanisha na kuwasikiliza na kugundua kuwa mahusiano yao hayana afya, utazidi kumshauri ama kumshurutisha dada yako arudiane na mtu wasiyeridhiana?
Je kama dada yako hawezi kurudiana na jamaa, stahiki za kutunza watoto ni za nani na ni hatua gani za kuchukua ili kuhakikisha haki na matunzo ya watoto yanaendelea?
Pata option mbili kichwani mwako: za kushauri kwa hekima warudiane na kuendelea kulea watoto wao wakiwa pamoja na kumaliza migogoro yao.
Ikishindikana bila kujali dada yako ndiye mkorofi, hakikisha unamuelekeza hatua za kuchukua kisheria ili kupata haki za malezi ya watoto, kama wewe hujui, tafuta wanasheria wakushauri hatua sahihi za kufuata na wapi pa kulipeleka jambo hilo.
Pia mwelimishe dada yako kuhusu namna anavyokaa na jamaa bila kufunga ndoa kuwa anapoteza muda na haki zake nyingi sana za msingi.
Hapo kafanywa ni kijakazi wa kumtengenezea jamaa watoto, hana haki kisheria ya mgawanyo wa mali hata kama kashiriki kuleta maendeleo ya familia yao, mshauri wafunge ndoa.
Angalizo: jamaa huyo kuishi na dadako miaka yote hiyo kihawara kajihami namna ya kuruka vihunzi vya kisheria kumkandamiza dadako, hivyo ni wa kuendea kwa akili na kisheria na pia dada yako kuendelea kuishi na jamaa kiharamu hakufai.
Dada yako anapigwa na mumewe unaona hakuna cha kukimbia hapo.Amewekwa chini akaulizwa changamoto zinazomkabili kwa mumewe binafsi nimeona ni za kawaida tu kwa wanandoa.
1.Mume anamgombeza sana tena mbele za watoto na dada wa kazi.
2.mume anaweza akamkasirikia hata mwezi mzima kwa kosa dogo tu.
3.sijui mume mkali sana.
4.mume kamwambia asifanye shughuli yoyote akae nyumbani tu.
5.Recently ndio mume kaanza pia kumpiga.
Kwackifupi me sijaona zito la kukimbia hapo.
Aisee 🤔WANAWAKE mnafanya sana maamuzi Kwa mihemko sn, afu mnawapa wengine misalaba
Nna dada angu nae hivo hivo aliondoka Kwa mumewe (na mimba changa bila mumewe kujua) Kwa ugomvi mkubwa na akamblock mumewe laini zake zote.
Nilipiga Sana KELELE, iki mnachomshauri sista hakifai, Hadi mama zangu wadogo wakataka kunipa laana. Wamemkumbatia TU sista,wanasubiri shemej eti mpk aje awaombe msamaha. (Shemej kauchuna kimya more than 7months)
Miez ya kujifungua ilivokaribia, ndugu nao washaanza kumchoka, anakaa Kwa huyu, kesho anahamia mwingine, Basi sista nahs akayamiss maisha ya ndoa yake na kuamua kurudi Kwa mmewe ili kujifungulia uko.
Mumewe kashangaa kuona mkewe aliondoka flat,anarudi na kitambi. Ile mimba jamaa kaikataa katakata na siku Ile ile akaenda mahakaman kufanya mpango WA talaka Hata mtoto hajazaliwa Bado.
Tunavoongea saivi, dada angu keshajifungua na Yuko divorced na anahangaika na maisha
HakikaHao washachokana ila wanaweza kurudiana ,mtu aishi miaka yote hiyo ,bora huo ugomvi wasiingilie kabisa...
Hakika sio utumwa kabisa.Kufanya kazi za nyumbani sio utumwa. Ni ajabu sana kwa mwanamke kuona vibaya kuwa mtumwa kwa mumewe. Ni sawa na mtoto kujiona mtumwa wa wazazi wake sababu wanampa kazi za kuosha vyombo, kusafisha nyumba kwa deki na kufyeka, kuosha gari, kupika nk, anaona kuwa anawafanyia kazi wazazi wake ilhali wao wamekaa tu hakuna wanachomfanyia.
Bibie sisi tulio oa, ndio tunawajua sana Wanawake na Hila zenu. kwa ufupi mna upungufu wa akili.Ila maisha haya
Mdogo mtu anawaza gharama anazoenda kutumia kumtunza dada yake na watoto wake kuliko yanayomkuta dada yake kwenye ndoa
Ninavyojua hakuna mwanamke anayeamua kuondoka kwenye ndoa yake ya miaka nane bila sababu za msingi
Nampa pole dada yako kwa kuwa na ndugu kama wewe