Naomba mnishauri kuhusiana na huyu dada yangu mkubwa

Nimeshangaa sana, Vipi huyo baba watoto angefariki wasingemsaidia dada yao?
Kufariki ni jambo lingine, shida inaonekana dada yao Hana sababu za msingi za kufanya aondoke nyumbani.

Kama mume angekuwa ni mzinzi, mshirikina au ahudumii familia hapo sawa, hizi ni sababu za msingi miongoni mwa sababu za msingi.
 
Labda kaja kugundua kuwa hao watoto sio wake bali ni wa mkewe.
 
Polee saana kwa changamoto ya dada. Ndoa ni muunganiko wa hiyari wa watu 2. Magumu na mepesi wanayojua ni wanandoa. Na hakuna sheria inayoruhusu mwanandoa kuvumilia vitendo vya kikatili na vinapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote.
Mimi ni mwanamke ukweli ni lazima tuuseme. Katika ndoa nyingi zinazovunjika wanawake tunasababisha.
Tunapotaka kutendewa haki basi na sisi tuwe wa kwanza kutenda haki. Sawa mgogoro umetokea na kunyanyasika sasa kabla ya yeye kuondoka alichukua hatua gani? Alishirikisha ndugu wa mwanaume? Viongozi wa dini? na familia yake wakakaa pamoja kujadili changamoto yao? . Na changamoto kubwa ya familia zetu zinachangia kuvunja ndoa za watoto wetu. Zikishavunjika ndo tunaanza kutupia wengine lawama. Mfano kwa mila zetu sisi binti ukishaolewa ikitokea ukaenda kusalimia nyumbani lazima uulizwe eeeh umekuja kusalimia unakaa siku ngapi na je mume wako umemuaga? Na ikitokea mwanaume anakufanyia ukatili au umetokea mgogoro basi unabeba watoto unaenda kwao na mwanaume kwa familia yake, au ndugu yake yoyote ambaye unajua fika huwa anamsikiliza mume wako.

Kosa la kwanza ni familia yako kumpokea mke wa mtu kabla ya kutafuta suluhu. Mlipobaini changamoto ilibidi muitishe kikao kwa kushirikisha pande zote. Hamuwezi kumuhukumu mtu kwa kusikiliza upande mmoja. Na binadamu tulivyo siku zote huwa kamwe hatuwezi kusema mabaya yetu.
Kikubwa fanyeni kikao kutafuta suluhu mtajua nani mwenye makosa nani hana makosa. Kikubwa kinachotuponza sisi binadamu huwa tunapenda wengine watutreat vizuri tukiamini ni wajibu wao lkn katika ndoa ni juhudi za kila mmoja kujua mwenzangu anapenda nini na kipi hapendi. Lkn pia hakuna aliyekamilika.
 
Wewe utakuwa hujawahi kuolewa upo nyumbani kwenu au umekaa ghetto. Kaka yake mwenyewe kama shahidi anasema dada yake aliishi vizuri kwa mume wake na alihudumiwa vizuri, sasa wewe ni nani useme aliteseka? Kama ni kuteseka kaka yake angesema humu
Kwa asilimia fulani mwanamke kwenye ndoa kusema anateseka unakuta mwanaume kashatambua kwamba anatumika kama ATM, na sampuli hii ambayo haifanyi kazi (siku hizi wanaume wachache sana wanakataza wanawake wao kufanya kazi maana sio kwa usawa huu) ndio kundi kubwa kati ya hawa; kama hujui zinazalishwaje basi lazima utazichukulia poa tu
Unakuta anataka mwanaume amnunulie kuanzia pedi mpaka kumbandikia kucha miguuni, atataka kabati lake la nguo lijae mara 3 ya mumewe na bado alalamike hana nguo, na hapo sahizi ni watoto watatu (hajui mzigo wa majukumu uliopo kwenye mabega ya huyo mwanaume wake)
Kiufupi, huyo mwanaume ndani ya nyumba ana watoto wanne na sio wa tatu; hao watatu wana mtii ila huyu wa nne pasua kichwa
 
Hakuna mwanamke anaondoka mahali penye amani akaenda kupata shida. Hayupo huyo Mwanamke
👆🏿👆🏿👆🏿hii kauli futa mama kuna wanawake waliacha ndoa leo hii ni mabaamedi. Hii ina affect hadi watoto
 
Tatizo ni hulka ya utoto (infantilization)
 
Kabisa ,this is wise
 
watoto ni wako hilo halitobadilika kamwe either wawe kwako au nje ya kwako,huwezi achia dunia ilee watoto wako kwakisingiziocha mama yao kuondoka naohuko ni kukimbia majukumu
 
Kwa miaka 38 mwambie either arudi kwa Mme wake au arudishe watoto kwa Mme wake.

Kwakuwa anatafuta matatizo ambayo yatamuua bure.

Miaka 38 sio umri wa kutanga tanga
 
Mindset za wazee wa siku za leo. Mnaomgoza kuvunja ndoanza watoto wenu.
Unakumbuka yule binti aliyechomwa moto na magunia mawili ya Mkaa?

Huenda mazingira yalimlazimisha kuendelea kumvumilia mpenzi wake, mwisho wa Siku akauawa Kwa kuchomwa moto.

Unakumbuka yule Kijana pale Kimara aliyechomwa moto na Mwanamke wake?

Inapotokea changamoto Kwa wapenzi, vyema wakazisovu mapema Kwa kupatanishwa wenyewe ama na watu wazima wanao waheshimu

Otherwise wanaweza kuishia kuuana tu.
 
Wewe ni linga saana. Hizi unaziita changamoto za kawaida?????

Wewe ndiye umesababisha dada yako anapitia matatizo yote haya....mtu anajichukuliaje mwanamke na kuishi naye miaka 8 na kumzalisha watoto watatu halafu nyie mmekaaa mnamwangalia na kumkenulia meno??

Huyo jamaa mmpe mwezi achague kufunga ndoa la sivyo mpelekeni ustawi wa jamii ahudumie watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…