Ndio elimu hyo ya majini...
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kwa muktadha tu. Kuna siku ustadhi alikuwa anatupa kisa cha Nabii Sulayman alayhi ssalaam. Akatuambia Nabii Sulayman alimuomba Allah subhanahu wataala amuoneshe jinsi alivyowaumba majinni kwa maumbile yao halisi.
Malaika Jibril alayhi ssalaam akashuka kutoka Mbinguni hali ya kuwa Nabii Sulayman alayhi ssalaam akiwa katika sijda ya sala akiyaomba hayo. Ndipo Malaika Jibril alayhi ssalaam akatoa sauti kubwa ya wito ya amri ya kuamrisha majinni wote waje mbele ya Nabii Sulayman alayhi ssalaam kwa maumbile yao halisi. Dunia nzima ulimwengu wa majinni sauti hiyo ilisikika, wakajua sauti ya bwana mkubwa imetoa amri ya kuwataka waje na wakaja huku Malaika wengine wakiwachunga mithili ya mchungaji anavyochunga mifugo yake.
Baada ya hapo ndipo ustadhi akatuelezea jinsi Nabii Sulayman alayhi ssalaam alivyoona hayo maumbile yao halisi, na mfano waaumbile na muonekano ndiyo hayo kwa uchache niliyoelezea. Sulayman ambaye ni Nabii, kwa ghafla aliingiwa na hofu baada ya kuona maumbile ya majinni wengine. Kwani ni yenye kutisha, mithili kama Nabii Mussa alayhi ssalaam alivyoingiwa na hofu pale wachawi walipotupa kamba zao na kugeuka Nyoka wa ajabu ajabu. Lakini Mungu alimuambia Nabii Mussa alayhi ssalaam ya kwamba asihofu, kwani yeye(Mussa) ndiye mshindi. Ndivyo vivyo hivyo kwa Nabii Sulayman, Malaika Jibril alimuambia wala usiwe na hofu, kwani hawa majinni ndiyo watakao kuogopa badala ya wewe kuwaogopa.
Lakini kisa cha Nabii Sulayman alayhi ssalaam kwa uchache kina kwenda hivi;
Nabii Sulayman alayhi ssalaam alipewa "Mulkiya" ambayo hakupewa Nabii yeyote wala mtu wa aina yoyote baada yake. Hii ilitokana na Dua yake yeye mwenyewe aliposema " Ewe Mungu nakuomba unipatie ufalme ambao hakuna atakao kuwa nao baada yangu". Kwa sababu ya hii dua yake, Mungu akampa ufalme wa kudhibiti au wa kutawala kwa kudhibiti yaani hakuna atakayeweza kufurukuta kwako. Katika Qur'an Mungu anasema akampa nguvu zifuatazo;
• Nguvu(ufalme) ya kuudhibiti upepo na kuutumia upepo atakavyo.
• Nguvu ama Ufalme wa kudhibiti Majinni/Mashayatwiin.
• Nguvu ama Ufalme wa kuongea na wanyama, wadudu na ndege.
Nguvu ama Ufalme wa kuwadhibiti Majinni, mashayatwiin wa kijinni ndiyo ambayo watu wengi wa jamii tofauti wanajiuliza. Kuna machimbo ya dhahabu Sulayman alikuwa anachimba kwa zama zake ambayo mpaka sasa yanaleta maswali kwa watu kwamba aliwezaje. Lakini hii nguvu ama Ufalme alipewa na aliyeviumba hivyo wakiwemo hao Majinni. Majinni hii hali ya kudhibitiwa na Nabii Sulayman alayhi ssalaam waliona kwao ni udhalili mkubwa sana. Wakikataa kutii amri adhabu hapo hapo inawashukia na wanakamatwa na wanawekwa gerezani. Gereza lao lipo chini ya bahari.
Baada ya Nabii Sulayman alayhi ssalaam kufa. Majinni wakawa huru ila wakaleta madai kwa watu ya kwamba, wamegundua siri ya Nabii Sulayman alayhi ssalaam. Siri ipi? Ni siri ya kwa njia gani Nabii Sulayman alayhi ssalaam alivyo wa control jinni na wanyama.
Angalizo: majinni wana uwezo wa kujigeuza binadamu na ndiyo njia waliyotumia kujitokeza kwa watu baada ya kufa Nabii Sulayman.
Hawa majinni mashaytwani waliwaambia watu ambao ni Wayahudi kwamba Sulayman alayhi ssalaam anajua "sihri" Nabii Sulayman alikuwa ni mchawi. Kwa hiyo, aliwa control majinni kwa kutumia uchawi. Na hii ndiyo hali waliyokulia nayo baadhi ya Wayahudi kwamba Sulayman alitumia uchawi. Lakini Allah subhanahu wataala alimtetea Nabii wake katika Qur'an akisema;
"Wamaa kafara sulaymana walaa kinna sh'yatwiin kufr, Yuallimuna nnasa s'sihr"
Kwa maana, Sulayman hakukufuru Bali ni majinni hao wa kishaytwani ndiyo waliyokufuru kwa kuwafundisha watu uchawi"
Hapa inaonesha uchawi ni kufuru kwa Mungu. Ndiyo maana Mungu kasema Sulayman hakukufuru. Na hii aya inatumika miongoni mwa makambora kwa majinni.
Nipo ofisini aisee! Yani hapa yenyewe nimeiandika huku nafanya kazi. Baadae.