Naomba Msaada. Nifanyeje ili niweze kupona ini?

Naomba Msaada. Nifanyeje ili niweze kupona ini?

Kuna mama mmoja aliandika symptoms za ugonjwa wa mwanae uliomsumbua kwa muda mrefu sana kwenye AI,AI ikampa majibu, akachukua majibu na kuyapeleka kwa daktari wake, daktari akashangaa na kusema huenda hichi ndo kinachomsumbua mwanao kweli, mtoto akatibiwa akapona. Source: News za redioni.

Sisemi kuwa AI itakupa majibu ila jaribu tu uone itasemaje, ukiona kuna jambo la tofauti na madaktari walichokuwa wanasema, nenda kawaonyeshe.
 
Habari wanajamvi, mwaka jana 2023 mwezi wa 3 nilianza kupata dalili ambazo sikuzielewa km vile; Kuvimba miguu, tumbo kuuma nk.

Ikabidi niende Amana hospital ambapo nilipima vipimo kadhaa ie, Moyo, Figo na Ini. Majibu yalipotoka ilionekana ini lina shida kutokana na enzymes ya AST (SGOT) kuwa juu sana kuliko inavyotakiwa kuwa lkn alipopima homa ya ini B ilisoma negative. Hivyo Dr aliyeniattend akaniandikia dawa/ Supplement zinaitwa LIVOLIN FORTE nitumie kwa muda wa mwezi mmoja kisha nirudi kucheki km AST imeshuka.

Nikafanya hivyo so niliporudi kucheki AST level ilikuwa imeshuka kutoka 51 hadi 48, Dr akaniambia niendelee kutumia miezi mingine mitatu mbele hadi AST ishuke kbs hadi <34.

Nikazingatia na niliporudi kucheki nikakuta AST level imeshuka hadi 36, Dr akasema umishapona na kweli zile dalili sikuwa nazisikia wala kuziona tena.

Lkn mwaka huu mwezi wa 3 nimeanza kuona na kusikia dalili zilezile za mwanzo, ikabidi nirudi tena Amana hospital na kupima Liver function test, majibu ni yaleyale AST level ni 36 ALT level iko normal na zile protini zingine ziko level. Dr akaniandikia tena LIVOLIN FORTE nitumie mwezi mmoja kisha nikae miezi mingine miwili ndo nirudi kucheki.

Lkn wakuu pamoja na kutumia hizi FORTE bado napata maumivu makali upende wa kulia wa juu wa tumbo lilipo Ini.

Sijui hata nifanyeje ndugu zangu msaada tafadhali.
Pole mkuu.
 
Kuna mama mmoja aliandika symptoms za ugonjwa wa mwanae uliomsumbua kwa muda mrefu sana kwenye AI,AI ikampa majibu, akachukua majibu na kuyapeleka kwa daktari wake, daktari akashangaa na kusema huenda hichi ndo kinachomsumbua mwanao kweli, mtoto akatibiwa akapona. Source: News za redioni.

Sisemi kuwa AI itakupa majibu ila jaribu tu uone itasemaje, ukiona kuna jambo la tofauti na madaktari walichokuwa wanasema, nenda kawaonyeshe.
AI kwa maana Artificial Intelligence ama umemaanisha nn mkuu
 
Sina mawasiliano alinitibu 2019 ni mda umepita na sim ilipotea ila ukienda pale Burhan we sema unataka kumuona Dr Kisanga watakwambia anapatikanaje au regency kimsingi anatibu kwa appointment
OK, shukrani
 
Back
Top Bottom