Mpauko
R.I.P
- Jan 19, 2019
- 2,323
- 3,428
Habarini ndugu zangu!
Nichukue nafasi hii kutoa dukuduku langu.
Mimi ni kijana wa kiume umri wangu ni miaka 24 sasa, naishi Mtwara mjini na ni Kiziwi(si wa kuzaliwa nilipata tatizo hli mwaka 2004 nikiwa darasa la tatu). Elimu yangu ni mhitimu wa ualimu grade A, 2018.
Kwa sasa najitolea kufundisha shule moja ya serikali hapa Mtwara For free. Ninaomba watanzania wenzangu kwa yeyote aliye na uwezo wa kunisaidia mnisaidie mtaji ili niweze kujiajiri.
Wazo langu ni ujasiriamali wa kuandaa vitafunwa na kuviuza mashuleni na wakati wa jioni kuviuza maeneo yenye mkusanyiko wa watu kama vile stendi pia kununua vifaa vya kufukuza mbu ambavyo hutumia umeme na viko mfano wa chaja ya kobe kwa vile huku ni nyumbani kwa mbu naamini nitapata wanunuzi.
Bajeti yangu katika mradi huu tshs100,000 naamini itatosha kunifungulia milango katika ujasiriamali huu.
SABABU ZA KULAZIMIKA KUOMBA MSAADA KWA WANAJAMII WENZANGU
Hali duni ya familia, haina uwezo wa kumudu milo mitatu kamilifu hivyo kusema ya kwamba haina uwezo wa kuniwezesha kuwa self employed
Ukosefu wa ajira na mtazamo wa jamii kuhusu wenye usikivu hafifu. Jamii haina imani kukabidhi kazi zao kwa kundi hili. Mwitiko hasi wa waajiri na mazoea ya wanajamii kwa kutowatilia maanani wasiosikia na mambo kadha wa kadha yamenifanya kushindwa kupata kibarua tangu nilipohitimu hadi leo sina kibarua kinachoniwezesha kutoa mchango kwa famiia yangu (ukizingatia umri wa miaka 24 huna cha kudai kwa wazazi tena badala yake wazazi ndio hukutazama wewe)
Malengo na hamasa, bila shaka kila mtu ana malengo na hamasa katika kufanikisha ndoto zake, kila mtu anapenda kufanya kazi na kufurahia matunda ya juhudi zake. Nakosa raha na amani sana kuona ya kuwa sina shughuli ya kufanya wala majukumu kulingana na rika langu.
Hitaji la kubadilisha mtazamo wa jamii.
Kwa kawaida jamii hutuchukulia kama watu dhaifu aghalabu kuona ikichukulia kama watu wasio na akili timamu. Binafsi ndugu wenye uwezo huniambia niende kijijini kumsaidia bibi kulima na kuchunga mifugo, they forget that nimekwishapita rika hilo napaswa kuweka mwelekeo wa maisha yangu sasa hizi ni dharau inaumiza sana!
Naamini kutoa ni moyo na sio kila atoaye ni tajiri, bali ni moyo, upendo na sense of humanity.
Naamini katika uzi huu hautowafurahisha wote hivyo niwaombe radhi wote watakaokwazwa na uzi huu.
Namba yangu ya Zantel ni 0776-741-545 jina EVARISTO MIHO(siyo jina langu natumia laini niliyopewa na mzazi yangu kutokana na kusubiri kitambulisho cha kura)
Asanteni.